Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

tunaita sin retribution.
Ukifanya dhambi utaikuta tu mbele, hilo hatukatai.

Ila wewe unawapa solution imperfect kwamba wao nao wajiingize kwenye uchaf pia nao waje waendelee kulipa gharama..

Yan unatengeneza catastrophic reaction which is endless but every action takes, triggers counter effect

Uovu unasafishwa kwa uchafu au uovu. Iko hivyo.

Ndio maana ukiua nawe unauawa.
Ukiiba únalipa kisha unafungwa .
Ukiwa mchawi unauawa

Huwezi safisha uovu pasipo kutenda uovu
 
Kuna baadhi ya mambo uko sahihi ila sio katika cheating kwa cheating.
Mapenzi sio vita kwamba piga nikupige, hayaendi namna hiyo. Na ukiona uko kwenye mapenzi ya aina hiyo basi hayo yenu sio mapenzi bali vita.

Anapaswa ajue kwamba akicheat atapoteza imani yangu juu yake, na kuirudisha sio rahisi. Na imani kwangu ndio mapenzi yenyewe, kiwango cha juu cha imani ndicho kiwango cha juu cha mapenzi.
Atakufanyia kuwa mnafiki na tapeli.
Kitendo cha imani kupotea hiyo itakufanya uwe tapeli

Alafu hii unatakiwa umwambie mapema mkiwa mnaanza
 
Uovu unasafishwa kwa uchafu au uovu. Iko hivyo.

Ndio maana ukiua nawe unauawa.
Ukiiba únalipa kisha unafungwa .
Ukiwa mchawi unauawa

Huwezi safisha uovu pasipo kutenda uovu
Hii sio tafsiri sahii..
Ukiua halaf ukamatwe ufungwe, sheria haihesabiki kama inakulipa uovu..

Kuna mambo unakosea kuyatazama ili uyaelewe.

Ndio maana ,ukiua, na mtu mwingine akakulipiza kwa kukuua wewe, bado na hawez kosa hesabiwa hatia.

Uovu haisafushwi kwa uovu. Never
 
Mwanaume Kumchiti Mkewe ni takwa la Kimila, Kidesturi na Kiutamaduni na pia ni Ushujaa sasa Wewe Mke wangu jichanganye Unichiti halafu GENTAMYCINE nijue ndipo utajua kwanini natokea Kanda Maalum ya Mkoa wa Mara ( Musoma ) na kwanini Wimbo wa Taifa huwa hauna Kolabo na kwanini Nyoka hana Ugoko.

Kudadadeki....!!

Huu ndio uonevu sasa.
Kudadadeki
 
MUMEO AKIKU-CHEAT NA WEWE M-CHEAT

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Najua wapo wanaume watanimaindi kwenye hii mada lakini hiyo ndio namna Watibeli tunavyofanya mambo yetu.
Hatuna msamaha kwa mtu anayefanya jambo kwa kudhamiria. Hiyo hatuna.

Kitu cha kwanza niliwaambia binti zangu kuwa hakikisha unajiweza, upo huru, unajitegemea na unaweza kujilisha wewe na watoto na mumeo(ikiwa mumeo ataumwa au itatokea dharura ya kimaisha). Niliwaambia msipende kuhudumiwa, wala kupenda vya bure ili muilinde furaha yenu.

Mwanaume kabla hajakuoa. Mpe misimamo yako. Mwambie mimi nipo tayari kujisalimisha kwako kama mkeo. Na nitakutii na kukusikiliza kwa kila jambo lililokuwa. Kwenye shida na raha tutakuwa wote lakini sio kwenye uovu na uasi.

Mwambie kabisa unamoyo mzuri lakini haimaanishi huwezi kutenda mambo mabaya na yakutisha kwa Watu wasiokuheshimu.

Mwambie siku atakayo-cheat ndio siku hiyohiyo ambayo utaandaa mipango kabambe ya kum-cheat. Mwambie kabisa kuwa hutamsamehe pasipo kumpa adhabu hiyo.
Ili aonje ule utamu alioufanya juu yako.

Mwambie yeye a-cheat kwa bahati mbaya lakini wewe utafanya makusudi. Mwambie yeye a-cheat kwa kujificha na kwa siri lakini wewe utafanya waziwazi bila kificho.

Mwambie kama anahitaji uaminifu wako itampasa naye awe mwaminifu.

Mwambie ndoa za Watibeli sio za kitapeli (dhulma) utakachokifanya ndicho utakachofanyiwa. Haki bin haki.

Akikuletea porojo sijui huwezi mkomoa Mwanaume zaidi ya kujikomoa mwenyewe mwambia naye hawezi kukukomoa wewe zaidi ya kujikomoa yeye mwenyewe.

Usikubali akuzalishe watoto ambao hautakuwa na uwezo wa kuwatunza hata siku asipokuwepo( iwe kwa kuachana au Kufariki) zaa watoto kulingana na uwezo wako wa kuwatunza. Kulingana na kipato chako.

Binti za Tibeli sio Wajinga. Usidai pesa za matumizi ikiwa mwanaume hataki kukupa hizo pesa huko ni kujishushia heshima na kujidhalilisha. Ikiwa ataichukulia hiyo kama faida au kuvuja kwa pakacha. Badilisha majina ya mtoto na mpe majina ya Watibeli.

Usiwe na moyo safi kwa mtu mwenye moto mchafu dhidi yako.
Usiwe na upendo kwa mtu mwenye chuki na wewe.
Usiwe na heshima kwa mtu mwenye kukudharau.
Usimpe mtu kipaombele ikiwa yeye anakuona wa ziada.

Ikiwa mumeo au mwanaume anapenda ndugu au wazazi wake kuliko wewe. Anakuweka nafasi ya pili au ya tatu. Wewe mweke nafasi hiyohiyo aliyokuweka. Hiyo ndio HAKI.
Ikiwa mwanaume amekuweka nafasi ya kwanza nawe muweke nafasi ya kwanza.

Usiwe mtumwa wa yeyote. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

Usifikirie maisha yatakuwaje ikiwa mtu anataka kukuacha iwe kwa kusema au kwa matendo yake. Huo ni utumwa.

Binti zangu msijesema Baba yenu sikuwaambia namna ya ku-deal na wanaume. Hivyo ndivyo mtakavyoishi kwa furaha. Kamwe usiwe mtumwa wa mtu mwingine hasa asiyemtumwa wako.
Kama mume au mwanaume anajitumikisha kwaajili yako nawe jitumikishe kwaajili yake.
Mpe kile alichopanda. Nawe usione shida kulipwa kile ulichopanda. Hivyo ndivyo mambo yalivyo.

Usiogope kuwa sijui atakupiga au atakuua. Usiwe mwoga kama nilivyokufundisha. Woga utakufanya uonewe. Ni bora akuue kuliko akufanye kuwa mtumwa wake.
Akikufanyia uhalifu wapo Watu wa haki watakaodili naye ikiwemo sisi Watibeli.

Acha Baba yenu nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ww dogo leo umeandika pumba.

Nyie wanaume wenye chembe chembe za ufeminist ndo mnakuja kuwa weak sana mwishowe na nyie mnapigwa paipu kama hao mnaowatetea.

Mwanamke ni object. Mm nikiwa na wanawake hata mia haina shida, ila mwanamke asili yake ni kuwa na mwanaume mmoja at a time.
 
😄 😄 😄
Daaaaah nimecheka sana! Sijasema akicheat nitamuacha, bali kupunguza kiwango cha imani ambayo ndiyo mapenzi yenyewe kwangu mimi.
Otherwise, no comment.
Kupunguza imani gradually kunaua mahusiano na mtu. In the end imani ita fade kabisa na kuzima mtaachana.

Bora kuzima mapema sio ku dim
 
Ww dogo leo umeandika pumba.

Nyie wanaume wenye chembe chembe za ufeminist ndo mnakuja kuwa weak sana mwishowe na nyie mnapigwa paipu kama hao mnaowatetea.

Mwanamke ni object. Mm nikiwa na wanawake hata mia haina shida, ila mwanamke asili yake ni kuwa na mwanaume mmoja at a time.

Utakuwa na wanawake mia wasiojitambua. Ila Watibeli ukileta hizo pigo laizma utakuwa mfano kama wengine wanaofanyiwa matukio ya kushangaza.

Unamuitaje mtu object? Huo ni ubinafsi.
Wanawake wanamatatizo yao lakini hawafanyi wawe object.
 
Hii sio tafsiri sahii..
Ukiua halaf ukamatwe ufungwe, sheria haihesabiki kama inakulipa uovu..

Kuna mambo unakosea kuyatazama ili uyaelewe.

Ndio maana ,ukiua, na mtu mwingine akakulipiza kwa kukuua wewe, bado na hawez kosa hesabiwa hatia.

Uovu haisafushwi kwa uovu. Never

Ni uovu gani usiosafishwa kwa uovu?
Ukifanya mabaya lazima ulipwe mabaya. Hiyo ndio kanuni.
Yaani uovu kwa uovu.
Wema kwa wema.

Unajua maana ya Haki?
 
Endelea kutamani.
Papa ameshapitisha lile tamanio lenu. Sasa yule aliyekuwa anakufumua sirini mwambie ajitokeze hadharani mambo yamejipa.
Dada yaani leo GENTAMYCINE nafumuliwa Sirini? Uko tayari kwa Vita nami na nianze kabisa Kusogeza Makombora yamgu Mipakani? Naona Umenibipu sasa Mimi nataka Nikupigie kabisa. Nasubiri jibu lako.
 
Back
Top Bottom