Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

I see. Habari ya muda hata mie nimekumiss. Ndio maana tunaambiwa baada ya msamaha enenda zako usitende dhambi tena. Sasa unaita hadi waandishi wa habari daahh
Mtu gani asiejuwa kusamehe mwenye chuki na mwenye kuhifadhi vitu moyoni mpaka leo miaka yote hiyo bado anasema amemkiri yesu
 
He took you and your unborn child in when no one else did.

He gave you and your child his last name. Provided for the child until The Angel of Death took him to heaven.

.... Am lost for words. 🙁🙁
Umeongea maneno matamu sana ingawa yana huzuni ndani yake, can you imagine biological father kamkataa mtoto however he came another man declare atafanya kila kitu kumchukua mtoto na kumlea na kumpa matunzo mtoto haijalishi eti leo in public unamkana tena na maneno juu ya kumkashifu peter hivi muna ana akili iliyotimia kweli? Casto tulimuona akipiga picha tu na mtoto kwenye mitandao lakini hamtunzi mtoto thats too selfish
 
Kesho tulikuwa tuende kumpa pole majirani hata siendi tena.hana adabu yule
Yule peter nae alichelewa kuoa ,kumuona huyo binti ndani ya mwezi ndoa wala hakumchangisha mtu.alikuwa na hela balaa.
Muna sio binti ni mbibi na ndio alikuwa analazimisha ndoa kwa peter
 
Sasa inasaidia nini kutangaza siri za ndoa yake?!
Kama ameokoka ukweli wake akatubu huko kanisani.
Hapa anampa nani faida?!
Nimemsikiliza huyo mwanamama,Mungu anisamehe na kama kuna ndugu zake humu pia watanisamehe nimegundua kichwani ni mtupu/mweupe/chenga.

Halafu kipindi hiki kuongea na waandishi wa habari imekuwa kama fashion, mtu anaona raha na ufahari kabisa.

Mtu ameshazika mtoto,watu wameshaacha kumsemea anakuja kuamsha tena watu waanze kumsema.

Kuna watu wanapenda sana kuzungumziwa,hapo alikaa akaona kasahaulika.

Nakumbuka nilisema hata ule ujinga waliokuwa wanafanya walifanya makusudi kabisa ili aendelee kuwa habari.
 
Muigiza Maarufu Bongo, Muna Love, amezungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuweka wazi jinsi ambavyo alikutana na Peter Zakaria Komu, mwanaume ambaye hivi karibuni ilisemekana kuwa ndiye baba wa mtoto wake Marehemu Patrick.

“Nilikutana na Peter jijini Mbeya tukiwa tunafanya kazi Safari Pool Table, tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi miwili tukaingia kwenye ndoa, lakini kuna vitu nilivyokutana navyo kwenye ndoa hiyo nikaamua kuachika.

“Wakati naingia kwenye mahusiano na Peter nilikuwa nina mimba ya Casto ya miezi miwili, Casto aliikana mimba hiyo. Baadaye alirudi wakati mtoto Patrick akiwa na miaka mitatu. Kwa sababu nilizaa nikiwa kwenye ndoa na Peter ndiye alisimamia hata ubatizo ndizo picha zilizosabaa, lakini hata yeye Peter anaujua ukweli kuhusu mtoto huyo.

“Tulifanya taratubu na Casto za kubadilisha jina la mtoto pale RITA lakini kuna ugumu uliotokea, lakini tulikuwa tunaendelea kufuatilia,” amesema Muna.
Kuishi na mwanamke kama huyu inataka ujitoe akili kweli kweli
 
Mara ya kwanza kusikia hili jina MUNALOVE ni wakati anasemwa kuwa kaiba chupi za Wema Sepetu sijui Muna alitaka kumvalia nani chupi za Wema kwanza zingemtosha?

Nadhani ni mwizi mwizi flani hivi amazing anaiba hadi sperms za casto kamgawia Peter tena kaiba mtoto kamgawia Casto akawaacha wote kaambatana na Joel kwenye bus hadi Nairobi kwenye matibabu ya mtoto wakati huo kumbe kapewa nauli ya ndege mara pesa za matibabu ya mtoto ndefu ndefu tuu amepiga piga pasi mtonyo wa matibabu yaani mwizi mwizi hadi kwenye sauti yake ukiaksililza kajizi kajanja janja haka kamama kumbe?

Sasa naanza kuamini bikini za Le Madame zilipitiwa na huyu mama asiye na soni. Pole mwaya Wema Sepetu kwa kukwapuliwa bikini hizi lazima zilikuwa brand za akina Alix or Amoressa [emoji13][emoji13][emoji13][emoji13]

Shame on you Muna unajiadhirisha mno
 
Katika hili sakata nimegundua mambo mawili makubwa;
1. CCM kweli itaendelea kutawala milele kutokana ujinga wa watanzania.
2. Mwanamke akiwa mjinga dunia inakua hatarini zaidi.
 
Tu assume mimba hajatiwa na huyo Peter, kitendo cha dada kuolewa na huyo baba Peter akiwa na mimba na baadae kuandika jina la baba Peter kwenye cheti cha kuzaliwa cha mwanae (ni kama alikubali Peter a adopt mtoto), na kumruhusu baba Peter kumlea mtoto kama mwanae kina halilisha Peter kuwa baba wa mtoto. Kitendo cha huyo dada kuwasiliana na baba Peter kuomba matumizi ya kuuguza mtoto ni kuhalalisha kuwa baba Peter alikuwa na jukumu la kulea mtoto.

Iweje mtoto aondoke duniani ndio aite press kukana kwa baba Peter sio baba wa mtoto? Hakuna mtoto anatolewa kwa adoption halafu akifariki uanze kusema huyu si mwanao ulim adopt tu. Anayelea mtoto ndio mlezi wa mtoto na ana haki za ubaba unless kuna makubaliano mengine.

Hata kama baba Peter aliongea na press kuaminisha yeye ndiye baba mtoto, huyo dada hakutakiwa naye kufanya hivyo, hana cha kuuaminisha umma. Two wrongs do not make a right. Kwa kukubali baba Peter asimame kama baba kwenye msiba wa mtoto ni kukubali kuwa baba Peter ndio baba wa mtoto. Kama mtoto alikuwa na baba wengine mbona hawakujitokeza kupigania damu yao? Haoni kama baba Peter ndie alikuwa na mapenzi ya dhati kwa mtoto? Kuwa baba sio kutia mbegu tu.

Watu walio karibu na dada huyu wampe elimu, kwamba kuwa baba sio kutia mimba. Na kwamba Peter ana haki zote kwa mtoto kama baba kwa vile mama wa mtoto alimpa haki hizo kupitia cheti cha kuzaliwa. Alitaka kumtumia baba Peter kulea wakati akiwa na dhiki ya maisha na alipopata akaona anaweza kulea mwenyewe (ambapo bado alisaidiwa na huyo baba Peter) akaanza kuona baba Peter si baba halali.

Hii habari ni private na sikutaka kuchangia ila kama wachangiaji wengine wanavyosuggest huyu dada pengine amechanganyikiwa na anahitaji kusaidiwa kimawazo na kuelemishwa na wanaomzunguka kuhusu maisha na malimwengu.

Ni kweli hakuna msafi wa kuweza kumhukumu kama ni mdhambi ama la, tunakosoana na kuelemishana. Hivyo tumwambieni dada ukweli, mtoto ni wa baba Peter no matter nani katia mbegu; tumkosoe kwamba alimwandikisha mwanae kwa jina la baba Peter, hivyo hana haki ya kusema mtoto ni wa mwingine hadi atuonyeshe vipimo vya DNA. Kwa sasa atabaki kusema mtoto sio wa huyu ni wa yule lkn kimantiki mwenye haki na mtoto ni aliyemhudumia tangu akiwa pande la damu tumboni hadi anafariki.

RIP mtoto mzuri.
 
safi Muna na hongera kwa kuutua mzigo Patric atakuwa na amani huko aliko
hongera gani mwanamke analaana huyo huwezi kudanganya mtoto baba yake mpka ndugu wanaenda kumzika wakijua ni damu yao kumbe la...halafu anadiriki kuanika mambo hadhalani vile...akilini hamnazo yule...hata ajifanye kaokoka dhambi itamtafuna hio yeye na malaya mwenzie castrol sijui...
 
mnh,kuna kitu kinaitwa assertive tactics in impression management..

msimcheke muna, labda na nyie mngekua kama yeye,mngefanya the same...

desperate need to repair image ambayo imekua tarnished,

pole Muna,mie nakuelewa unachofanya,

ila ,

iwe mwisho kuwasiliana na waandishi,

unamwaga petrol kwenye moto tayari…

wataendelea kukusema tu..

wanadamu wabaya..

watavunja ndoa yako for real
hana akili anaolopoka kama toto hv..yani mademu wa bongo bana..
 
hongera gani mwanamke analaana huyo huwezi kudanganya mtoto baba yake mpka ndugu wanaenda kumzika wakijua ni damu yao kumbe la...halafu anadiriki kuanika mambo hadhalani vile...akilini hamnazo yule...hata ajifanye kaokoka dhambi itamtafuna hio yeye na malaya mwenzie castrol sijui...
nafikiri wengi tunachoshindwa kuelewa ni kwamba Peter alikuwa anajua kuwa yule si mtoto wake si kwamba slidanganywa kosa la Muna lilikuwa kukubali mtoto apewe ubini wa Peter hilo tu ndo lililomfikisha Muna hapa.
 
Mtoto wa nje ya ndoa anahesabika kuwa ni mtoto wa mama na si mtoto wa baba, ni hayo nkoi..

Kwa theory yako mtoto si wa Peter wala wa Castor. Angesema mtoto ni wake hakuna angeshangaa. Kinachoshangaza ni yeye kusema mtoto si wa Peter bali ni wa Castor.

Hawa wana ndoa wamalize tofauti zao kwa kuvunja ndoa au kurudiana.
 
Dah......Baba yangu kila siku ananihubiria mwanangu kwenye maisha kosea yote unaweza kusimama na kuendelea hila usikosee kuoa maana utapata tabu sana sasa ndio nayaona kwa huyu dada
 
Alieanza kumpiga P ndo mwenye mtoto...case closed.
 
Back
Top Bottom