Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
Kaka mmoja anaishi Ughaibuni, alikuja likizo nyumbani. Siku moja akiwa matembezini alikutana na kijana wa miaka 15-16 amebeba mtoto mdogo wa mwaka mmoja. Mtoto yule alikuwa anaumwa sana. Yule kijana alikuwa anatafuta usafiri wa kwenda Mwananyamala hospital. Daladala zikiwa zimejaa na kijana akiwa na mtoto mdogo.
Kaka wa diaspora alimuita yule kijana akamwambia wachukue taxi, walikuwa ndani ya taxi yule kaka alimwambia taxi driver tupeleke Aga Khan, walifika Aga Khan kuandikisha kadi tu ilikua 40,000. Mtoto alionwa na madaktari, alikuwa na malaria kali sana. Walilazwa pale kwa siku tatu. Kaka diaspora alikwenda kuwajulia hali kila siku.
Yule kijana anaishi kwao na wazazi wake. Mtoto ni wa dada yake ambae aliamka asubuhi kwenda kazini. Wazazi walikwenda shambani Mkuranga. Akijaribu kumpigia simu dada amfahamishe hali ya mtoto dada hapatikani.
Mama yake aliporudi jioni alifahamishwa kuwa mwanae yuko Aga Khan, aliwaza hizo gharama. Amefika pale aliambiwa muuguze tu mtoto usijali malipo.
Baada ya kuruhusiwa kutoka, familia ilimkaribisha kaka diaspora chakula na kumuombea dua nyingi kwa ukarimu wake.
kaka diaspora anasema aliwaza kuokoa maisha ya mtoto na aliona Aga Khan ni karibu kuliko Mwananyamala kwa hiyo sehemu waliyokuwa.