Nadhani nami pia nahitaji elimu zaidi juu ya malimwengu (galaxies)
1. Tofauti ya universe, galaxy, constellation, star, some sort of those nebula and star dusts ni kipi na kipi siyo kipi.
Universe ni kila kitu (Galaxies+Nebula+planets+blackholes+Everything).
Galaxy ni kundi la nyota zinazoorbit kwenye plane moja(galaxy nyingi zina nyota nyingi sana mabillioni kwa matrillioni).Mfano wa galaxy ni hii tunayoishi inaitwa milkyway.
Constellation ni nyota ambazo zinaunda shape fulani ukiziangalia kutokea duniani..Mfano kuna nyota zina shape ya nge wanaita scorpion constellation, Lakini kiuhalisia unaweza kukuta nyota ya kichwa cha nge na nyota ya mkia wake zimeachana umbali wa lightyear hata 1000(haziko pamoja)..Constellation zote tunazoziona zipo ndani ya galaxy yetu ya milky way.
Nyota ni body angani inayotoa mwanga kwa kuunguza gesi zake.
Nebula ni wingu kubwa la vumbi au gesi angani, mara nyingi huwa ni gesi au vumbi zinazopatikana baada ya nyota kufa.(stardust)
2. Ni kweli Milky way Galaxy (njia ya maziwa ndiyo seven sisters constellation (kilimia)?
Si kweli...constellation zipo ndani ya galaxy.
Ukielewa jibu la hapo juu hii inajieleza
3. Our universe ( Milky way Galaxy) with 9 planet (entirely solar system) including our home Earth is the same to kilimia (seven sisters constellation)
Ukielewa jibu la kwanza hili swali halimake sense.
4. Je hiyo Orion/Lion (Simba mwindaji) constellation iko hapa kwenye solar system au iko kwenye galaxy nyingine km vile spiral galaxy, au Andromeda ( our neighboring galaxy?
Ipo kwenye milky way, Constellation zote zipo milky way..Yaani nyota zote tunazoziona angani hazizidi 6000 tu. Lakini milky way ina nyota billioni 100-400
5. Je kuna ulimwengu/malimwengu/ universe ngapi? Na kila universe is it equal or same as galaxy or equal to constellation or star?
No one knows.
Lakini kuna kitu kinaitwa observable universe..Yani sehemu ya ulimwengu inayoonekana.
Hiyo sehemu ya ulimwengu inayoonekana ina galaxies kama milkyway zaidi ya trillioni 2
Na hapo bado kuna unobservable universe, yani ile sehemu ya ulimwengu ambayo mwanga wake haujafika duniani na hautakuja kufika kwasababu ulimwengu unapanuka fasta kuliko spidi ya mwanga.
Na inaaminika ulimwengu ambao hatuuoni ni mkubwa kuliko tunaouona wenye galaxies trillion 2.
Lakini swali la je, ulimwengu una mwisho? Upo mmoja? Hayana majibu..No one knows.
6. Vipi kuhusu makundi nyota hizi (constellation) dubu, nge, vigor, msalaba wa kusini, Orion vs Betelgeuse (the giant star in constellation) , kilimia nk?
Yote yapo katika hizi nyota 5000+ tunazoziona kwa naked eyes hapa duniani. Zote zipo milky way, tena huu upande tuliopo sisi, kasehemu kadogo sana.
7. Je Orion vs Betelgeuse deep hole concerp of heaven place ikoje boss?
Hizi ni story za kufikirika hazina ushahidi wowote. Ni changamsha genge la kanisa au kijiwe cha gahawa tu.
Mi sijakupata Mzee baba naomba ongeza nyama kwenye huu Uzi km bado upo kwenye hili jukwaa.
Ahsante sana