Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya mvua

Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya mvua

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
7,893
Reaction score
8,816
Ahsante Mungu kwa kusikia na kujibu maombi yetu ya kuomba mvua. Nimeshuhudia mvua zikiendelea karibu maeneo yote ya kanda ya ziwa.

Mkoa wa Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Musoma, Sumbawanga n.k mvua inamwagika. Sijui maeneo mengine.

Tuendelee kumuomba Mungu.
 
Mwenyezi Mungu anawashushia mvua viumbe wote wanao omba wasio omba hii ni neema yake ndio maana hukuti huko UK wakiomba mvua ila wanashushiwa mpaka wanachukia mvua. Mungu katupa majira usiku, mchana, kiangazi na masika sasa unakuja unaomba mvua wakati wa masika? hao wanafiki wakaombe kiangazi mvua halafu tuone kama itanyesha. Ni kama kuomba jua mchana ukasema dua limekubaliwa.
 
Tunajipangaje kama familia, jumuiya, wilaya, mikoa na Taifa katika upandaji wa miti mingi na ya kutosha kufidia miti mamilioni ambayo imekatwa na inaendelea kukatwa ili kutusaidia sisi na hata vizazi vyetu?
 
Ahsante Mungu kwa kusikia na kujibu maombi yetu ya kuomba mvua. Nimeshuhudia mvua zikiendelea karibu maeneo yote ya kanda ya ziwa.

Mkoa wa Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Musoma, Sumbawanga n.k mvua inamwagika. Sijui maeneo mengine.

Tuendelee kumuomba Mungu.
Hivi ninyi watu huangalia ama kufuatilia weather forecast kweli?
 
Jana hapa mafinga nimeangukiwa na matone mawili. Its a good sign inshallah
Uliangalia juu kuthibitisha ni matone ya mvua?

Nasema hivyo kwa maana hapo mafinga hiyo jana kunguru wengi walitanda angani
 
Tanga sasa [emoji1][emoji1]

Jua limeshuka chini [emoji119][emoji119]
Bukoba nayo anga imefunga, wingu zito la mvua, mwanza Shinyqnga, Tabora anga imefunga kwa wingu zito la mvua.
Asante Mungu.
 
Uliangalia juu kuthibitisha ni matone ya mvua?

Nasema hivyo kwa maana hapo mafinga hiyo jana kunguru wengi walitanda angani
Ndiyo mkuu jana mchana mida ya saa sita mawingu yalitanda. Lile jua sahv halipo angalia hata sasa mawingu tu. Inarudi hali tuliyoizoea
 
Hivi ninyi watu huangalia ama kufuatilia weather forecast kweli?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
unadhani huo utabiri wa hali ya hewa (weather forecast) una uhakika kuliko kudura za Mungu?

utabiri ni jambo moja na kudura za Mungu ni jambo jingine.

huo utabiri pia unategemea majaaliwa ya Mungu.

wao wanatabiri tu lkn muamuzi wa yote ni Mungu.
 
Mwenyezi Mungu anawashushia mvua viumbe wote wanao omba wasio omba hii ni neema yake ndio maana hukuti huko UK wakiomba mvua ila wanashushiwa mpaka wanachukia mvua. Mungu katupa majira usiku, mchana, kiangazi na masika sasa unakuja unaomba mvua wakati wa masika? hao wanafiki wakaombe kiangazi mvua halafu tuone kama itanyesha. Ni kama kuomba jua mchana ukasema dua limekubaliwa.
inashangaza maombi ya kuomba mvua yanaitishwa wakati ni msimu wake, huko ni kumsumbua Mungu, na hajibu hayo maombi yasiyo na maana kwani mvua hunyesha kwa wakati wake
 
Back
Top Bottom