Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya mvua

Mungu ameanza kujibu maombi yetu ya mvua

Tunajipangaje kama familia, jumuiya, wilaya, mikoa na Taifa katika upandaji wa miti mingi na ya kutosha kufidia miti mamilioni ambayo imekatwa na inaendelea kukatwa ili kutusaidia sisi na hata vizazi vyetu??
Sipati picha kama Mbowe angekata na miti ktk mikoa Tajwa huenda mvua zisingenyesha mpaka kikao cha bunge la bajeti 2022,

Cc Kingai Mbowe sio" Tourist "kama msemavyo
 
Tabora, Nzega, Igunga imetandika kisawa sawa.
 
Babu kama una imani juu ya Mungu basi utakuwa umenielewa nilicho kisema.
kinyume cha hapo itakuwa vigumu kwako kunielewa.

Nimekuelewaje, kama maombi yangekua yanasaidia hakuna nchi ingekua inakosa mvua
 
Maombi yameanza kujibu Dar.
mvua nzito inaendelea kumwagika mchana huu wa leo trh 27/11
Asante sana Mungu wetu wa mbinguni kwa huruma yako kwetu sisi.
 
Ahsante Mungu kwa kusikia na kujibu maombi yetu ya kuomba mvua. Nimeshuhudia mvua zikiendelea karibu maeneo yote ya kanda ya ziwa.

Mkoa wa Mwanza, Geita, Shinyanga, Kigoma, Musoma, Sumbawanga n.k mvua inamwagika. Sijui maeneo mengine.

Tuendelee kumuomba Mungu.
Kweli Mungu amesikia maombi ya waja wake, hapa Kibaha Pwani tumepata mvua kubwa.
 
maombi ya mvua hujibiwa siku hiyohiyo au baada ya maombi kwa siku 3 ukiona zimepita ujue maombi yenu hajakubaliwa mvua unayoiona sasa si kwa ajili ya maombi yenu
 
Mungu katika kuwaruzuku na kuwapa neema viumbe wake hasubiri kuombwa kwanza hao mnaowaita viongozi wa dini ndio wanaoongoza kwa madhambi na kumkufuru mwenyezi Mungu.
 
Hakika, hata nilipokua muda huu mvua imenyesha sana...
 
Coincidence tu...Huu ni msimu wa mvua.
kwa maeneo ya Pwani msimu wa Vuli umepita na hapakuwa na Mvua, kwa faida tu ni kwamba mvua za vuli ktk maeneo ya Pwani huanza mwezi Agosti na kuisha mwezi Octoba, lkn safari hii hakuna kitu mpaka leo hii trh 27 ndio tumeshuhudia mvua kubwa.
Mungu Ashukuriwe kwa uwezo wake.
 
Tunajipangaje kama familia, jumuiya, wilaya, mikoa na Taifa katika upandaji wa miti mingi na ya kutosha kufidia miti mamilioni ambayo imekatwa na inaendelea kukatwa ili kutusaidia sisi na hata vizazi vyetu?
Yaani ukataji miti na umasikini ni sawa na pipa na mfuniko!!juzi namuona mkuu wa mkoa wa songwe eti anapiga marufuku kuchoma mkaa ndani ya mkoa wake!!!kweli kwa maisha yetu haya hili linawezekana kweli??haya magereza yote nchini bado nishati wanayotumia kupikia ni kuni, yaani kule hadi miti mibichi inayotoa utonvu inapikiwa hadi inaivisha chakula!!!
 
Halafu watatokea wapuuzi na kutuambia maji yemepungua kwenye mabwawa.
 
Yaani ukataji miti na umasikini ni sawa na pipa na mfuniko!!juzi namuona mkuu wa mkoa wa songwe eti anapiga marufuku kuchoma mkaa ndani ya mkoa wake!!!kweli kwa maisha yetu haya hili linawezekana kweli??haya magereza yote nchini bado nishati wanayotumia kupikia ni kuni, yaani kule hadi miti mibichi inayotoa utonvu inapikiwa hadi inaivisha chakula!!!
Ndio maana naona tuna haja sasa ya kuwa na nia ya dhati kwa vitendo kuanza kureplace hayo mamilioni ya miti ambayo imeshakatwa na itaendelea kukatwa mpaka hapo tutakapo pata mbadala kama upo.

Zoezi liwe endelevu kila mwaka. Tukijiwekea malengo ya kupanda miti Billioni 10 nchi nzima ndani ya miaka 5.
 
Dar es salaam tumeongeza maombi!
tayari maombi yamejibu, anga limebadilika wingu la mvua nzito limetanda anga la Jiji, mvua inamwagika ya kutosha jana na leo trh 28/11
ukame wa jua kali itatoweka kabisa.
 
Back
Top Bottom