"Mungu anaangalia roho haangalii mavazi" ni kauli inayohamasisha mmomonyoko wa maadili. Wakristo tuwe na msimamo juu ya mavazi kanisani

"Mungu anaangalia roho haangalii mavazi" ni kauli inayohamasisha mmomonyoko wa maadili. Wakristo tuwe na msimamo juu ya mavazi kanisani

Huu utamaduni umekuwa ni cancer kwa ukristo maana baadhi ya waumini waliozoea kuvaa hovyo wakienda kuanzisha makanisa yao wanachafua ukristo, Mtu kama Masanja anavaa kata k / Mlegezo / Suruali chini ya ma*****
Masanja sio mchungaji usihangaike nae
 
NB: mods nawaomben msihamishe huu uzi jukwaa,kuuedit,au kutoa kipande chochote kile, kwa niloandika, Kuna funzo kubwa sana hapa kuzuia kasi ya mmomoo wa maadili (Moral Decay) ambao unazidi kumea.

ni jukumu letu kama wakristo kujaribu kukumbusha waumini juu ya wajibu wao kuvaa mavazi yanayositiri, hili likipuuzwa litafanya makanisa yawe sehemu ya kuongeza ufuska, hapo zamani sheria kama mwanamke asivae nguo za wanaume hususani suruali zilizingatiwa na yeyote aliekiuka aligeuzwa mlangoni, lakini sasa hali imebadilika.

Mfano mimi kwa jumapili iliyopita ya ppasak niliweka mkasa nilipoenda kumpa kampani na kusikiliza neno kanisa flani ambalo lina waumini wengi hata duniani lakini nilichokutana ni mabinti kuvalia suruali, nilishangazwa kuambiwa kinachoangaliwa ni roho, moja wao nilimpiga picha hii hapa.
img_20230409_120124-jpg.2582156

Hawa wenzetu wachache wa jumamosi naona kwao suala la mavazi hawataki masikhara na kwa hili wamefanikiwa kwa kuendelea kukazia maandiko, hata iwe suruali pana utapigwa stop mlangoni! ishu iliyopo ni makanisa mengine hasa kkkt, katoliki na kwa walokole, hali ni mbaya kiasi kwamba unaona kama vile nayo makanisa yanaenda na mabadiliko ya utandawazi hata kwa mavazi (hapo zamani ukivaa ovyo unafukuzwa)

Huku mitaani tunaweza kuvumiliana lakini yatupasa tujue nyumba yoyote takatifu inabidi mtu asiende kwa namna yoyote ambayo inakera wengine ama kuwatia wengine majaribuni hasa katika mavazi

JE KAMA MUNGU HAANGALII MAVAZI ANAANGALIA ROHO, HAYA MAVAZI NI SAWA ?

View attachment 2585387
View attachment 2585391

View attachment 2585393

View attachment 2585392


PAMOJA TUUNGANE KUZUIA MMONYOKO WA MAADILI
Hayo mavazi yote hapo inategema na context, sitegemei aliyeko ufukweni , ama aliyealikwa dinner avae suti, hapana:
wote wapo sahihi kwenye mazingira yao:
suala la mavazi ya kanisani ni mtambuka, wapo wanaovaa madera marefu mpaka mguu unafunikwa na kilembe juu, ndani anavaa chupi tu bila andasketi na dera ni transparent unaona milima na mabonde kama mungu alivyoumba na kuna anayevaa nguo fupi lakini huoni ndani.

Wapo wanaovaa dera na kwakuwa ni refu anachomekea kwenye chupi, hii unasemeaje?
Sema tu skin tight ni nguo za kulalia ama michezo ila wadada wanavaa mtaani na kuwamiza wanaume roho .
 
... hapo zamani sheria kama mwanamke asivae nguo za wanaume hususani suruali zilizingatiwa na yeyote aliekiuka aligeuzwa mlangoni, lakini sasa hali imebadilika.
Ni wapi imeandikwa kwamba suruali ni nguo ya mwanaume?
 
Kuna zingine apo juu mtu akiingia hivyo ibadani ata malaika akija kuchukua maombi anaingia katika vishawishi "utani"

Siyo suruali tuu kuna magauni special na yakushona pia hayafai kuingilia ibadani hadi kunasiku nilimwambia jamaangu ingependeza kama kungekuwaga na vazi rasmi la kuingia ibadani
 
Ni wapi imeandikwa kwamba suruali ni nguo ya mwanaume?
MSAHAFU inasema wanawake wavae nguo za kike na wanaume wavae za kiume, wewe unaweza kuvaa bikini? Itaweza kuzuia dushe likae vizuri?

Mwanamke anaweza kuvaa boxer? kama yupo kwenye MP boxer inaweza kushikilia pedi?
Acheni ushamba namambo ya usasa , mrudie muumba.
 
Mwanamke anaweza kuvaa boxer? kama yupo kwenye MP boxer inaweza kushikilia pedi?
Kwani pedi zinavaliwa muda wote? Zinavaliwa umri wowote? Adam na Eve walipojiundua wapo uchi walijisitiri kwa kuwaa majani, Je, majani ni mavazi ya kiume au ya kike?
 
Kwani pedi zinavaliwa muda wote? Zinavaliwa umri wowote? Adam na Eve walipojiundua wapo uchi walijisitiri kwa kuwaa majani, Je, majani ni mavazi ya kiume au ya kike?
Mwanamke anavaa sketi akikoja apandishe juu kwakuwa lazma achchumae, hivi unavyongangania kuvaa nguo za kiume huko chooni huwa unakojoa umesimama?

Ushaona mwanaume akingangania kuvaa nguo za kike?
 
Wasabato, mashahidi wa Yehova pia wakatoliki kwa mbaali kidogo uzingatia suala la mavazi kwingine huko wanaogopa sadaka zitapungua. Haya christianity science church yaani makanisa ya kizazi kipya hali ni mbaya kabisa kwenye mavazi, muhimu sadaka tu.
Hakika RC Church na Sabato ndiyo makanisa angalau yaliyobaki katika misingi ya Imani Thabiti na Misingi ya Ukristo. Haya mengine yamekuwa ni vurugu tu hasa Lutheran, Anglican na Moravian yamekuwa ni makanisa ya matamasha na kuhubiri mafanikio ya kidunia, na ndiko waumini wengi huvaa mavazi ya ajabu sana. Na hili wimbi la wahubiri wanaoanzisha makanisa ya Kinabii, uamsho, ufufuo na uzima na hawa wanaotusumbua na maspika mitaani wengi wametokea Lutheran na hayo mengine. RC na SDA yatabaki kuwa ni makanisa ya kweli na waumini wao huwa hawayumbi katika misingi yao
 
Mwanamke anavaa sketi akikoja apandishe juu kwakuwa lazma achchumae, hivi unavyongangania kuvaa nguo za kiume huko chooni huwa unakojoa umesimama?
Nguo za kiume ndio zipi? Hiyo ni kwa mujibu wa sheria gani? Ni akina nani walikaa wakaweka makubaliano kwamba nguo za kiume ziwe hivi na za kike ziwe hivi?
 
Back
Top Bottom