Mungu anaangalia roho sio mavazi, Makanisa muwaachie dada zetu kuwa huru kuvaa wanavyotaka, hata vipensi ni mavazi, tunachoangalia ni roho

Mungu anaangalia roho sio mavazi, Makanisa muwaachie dada zetu kuwa huru kuvaa wanavyotaka, hata vipensi ni mavazi, tunachoangalia ni roho

Agano la kale lilipitwa na wakati, tupo agano jipya, tunakula hata kitimoto kilizokatazwa kwenye sheria za agano la kale.

Wadada wavae wanavyotaka, makanisa yasiingilie
Lilipitwa lini na wakati
 
Maandiko yapo wazi kabisa Mkristo avaaeje.
Mwanamke apaswi kuvaa mavazi ya mwanaume.
Hata nchi za baridi utasingizia baridi lakin hekima suruali isionekane avae ndani ya gauni
Maandiko haya ambayo yamekataza wanaume kuchonga nywele na ndevu ?

Mbona wachungaji karibu wote wanachonga ? ni kwasababu yalipitwa na wakati
 
Maandiko haya ambayo yamekataza wanaume kuchonga nywele na ndevu ?

Mbona wachungaji karibu wote wanachonga ? ni kwasababu yalipitwa na wakati
Pana Wakristo wa kiroho na pana Wakristo wa kimwili
 
Mavazi ni roho kamili mavazi usema kuhusu tabia ya Mtu.
Asiye na heshima katu hawezi Vaa mavazi ya heshima
 
Ulisema kinacho angaliwa ni Roho. Nami nimekupa hilo fungu.

Kuhusu Mavazi.

1 Timotheo 2:9-10.

9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
Mngekuwa mnafuata haya maandiko msingikuwa hivyo mlivyo...

WAKRISTO wengi ni wajasiriamali dini wakiongozwa na viongozi wao...
 
View attachment 2771650

Hapo zamani nilishuhudia kwa macho yangu makanisa yalikuwa na tabia za ajabu kuwavisha kanga wanawake waliokuja wamevaa sketi zilizobana kwa mbali, waliovaa suruali hata ziwe pana walifukuzwa kabisa kurudi nyumbani.

Tunashukuru kadri muda umeenda makanisa yamejitambua, Leo hii wanawake wanaruhusiwa hata kuvaa suruali, gauni zinazowachoresha ili wapendeze, gauni zenye uwazi wa kupitisha hewa vifuani na mgongoni, n.k.

Kero kubwa ipo kwa makanisa kujitungia sheria za kukataza vimini na vipensi, huu ni ubaguzi !! Wadada wavae wanavyotaka, makanisa yasiingilie.

Sheria za agano la kale zilishapitwa na wakati, sheria za aina ya mavazi na makatazo ya kuchonga nywele zilishapitwa na wakati na tunajionea hata wachungaji wanachonga nywele, Nazo sheria za vyakula zilishapitwa na wakati kuna uhuru wa kula kitimoto.
Ivi kuna mwanaume anaenda na kipensi ofisini au hata nyumba za ibada?

Bila ya shaka jibu ni NO

Kwaio yeyote yule anaevaa uchi ni rafiki wa shetani na anaitangaza zinaa hadharani

N.b.Uzinzi haujawahi kumuacha mtu Salama
 
Mngekuwa mnafuata haya maandiko msingikuwa hivyo mlivyo...

WAKRISTO wengi ni wajasiriamali dini wakiongozwa na viongozi wao...
Wewe unasema wakristo?

Shetani kaingia kotekote. Keshajitwalia hadi Misikiti, Temple, Sinagogi..

Siku hizi mashehe wewe wanagawana sadaka kama posho tu.
 
Wewe unasema wakristo?

Shetani kaingia kotekote. Keshajitwalia hadi Misikiti, Temple, Sinagogi..

Siku hizi mashehe wewe wanagawana sadaka kama posho tu.
Shehe gani anatembea vie8 au Corora!! Ukiacha na mufti .Sisi hatuna mbambamba nyingi ukila Hela ya waumini utaitapika mapema tu.
 
sasa kwanini wa kulia asiruhusiwe kuingia kanisani kama sio unafki wa makanisa ?
Mlevi na mnywaji wana hadhi tofaut.
Lile kanisa la Grace angeeingia bila shida kwa makanisa ya mungu anaangalia roho anaweza ingia.
Yule wa kushoto aliyeusitiri mwili lakin umechora umbo angalau lakin Sio kwa makanisa ya kiroho
 
Vazi limemchora matak* makubwa, hips pana na mapaja makubwa, kuna usitiri gani hapo ?
 
Sawa, tumekusikia Mungu haangalii Mwili. Kama ni hivyo, isiwe kanisani tu iwe na msikitini pia. Shauri na Waislamu nao au huko Mungu anaangalia mwili. Pumbavu kabisa wewe.
 
Back
Top Bottom