Mungu anaongea na watu mara nyingi. Wengi hawaelewi kwa sababu ya ujinga wao wa mambo ya kiroho

Mungu anaongea na watu mara nyingi. Wengi hawaelewi kwa sababu ya ujinga wao wa mambo ya kiroho

Mandela5599

Member
Joined
Jul 28, 2020
Posts
93
Reaction score
306
Mungu ni roho, Mungu anaongea kiroho


Haongei kama sisi wanadamu, ana namna zake ambazo ni muhimu uzifahamu


KUNA NJII KUU 3 ZA MUNGU KUONGEA NA WEWE


1. KUPITIA NDOTO/MAONO


2. KUPITIA NENO LAKE. Biblia Takatifu


3. KUPITIA WATUMISHI WAKE(MANABII, WALIMU N.K

LEO TUONE NJIA YA NDOTO

Ndoto zimegawanyika katika makundi makuu matatu kwa mujibu wa maandiko

i) Ndoto zitokazo kwa Mungu... mtu yeyote awe mbaya au mwema anaweza kupata ujumbe kwa Mungu

ii) Ndoto zitokanazo na shughuli nyingi. Baada ya kazi nyingi akili inaweza kurudia baadhi ya matukio unayo kutana nayo.. ndoto hizi hazina madhara

iii) Ndoto zitokazo kwa shetani. Hizi mara nyingi ni mashambulizi, zinaleta hofu, mashaka na kukukosesha amani

Kuna watu wanarithishwa uchawi au uganga kupitia ndoto na baada ya hapo wanaanza kazi. Hizi ni ndoto za shetani

Tafsiri ya ndoto haitoki kwa wanadamu, inatoka kwa Mungu.

Kutafsiri ndoto sio issue sababu hata waganga wa kienyeji hutafsiri ndoto... what matters ni kutoa maelekezo au miongozo yakufuata. Waganga kamwe hawawezi kukupa mwongozo sahihi wa nini chakufanya... Muombe Mungu atakuelekeza cha kufanya

Watu wengi wanaota wakiwa shule, wakifanya kitihani wakati walimaliza shule siku nyingi

Watu wengi huota wakiwa vijijini kwao waliko zaliwa, wakati wako mjini...mara nyingine inatokea wakati hujapakumbuka kabisa kijijini kwenu

Kuota umelala na mwanamke/mwanaume bila ridhaa yako na ukiamka unajiskia vibaya sana

Hizo ni baadhi ya ndoto ambazo huwatesa wengi na hawajui wafanye nini.

Tutaendelea siku nyingine
 
Back
Top Bottom