Nadhani hatujaelewana, wewe haya unayoyaeleza kuhusu huyo mungu wako unadai kuwa umeyapata kutoka kwa hao watu wa mwanzo kuumbwa ila nachouliza mimi hapa kwanini na sisi tusiyajue hayo ya huyo mungu kwa njia kama iliyotumika kwa hao watu wa kwanza ambayo ni kupitia miujiza ya uumbaji? maana umesema uumbaji bado unaendelea ila ajabu watu hawapati hiyo elimu ya kumjua huyo mungu kupitia huo uumbaji na matokeo yake tunategemea masimulizi ya hao watu wa mwanzo tu.
Labda Ndugu yangu Wewe ndio hutaki kunielewa mwenyewe. Ni sawa na Mimi nikuambie Hivi. Kama Adam aliweza Kuongea na Mungu kwanini Sasa Hivi Haongei na Wanadamu.? Au Haongei na Wewe hapo ili akufundishe ila Unaenda Kusikiliza mafundisho Kanisani au Msikitini
Nimekuambia hapo Juu Elimu ya Jadi na Wazee wetu ilitoka Kwa Mwanadamu wa Kwanza Fumbakasa na Mkewe. Maana Binadamu ndio tunaongea sisi kwa Sisi na Kufundishana Yeye aliipokea Kutoka Kwenye Muujiza wa Mungu.
Ni sawa na Wewe upo Darasani unafundishwa na Mwalimu huwezi kuanza Kuuliza kwamba Namtaka Mwalimu aliyemfundisha Mwalimu wako. Au unataka Wakoloni wa Kizungu ndio waje Kukufundisha ndio Utaelewa kwamba elimu imetoka Kwao.
Mbona Biblia unayoamini au Kitabu chochote kile hukuwahoji kwamba Mbona Mungu haongei na Sisi Kama Alivyoongea na Adam na Hawa ndugu yangu
Nimekwambia hivi ukiondoa hayo ya sadaka na kuchinja bado watu huomba dua pasipo kutumia sadaka wala kuchinja, hilo unalizungumziaje?
Sasa Unaendaje kinyume na Maelekezo uliyoambiwa Na Mungu wako ufanye. Utakuwa unafanya Dua zako Na kumuabudu Mungu mwingine sasa. Mungu wa Kwenye Vitabu kakuambia Niabudu Hivi chinja na Fanya Hivi na Hivi na Umjaribu kwa Sadaka wewe unasema Unaomba Bila Sadaka Ndugu yangu. Huoni kwa Akili ya Kawaida unafanya Ibada yako mwenyewe
sasa wewe umekazania issue ya sadaka na kuchinja tu.
Siyo nakomalia Ndugu si Ndivyo Mungu kaelekeza Umwabudu hivyo. Utoe sadaka na Uchinje wanyama bila Hivyo Kuvifanya Wewe unafanya Ibada zako mwenyewe Na Huna Haja ya Kwenda Kanisani Kuabudu wala Msikitini kaa Nyumbani tu ndugu yangu maana Unakuwa Hufuati Maelezo ya Mungu
Kasome Haya Maandiko Ujue Muongozo wa Kusali na Kama Unaposali kwa Mungu unatakiwa Kujua anataka Nini Ili Akusamehe na Kukubariki maana Ndio maagizo yake hayo
Walawi 7:1 na Kuendelea
“Ufuatao ni mwongozo wa ibada kuhusu sadaka ya kuondoa hatia. Sadaka hiyo ni takatifu kabisa.
Malaki 3:10 na Kuendelea
Leteni ghalani mwangu zaka yote, ili nyumbani mwangu kuwe na chakula cha kutosha. Kisha mwaweza kunijaribu. Nijaribuni namna hiyo nanyi mtaona kama sitayafungua madirisha ya mbinguni na kuwatiririshia baraka tele........
Hayo ndio Maelekezo ya Kwenye Biblia unayoiamini Usipofanya hivyo Ujue Unafanya Ibada zako tu