Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Hiyo ni phrase , Mungu pamoja nasi
Usilete maana zako kwenye Imani za wengine ,

Ndio maana napo wajibu waislamu unaona natumia maana zao na vitabu vyao sio maana zangu na jinsi navyo amini mimi
Huvijui vitabu vya Kiislaam wewe. Umeenda kupiga porojo za nani sijui huko ukasema ndio msimamo wa Waislaam. Muislaam muongozo wake (na wako pia) ni Qur'an pekee.
 
Hiyo ni phrase , Mungu pamoja nasi
Usilete maana zako kwenye Imani za wengine ,

Ndio maana napo wajibu waislamu unaona natumia maana zao na vitabu vyao sio maana zangu na jinsi navyo amini mimi
Mungu pamoja Nasi imeandikwa Wapi Ndugu yangu. Isaya alisema Aitwe Emanueli. Kama Jina Linamaana ya Mungu pamoja nasi hiyo Ni maana yako. Ila Isaya Alitabiri Ataitwa Hivyo ww kulazimisha Maana Ya Jina Utakuwa Umeenda Nje Ya Utabiri wa Isaya

Malaika Angetakiwa Kumwambia Mariam amuite Emanueli na Si Yesu ili Utabiri wa Isaya Utimie kweli Mtoto aliitwa Emanueli
 
Demons wamefunga uelewa wako , nakuambia ni mifano wewe unaleta ubishani wa kitoto
 
Huvijui vitabu vya Kiislaam wewe. Umeenda kupiga porojo za nani sijui huko ukasema ndio msimamo wa Waislaam. Muislaam muongozo wake (na wako pia) ni Qur'an pekee.
Wewe maswali Yako haya hapa , nimesoma sura nzima sijapata majibu

Koran 66:4. Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake muhammad, basi hakika Allah ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

maswali
1. hao wawili ni kina nani? ,
2. Wamefanya dhambi gani mpaka waambiwe watubu? ,
3. Wakisaidiana dhidi ya Muhammad kwani Muhammad kafanya nini? ,
4. Kwa nini Allah asaidiane na Malaika wote , jibril na waumini wote kupambana na hao wawili?
5. Awa wawili wana nguvu gani mpaka Allah asaidiwe
 
Nimesahau lakini kuanzia matayo mpaka matendo ya mtume ukisoma vizuri humo utakutana na Mungu alikaa kikao na wasaidizi wake kwamba nani aende kuokoa wanaadam ndipo yesu alipojitokeza kuwa yeye atakuja dunian kutuokoa na kwamba mateso yote atayamudu
Na Wewe unaamini Mungu anaweza Kukaa Kikao na Wasaidizi wake.!? Kukaa ni Sifa za Viumbe.. Kufanya Kikao ni Sifa Za Viumbe. Wewe na Mimi na Majini na Malaika. Mungu hakai Na Viumbe wake wala Kuwatuma. Au Unaamini Pia Kuhusu Shetani Kwenda Kupiga Stori na Mungu ili Wamjaribu Ayubu? Hili Jambo Linaingia Akilini Kweli
Kumbuka Afrika Ilikuwa Chini ya Wakoloni miaka na Miaka. Mungu hajawahi kuwatumia Nyie Mtume ila Akawaenda Kuwatumia Wana Waisraeli Pekee. Huoni Hapo Mungu ni Mbaguzi
 
Nimecheka
 

Mkuu mokiti ni wapi kwenye biblia pameandikwa Mungu ana nafsi tatu?
 
Mungu haubiriwi ndugu yangu. Mahubiri na Kusambaza Imani Zimeletwa na Hao Watu kutoka Huko Ukoloni. Afrika Mungu ikuwa haubiriwi popote pale

Bali kulikuwa na Taarifa za Jadi. Kufundishana Taratibu za Kuishi si Kimhubiri Mungu
Sawa inapaswa nao wafundishwe taratibu za kuishi muwape hizo taarifa za jadi kama ambavyo mnavyotaka watu wa dini wapate hizo taarifa za jadi.
 
Demons wamefunga uelewa wako , nakuambia ni mifano wewe unaleta ubishani wa kitoto
Kama ni Mifano Basi Mungu Hafanani na Mifano kama Unamjua Muweke kwenye Uhalisia wake. Kwanini Utumie Mifano wakati Unamjua alivyo

Unatumia Mifano kwa Sababu Unataka Kumfananisha Na Viumbe wake.

Ukisema Nimefungwa Uelewa Angalia wewe ambaye Hujafungwa Unavyomuelezea Mungu Kwa kumfananisha na Viumbe.

Unataka Mungu awe anakaa.. Anasema.. Anakasirika.. Mungu wa Majeshi.. Mungu kamtuma Fulani, Mungu analindwa na Makerubi n.k n.k Hizo ni Sifa za Viumbe Siyi Mungu
 
Huyo mwanae tena si ndio Mungu mwenyewe au hata Sielewi biblia inanichanganya
Mwanaye siyo mungu! Ni mtoto wa Mungu ambaye huko mbiguni sijui ndiyo alikua malaika? Ndiyo siye waroma tupo zetu na bikra maria tu huku kuchanganywa hatutaki
 
Mkuu mokiti ni wapi kwenye biblia pameandikwa Mungu ana nafsi tatu?
Haya Piganeni Wenyewe kwa Wenyewe Tena. Mungu angetaka muwe wamoja Asingewachanga hivi

Ndio mjue Mmeharibikiwa sana Kwenye Hizi Dini. Wewe una amini Hivi Yeye anaamini Hivi ila Wote mnashika Biblia Moja
 
Nimesahau lakini kuanzia matayo mpaka matendo ya mtume ukisoma vizuri humo utakutana na Mungu alikaa kikao na wasaidizi wake kwamba nani aende kuokoa wanaadam ndipo yesu alipojitokeza kuwa yeye atakuja dunian kutuokoa na kwamba mateso yote atayamudu
Kama alishakuja kuokoa wanaadamu sasa haya mateso yanatoka wapi? Na hizi dhambi zinazoendeleaje?
 
Mwanaye siyo mungu! Ni mtoto wa Mungu ambaye huko mbiguni sijui ndiyo alikua malaika? Ndiyo siye waroma tupo zetu na bikra maria tu huku kuchanganywa hatutaki

Soma maandiko uyaelewe mkuu, kuwa Roma siyo sababu ya wewe kutoyajua maandiko.
Maandiko yanasema Yesu ni Mungu
 
Sasa Ndugu unaanzishaje wakati Binadamu wa Kwanza keshawapa Watu(Wabantu) utaratibu wa Kumwabudu Mungu katika Jadi.
Mkuu usichoelewa ni kwamba tunatofautiana mbali na hizo dini za uislamu na ukristo bado kuna mitazamo na imani tofauti tofauti, kwahiyo hayo unayoyajua wewe na kuyaamini basi tambua kuwa ni sehemu tu katika mitazamo au imani zilizopo kwa watu na ndio maana kuna hadi ambao wana mitazamo kabisa ya kuwa hakuna Mungu tofauti na wewe unayeamini mungu ila unasema haongei ila wao hata huyo mungu wako asiyeongea wao wanasema hakuna kitu kama hicho.

Kwahiyo unapoleta hizo story zako sijui za binaadamu wa kwanza sijui utaratibu wa jadi lazima ukumbuke hilo kuwa ni moja tu ya mitazamo mingi iiliyopo duniani kuhusu Mungu.
 
Hawa ndiyo alimkuta mwanamke mwingine ila adam alikua wakwanza
Ukienda Mbele Utajichanganya Mwenyewe. Kaini na Abel walikuwa ndio watoto wa Adam na Hawa Kulingana na Maandiko hayo Hakukuwa na Binadamu wengine. Sasa Kulingana na Maandiko Mungu alimfukuza Kaini. Ila Kaini akalia Akasema Anaweza Kukutana Na Binadamu wengine wakamuua. Sasa Jiulize Mwenyewe kama Adam na Hawa Walikuwa ni Binadamu wa Kwanza wakati hata Wao walitambua Kuna Binadamu wengine



ANDIKO NI HILI

Leo umenifukuza kutoka ardhi yenye rutuba na mbali nawe. Basi, nitakuwa mtu wa kutangatanga, asiye na makao maalumu duniani, na yeyote atakayeniona ataniua.” Lakini Mwenyezi-Mungu akamjibu, “Sivyo! Atakayekuua wewe Kaini atalipizwa mara saba.” Basi, Mwenyezi-Mungu akamtia Kaini alama ya tahadhari, ili yeyote atakayemwona asimuue.

Mwanzo 4:14‭-‬15


Mungu alikuwa na haja Gani ya Kumpiga Chapa kama Hakuna Binadamu wengine Duniani
 
Biblia ni hadithi za Wayahudi tu.

Hata Waafrika tunazo ila watu hawafuatilii.

Kihistoria Waafrika wamekuwepo malaki ya miaka kabla hiyo historia ya Adam haijaandikwa.
 
Ukianzisha Dini Hutakuwa tofauti na Dini zingine tu. Mnatakiwa Kurudi katika Taratibu zilizoachwa na Wazee wenu kipindi wanapelekwa Kutumikishwa
Ngoja nikwambie mkuu kila jamii ilikuwa na taratibu za wazee wao, taratibu za wahindi huko zilikuwa tofauti na waarabu na wazungu au waafrika. Sasa hapo tuseme kwamba hizo taratibu tofauti za wazee zote zilikuwa sahihi au point si usahihi bali ni asili tu kwamba muhimu zilikuwa taratibu za wazee basi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…