Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

jiulize swali moja kisha utapata jibu
kwanini wachawi ukiwatamkia jina la Yesu wanakimbia na kuumia
na kwanini jina la Yesu Lina nguvu ukijibu hayo utaelewa
Mbona bado wachawi wanaongezeka mitaani pamoja na kuwepo na maombi kadhaa na makelel ya walokole kila mahali mitaani mwetu?
 
Ungeweka reference kabisa ili kusapoti ulichoandika, otherwise hili bandiko lako litakuwa halina maana yoyote wala hujui ulichoandika. Pili, tatizo lako kuu ni kwamba mambo ya kiroho unayafikiria kwa jinsi ya kibinadamu.
 
Ungeweka reference kabisa ili kusapoti ulichoandika, otherwise hili bandiko lako litakuwa halina maana yoyote wala hujui ulichoandika. Pili, tatizo lako kuu ni kwamba mambo ya kiroho unayafikiria kwa jinsi ya kibinadamu.

Ok!
 
Ukienda kwa waganga wa kienyeji utambiwaa kalete mnyama tumchinje tumwage damu ili mambo yako yaende so nahisi hiyo ndio Sheria katika ulimwengu wa roho so Yesu amemwaga damu yake Mimi nipone na Yesu ni Mungu na atarudi mara ya pili,nabiii issa eti hajafaaaa hadi leo huyo binadamu wa namna Gani hajafaaaa tokea kipindi Cha mitume basi huyo si binadamu wa kawaida amini hilo na nasikia eti na yeye atarudi just think loud
 
Kama Mungu ni Mmoja Inakuwaje Yesu ni Mungu!?
Mungu ni mmoja tu - Nafsi ni tatu.
Sikiza, Ee Israeli; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja. Cf. Kumbukumbu la Torati 6:4

Ukitumia common sense zako tu kama unavyotamba katika thread hii, kamwe hutakaa uelewe.
Roho Mtakatifu ndiye atutiaye ufahamu wa kuelewa mambo ya Mungu pale tunapoomba kwa dhati.
Kadri ya mafundisho ya imani yako, neno Roho Mtakatifu ni msamiati mkubwa mno kwako. Hapa najua huwezi kuelewa lolote.

Mathayo 3:16-17
Mara tu Yesu (Mungu Mwana - Nafsi ya pili ya Mungu) alipokwisha batizwa, alitoka majini; na kumbe mbingu zikafunguka, akaona Roho wa Mungu (Mungu Roho Mtakatifu - Nafsi ya tatu ya Mungu) akishuka kama njiwa na kutua juu yake. 17 Sauti kutoka mbinguni (sauti ya Mungu : Mungu Baba - Nafsi ya kwanza ya Mungu) ikasema, “Huyu ndiye Mwanangu mpendwa, nimependezwa naye.”
Kubatizwa kwa Yesu Kristo lilikuwa tukio muhimu sana ambalo nafsi zote tatu za Mungu zilikuwepo.
 
Luka Hakuwa Mwanafunzi wa Yesu na Wala Hakuwepo Wakati wa Yesu anahubiri ila Leo hii anakundikia Kitabu unaamini
Ndugu una maswali ya kijinga sana. Najua ulitaka kuandika mtume wa Yesu ukaishia kuandika mwanafunzi wa Yesu.
Iko hivi, walikuwepo mitume wa Yesu pia walikuwepo wanafunzi wa Yesu. yawezekana hili hulijui.
Nitakujibu kwa kifupi sana. Luka hakuwa mtume/mwanafunzi wa Yesu lakini akiwa bado kijana, Luka alimuona Yesu na kusikia mafundisho yake pia baada ya kifo cha Yesu, Luka msomi na daktari wa binadamu, alijikita sana katika kufanya tafiti mbalimbali kuhusu Yesu kupitia watu mbalimbali wakiwemo mitume na wanafunzi wa Yesu pamoja na mkongwe Paulo na hatimaye kuandika vitabu kadhaa vya Biblia.
Je pia unataka tusiamini vitabu vya Paulo kwa kuwa hakuwa mtume wa Yesu?
 
Alikuwa akimwomba Mungu Baba.

Mathayo 10:16-20​

.... Basi, watakapowapeleka nyinyi mahakamani, msiwe na wasiwasi mtasema nini au namna gani; wakati utakapofika, mtapewa la kusema. Maana si nyinyi mtakaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye ndani yenu.

Kumbe huyu Baba si wa Yesu pekee ,bali hata wanafunzi wake pia ni Baba yao?
Ukienda kwa waganga wa kienyeji utambiwaa kalete mnyama tumchinje tumwage damu ili mambo yako yaende so nahisi hiyo ndio Sheria katika ulimwengu wa roho so Yesu amemwaga damu yake Mimi nipone
Hili la kumwaga Damu kwa waganga ni la washirikina , mwenziwao shetani, ili upate hueni.
Inamaana kifo cha huyo anyeambiwa kauliwa msalabani kimeuwa laana kwa nia ya shetani? ili waaminio hivyo wapatiwe haja zao?
Kamwe Mungu hana haja ya Kumuuwa Mwandamu ili asamehe dhambi za wengine, wala kiumbe chochote kile.
Bali ni hila tuu za Mashetani
 
Huko kwa mashetwan kumwaga damu ni fake na wenywewe wanaiga original ya Simba wa Yuda YESU kumbukaa story ya Ibrahim kumtoa sadaka mwanae hata kwenye hiko kitabu chenu hizo mambo kimeandikwaa think loud brother Yesu alitolewa kafara na Mungu mwenywe na damu yake Ina nguvu kwa sababu amefufukaaa ni tofauti na damu zile za mbuzi kwa wale waganga hiyo inananena mema amini hilo uokoke
 
Hili andiko lako Mungu alishatoa jibu kwamba "msichunguze maandiko maana mnatafuta ubatili"!

Mungu alijua upo na utachunguza lutafuta makosa tuu Wala hutafuti usahihi.

Yesu ni Mungu.
Yani unachunguza kutafuta usahihi badala yake unakutana na makosa to???
Inamana unataka tusiseme??
 
Kuna nyang'au wengine wameenda mbele zaidi kw kuamini na kuaminisha watu et yule liepigwa pale na kuuawa pale et ndo mungu mwenyewe duh?
 

Yaan we ndo kiazi kweli!!!! Et yesu ni mungu kwaiyo mungu alishawahi uliwa na wanadaamu?
 
Yaan we ndo kiazi kweli!!!! Et yesu ni mungu kwaiyo mungu alishawahi uliwa na wanadaamu?
Yesu ni Mungu na atarudi mara ya pili alitolewa kafara kwa ajili yetu ni Sheria za ulimwengu wa roho zipo hizo wewe kma unabisha basi kaaa na mtazamo wako na Mimi kiazi niache kiroho Safi tu
 
Yesu ni Mungu na atarudi mara ya pili alitolewa kafara kwa ajili yetu ni Sheria za ulimwengu wa roho zipo hizo wewe kma unabisha basi kaaa na mtazamo wako na Mimi kiazi niache kiroho Safi tu
Mungu anatolewa kafara kwa nani na kwa ajili ya nani? Wakati kama ni kweli si alikuwa na uwezo tu wa kusamehe hizo dhambi bila kujitoa!
Then atolewe kafara yeye kwa ajili yako kwa dhambi zipi ulizokuwa nazo!! Wakati hata ulimwenguni hukuwepo!!
 
Baada ya kuwa mtu mzima nilitafakari kwa makini kuhusu "Mungu kumtoa mwanae kafara" . Binadamu anamtoa mwanae ampendae kafara ili afanikiwe! Wameiga kitendo cha Mungu. Nimegundua hayo ni maujanja tu ya Wazungu ili waitawale Dunia. Ndugu zangu tumtafute Mungu wa kweli. Mimi hata ufufuko siamini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja yako ingelikuwa na mashiko kama ungelileta Ushahidi angalau mdogo wa unayoyasema,kutoka kwenye kitabu chochote au reserch yoyote ile ili kuthibitisha hoja yako.
Nadhani unatumia Mawazo yako too kukanusha au kukubali au siyo?
Akili ina ukomo.

Ni kweli Yesu Alizaliwa Bila baba kama Muujiza,
Nikweli baba yetu Adamu aliumbwa kwa udongo kwa mkono wa Mungu mwenyewe kisha Mkewe akafuatia.
Ni kweli kuwa wote ,wao na sisi na vilivyomo duniani vyote vinamlikiwa na Mwenye Dunia yake
Huyo Mmiliki ndiye MUNGU MUUMBA WA KILA KITU.
TUANZIE HAPO. KANUSHA HAYA KWA HOJA,
KWANI HATA WEWE YAMKINI MIAKA 50 ILIYOPITA HUKUWA CHOCHOTE WALA HUKUTAJWA.
Na miaka 50 ijayo pengine hutokuwepo tena wala hakuna atakaye jali.
Huna uwezowa kuzuia Mwisho wako na huna uwezo wa kubadili DESTIY YAKO, WEWE SI CHOCHOTE BALI Ni MAJI YA UZAZI YALIYOTIWA KWENYE UTUPU WA MWANAMKE UKAUMBWA WEWE NDANI YA TUMBO ,PILA WEWE KUTOWA MCHANGO WOWOTE WA KUWEPO KWAKO, NA KIUKWELI WAZEE WAKO WENYEWE WALIKUWA WANAJISTAREHESHA TUU KWA NGONO. TAHAMAKI MIMBA.
POLE KWA KUONA MAMBO VIBAYA.
 
Mungu anatolewa kafara kwa nani na kwa ajili ya nani? Wakati kama ni kweli si alikuwa na uwezo tu wa kusamehe hizo dhambi bila kujitoa!
Then atolewe kafara yeye kwa ajili yako kwa dhambi zipi ulizokuwa nazo!! Wakati hata ulimwenguni hukuwepo!!
Hil la kutolewa kafara ni FIX TUU YA WANA KANISA, HAYA SI MANENO YA MUNGU WALA YESU MWENYEWE.
UJUMBE WA YESU ULIKUWA MDOGO SANA LAKINI
wakristo hawautaki kuusema.
''na uzima wa milele ndio huu ' wakujuwe wewe MUNGU wa KWELI na wa PEKEE na YESU kristo ULIYEMTUMA'' Yohana 17:3
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…