Niliwasikia kwa Masikio yangu wakisema "Chepuka ila mumeo asishtuke" tena waliokua wakiongea hivyo ni wamama ninaowaheshimu sana na wanaheshimika mno na waume zao hawajui km wake zao huko nje wanauza mechi na hayo wanayoelezana wanaelezana pia kwenye kitchen party zao, walikua wakimzungumzia Dada mmoja ambae ameivuruga Ndoa yake kwa kuchepuka na wanaume wengi kiasi cha kujisahau mumewe akashtukia mchezo kesi ikawa kubwa ndio wakafikia kuongea hayo wenyewe wanakazia "hakuna Mwanamke ambae hachepuki ila chepuka kiakili mumeo asishtuke" nikasema duh hata hawa kumbe ndio walewale