Mungu atawaadhibu kwa dhambi za wazazi wenu, hata kizazi cha tatu mpaka cha nne

Mungu atawaadhibu kwa dhambi za wazazi wenu, hata kizazi cha tatu mpaka cha nne

Kwa Mateso na Kifo Chake YESU hayo yote ya hapo juu yaliuwishwa pale Msalabani- sasa hivi ni Wewe na Mungu! Ubebi dhambi wala hukumu ya Mwingine na wala Watoto wako awarithi dhambi zako

Vifungu vilivyohorodheshwa hapo tumevitoa kwenye kitabu mkuu hii imekaaje? Lile toleo limetoka wapi? Mkuu
 
Kabsa kabsa; tunalipa madeni ambayo hatujawahi hata kuyakopa: inaumiza
Na kuna madeni mengine tunatengeneza sasa watakuja kulipa mpaka wajukuu wa wajukuu wetu.
Ila TUKITUBU NA KUTENGENEZA,narudia tena tukikutubu na kutengeneza(hii ni package) hatumo miongoni mwao wadaiwa.Kwa sababu damu ya Yesu inautakaso wa ajabu
 
haja ya kumpangia Mungu!! Kwann? Asingewapa laana hao hao waliofanya hizo dhambi yaani wazazi mpaka kuamishia laana kwa watoto na wajukuu nn? Kilimkwaza Mungu

Eeee Mungu usituangamize!!!
Ikiwa hawatoziacha njia zao mbaya. Ukizisoma hizo aya(aya na sio sentens fupi fupi) utagundua kuna kichagizo kiashiria cha hiyo adhabu itaendelea kwao hao waendeleao kuzitenda dhambi zilezile.

Mfano 1. Mababu wakaendekeza uzinzi, matokeo yake ugonjwa wa zinaa ukaingia katika jamii hiyo. Madhara ya jamii yao kusumbuliwa na magonjwa ya zinaa yataendelea vizazi vyote endapo vitauendeleza huo uzinzi. Tu.
Mfano 2. Wazazi wakawa watu wema/mafisadi basi watoto wana uwezekano mkubwa wa kurithi tabia husika na kuyapata matokeo husika.

Ndio maana unaona maneno kama 'kizazi cha wanichukiao'. Maana ya wazi kabisa kwamba hicho kijamii ni cha wenye chuki naye. Lakini katika hali ambapo hao watu watabadili mtizamo wao, na ufikiri wao (tafsiri halisi ya kutubu); papo kwa hapo wanakoma kuvaa uhusika wa kizazi cha wanichukiao. Wanakuwa kizazi cha wanipendao na wanapata heri zote

Remember usipende kuchukulia kama Mungu ndo anaadhibu, mambo meeeengi ni kiotomati. We make shit happen. Sisi tukishirikiana na kani zote Mungu included
 
Nilikuwa nafikiria Kwa nn? Usiadhibiwe Kwa kosa lako kipi kifanye adhabu ya mwengine iwaumize wengine
Ndio adhabu hiyo kwa sababu ni kosa kubwa kumwaga damu ya mwenzako. Ni adhabu kali ili watu wasiifanye.
 
Inafikirisha sana, kumbe kuna mahali hata watu wakisaidiwa haina maana kwa sababu ile laana inafanya kazi bado. Mungu atusaidie kugundua laana kwenye familia ili tuweze kuomba toba maana kwa kweli kuna vizazi na familia zinapitia mazito kiasi akili ya kibinaadam inafikia ukomo wake.
 
Nilikuwa nafikiria Kwa nn? Usiadhibiwe Kwa kosa lako kipi kifanye adhabu ya mwengine iwaumize wengine
Ati kama Adam alifanya dhambi enzi zake kwanini adhabu haikuishia kizazi chake cha nne halafu tunateseka sisi leo kizazi sijui cha milioni tano huko
 
Habari waugwana

Rejea kichwa cha mzizi;
Inanifikirisha kidogo na simpingi Mungu bali nahitaji msaada zaidi kwenye hili, Mungu anakazia katika biblia HESABU 14:18 BHN
View attachment 2503098
Tena kwenye KUTOKA 20:5 BHN
View attachment 2503099

Atawaadhibu watoto na wajukuu hadi kizazi cha tatu na cha nne kwa dhambi za wazazi wao

Hizi hadhabu kwa makosa ya wazazi wetu ni hadhabu gani? Na kwa makosa yapi? Hasa ya wazazi wetu!!!

Mtoto kuzaliwa tu na ulemavu na kupata tabu palee anapozaliwa mpaka kufa kwake- inaogopesha na kutia huruma

Kufa kifo kibaya kama kusagwa sagwa kwa kugongwa na gari kubwaa na kutoka kama chapati ilee hali ya mtu kutokukutambua wewe ni nan?

Kuwa na maisha magumu pindi unazaliwa mpaka kufa kwako yaani wewe chakula chako cha shida una pa kulala wala cha kuvaa mpaka unaiaga dunia!!

Kuzaliwa una jinsia mbili ya kike na yakiume na pengine zote zinafanya kazi au mojawapo ilimradi tu ufedheheke

Nb; nilitaka nijue kutoka kwenu wakuu, dhambi ipi hiyo Mungu anaichukia mpaka akaamisha laana kwa watoto mpaka wajukuu yaani mpaka kizazi cha tatu mpaka cha nne!!

Sina haja ya kumpangia Mungu!! Kwann? Asingewapa laana hao hao waliofanya hizo dhambi yaani wazazi mpaka kuamishia laana kwa watoto na wajukuu nn? Kilimkwaza Mungu

Eeee Mungu usituangamize!!!
Pole kwa ndugu zetu wakristo.

Waislam hatuamini kabisa kwenye msingi wa dhambi ya kurithi, tunaamini kila mtu atabeba msalaba wake, kama unazini ni wewe mzinifu ndiye utakaeadhibiwa tena kwa dhambi hiyo hiyo ya kuzini, kama umeua ni wewe muuaji utahukumiwa kwa dhambi hiyohiyo ya uuaji.

Haiingii akilini kabisa kosa afanye babu adhabu aje aipate kitukuu ambae hata hamjui huyo babu mdhambi anafananaje. Huu ni uonevu wa hali ya juu sana.
 
Hii inawezekana ikawa sivyo ilivyo
 
Hivi vitabu vya dini za kutungwa na watu jamani, shida kweli kweli.....Hivi Yesu si alikufa msalabani kufuta dhambi zetu, sasa kwanini bado tunazaliwa tuna dhambi ikiwa Yesu alishajitolea kutufutia? Waafrika tuamke jamani, ujinga mwingine tunajitakia sie wenyewe. Kumbukeni tuliishi miaka kibao bila hizi dini kuja hapa duniani na tukaishi vizui tu, tukapata laana baada ya kuletewa hizi dini (Ukristu na Uislam), hizi dini hazina mantiki yeyote kwetu sie waafrika, tunachezewa tu akili.
 
Pole kwa ndugu zetu wakristo.

Waislam hatuamini kabisa kwenye msingi wa dhambi ya kurithi, tunaamini kila mtu atabeba msalaba wake, kama unazini ni wewe mzinifu ndiye utakaeadhibiwa tena kwa dhambi hiyo hiyo ya kuzini, kama umeua ni wewe muuaji utahukumiwa kwa dhambi hiyohiyo ya uuaji.

Haiingii akilini kabisa kosa afanye babu adhabu aje aipate kitukuu ambae hata hamjui huyo babu mdhambi anafananaje. Huu ni uonevu wa hali ya juu sana.
Mungu wetu sisi alitaka yale maovu unayowafanyia watu wengine ukiona furaha na kujigamba yawapate na wanao na wajukuu zako kama unaona ni mazuri na wao wayavune.
 
Mungu wetu sisi alitaka yale maovu unayowafanyia watu wengine ukiona furaha na kujigamba yawapate na wanao na wajukuu zako kama unaona ni mazuri na wao wayavune.
Sasa mkuu hao wana na wajukuu wana kosa gani?

Sio kwamba ni ‘fair’ kama aliyefanya ndio afanyiwe?
 
Sasa mkuu hao wana na wajukuu wana kosa gani?

Sio kwamba ni ‘fair’ kama alitefanya ndio afanyiwe?
Hawa wanaofanya maovu dhidi ya wenzao ni watu wenye nguvu hasa za kimamlaka na fedha. Na huwa wanadumu muda mrefu. Sasa Mungu hawezi kusubiri hadi wakati wa Kyama. Ikiwa hivyo watu watakuwa hawajifunzi. Ndio maana anataka awaadhibu hapa hapa. Na dhambi hiyo igawanywe kwenye uzao wako kama unaona ni nzuri basi waivune.
 
Back
Top Bottom