Wengi huwa wanamwendea Mungu kwa kutia huruma, yaani wanadeka yaani, wakihitaji kuonewa huruma, wakati Mungu anachohitaji kwako ili akutendee chochote ni Imani. unaweza kulia na kutia huruma bila imani ikawa kazi bure. Ni kweli Mungu ana huruma, lakini namna pekee anafanya kazi na sisi ni kwa njia ya imani, ukiwa na shida hutapona kwasababu unatia huruma mbele zake, unapiga magoti uombe badala ya kuomba unalia tuu kwa uchungu, badala ya kumwambia shida zako. Ongea shida yako, amini, nalo litatokea. Sema shida ni kwenye ufahamu wa Neno la Mungu, kuna watu wanamhitaji Mungu wakiwa na shida tu, ila wakati wakiwa wazima au hawana shida hawasomi hata Neno lake hivyo wanakuwa so ignorant of the word of God.
Faith never comes through discussing with people their, pains and aches, weaknesses and sicknesses. Faith is born when we hear the word of truth. Jesus said: You shall know the truth, and the truth shall make You free. He is the truth.
Imeandikwa, Ninyi mkikaa ndani yangu na Maneno yangu yakikaa ndani yenu ombeni lolote mtakalo nanyi mtatendewa. sasa mtu husomi Neno halipo moyoni mwako, utajua unaombaje? na imani yako itakujaje wakati Imani huja kwa kusikia, kusikia Neno la Mungu. muda wote watu wamekalia mitandao ya kijamii mara facebook, twitter, whatsapp, n.k ambavyo havijengi roho, ila wakipata shida hata kipiga magoti kuomba hawana Neno la Mungu moyoni walau la kuwatia imani wajue tu hata maeneo Mungu aliahidi kuwatatulia matatizo yao. mwisho wanaishia kutafuta waombeaji wawauzie mafuta maji na chumvi kama waganga wa kienyeji, na hakuna kinachotokea maishani mwako.
mtakuja kuishia kudondokea hadi kwa waombeaji wenye upako wa kishetani na wanaofanya kweli mazingaombwe, jueni kuwa hata shetani akikufanyia mazingaombwe yeyote ukaona kama kuna badiliko fulani, hakika imeandikwa "baraka za Mungu hutajirisha wala haichanganywi na huzuni (Baraka za BWana hazina majuto). Mungu anaponya na uponyaji wake ni wa kudumu na hauna garama, ni bure, ila mazingaombwe ya shetani hata ukiona kama amekuponya sio wa kudumu na lazima utegemee kulipa garama, waumini wote wa shetani wanajua kuwa hajawaku kukufanyia kitu bure, lazima kuna majuto yameambatana nacho icho kitu na kuna siku utajuta tu. Mithali 10:22.