Mungu aweza kukutoa kwenye hiyo shida!

🤣🤣🤣Sio kosa lako mkuu , kosa lipo kwa hao walikujaza hofu ya kifo na motoni.
 
Tatizo mwisho wa siku mnataka mpewe hela, acheni utapeli!
wala sipo huko ndugu yangu, mimi pia napinga watu kutoa pesa ili waombewe, napinga kuuza maji au kuambatanisha kitu chochote kama substitute ya JINA LA YESU. Yesu alisema ombeni kwa Jina langu, hivyo viambatanisho ni mpango wa adui. infact, ukisoma Neno la Mungu na kuliamini kuanzia hata kwenye post yangu pale awali, imeze ile mistari, mwamini Mungu, afu omba ukijua kuwa Mungu huwa anatenda hasemi uongo, UNAWEZA KUPONA HATA BILA KUWEKEWA MIKONO NA MTU. hivyo sio lazima uwekewe mikono, soma Neno la Mungu, liamini, litatenda kazi ndani yako (pamoja na kwamba kuwekewa mikono sio kubaya na sio watumishi wote ni wa shetani, wapo manabii wengi wa Mungu wapo pia wa mashetani),

cha muhimu, Mungu huwa hauzi baraka, uponyaji Yesu alishalipa kwa kifo cha msalabani huhitaji kulipia tena, ukiona mtu anasema ulipe pesa, kimbia, hapo umepotea. ukiona mtu anasema toa sadaka ya kujimaliza upone, kimbia, ukiona mtu anasema ili upone lazima utoe sadaka ya uponyaji kimbia mwambia kazi ya Yesu msalabani ilitosha na binadamu hana uwezo kutoa gharama ya kujikomboa wala kujiponya, Yesu alilipa yote, yatosha kumwamini Yesu na kupokea uponyaji.

ila ukweli usemwe, Neno la Mungu linasema, "akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote", ikiwa na maana uponyaji wako unaweza kuupata kwa kumpa Yesu Maisha yako, uokoke ili maisha yako yawe mikononi mwake, na kwasababu Isaya 53:4 kazi ya Yesu ya ukombozi iliambatana ya uponyaji, akikusamehe dhambi utakuwa na haki ya kuponywa pia. Ndio maana Yesu katika MARKO 2:4 - 12 alimwambia yule mgonjwa "umesamehewa dhambi zako, simama ujitwike godoro lako". kusamehe dhambi kuliambatana na kuponywa. pia katika ZABURI 103:3 inasema, akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote. HIVYO OKOKA, NA PIA JIEPUSHE NA HAO WANAOUZA WOKOVU NA UPONYAJI, HAWATOKANI NA MUNGU na sio walokole. ulokole hauko hivyo.
 
🤣🤣🤣Sio kosa lako mkuu , kosa lipo kwa hao walikujaza hofu ya kifo na motoni.
moto upo, na kifo kipo, kama wewe ni mwanadamu panga maisha yako sasa, where you will spend your eternity, motoni au uzimani, ila vyote vipo. ungali unapumua ni opportunity Mungu amekupa pengine utabadilika, na usipobadilika siku ile hautakuwa na wa kumlaumu, utajilaumu wewe wenyewe. kwasababu kama kafara la wokovu lilishatolewa, ni wewe tu kuliendea au kulipinga kama unavyofanya sasa. Nuru imekuja duniani watu mnapenda giza kuliko nuru, kwasababu matendo yenu yapo gizani.
 
Thibitisha unayosema ni kweli, na sio maneno yakuambiwa tu
 
Ukichukua mtizamo wa kwamba it is written hakuna mwenye kosa au uwezo wa kubadilisha ni kama movie imeshaisha tume-rewind sasa hivi inacheza kwa mara ya pili....

Ila ukichukua mtizamo kwamba kila jambo lina kanuni zake na ukilifanya kwa kufuata hizo kanuni au kama ni fair, wewe ukatumia unfairness na bila kukata tamaa basi hakika utafanikiwa....

Ila ingredient ya Mungu au Imani yoyote ile inakupa Confidence na mwenye confidence ana advantage kuliko asiye na confidence...
 

1. MK254 kuna maneno kuntu huku. Yako kwenye jukwaa lake. Tuko huku tumetulizana, tunapata neno kwa muda.

2. Kwenye majukwaa mengine tutarejea baadaye. Tupate madini yakueleweka kwanza hapa!
 
fafanua zaidi hapo ndugu. natamani kufahamu unachomaanisa.

Mungu akisema kitu amesema, hakuna kubadilisha. katika kujifunza, nimegundua Mungu ana tabia kadhaa, nitataja chache sana zinazoendana na mada.

1. Yeye ni Mungu, zaidi yake hapana mwingine.

2. Mungu hasemi uongo, chochote alichokitamka huwa anakitimiza, na wakati wowote atamkapo hua anaweka masharti, ukitimiza tu hilo sharti unakuwa umemaliza upande wako inabaki upande wake, atatenda.

3. Mungu habadiliki, akisema kitu huwa hakibadilishi, labda kama kwa makubaliano nawe upya labda baada ya kuona mwanadamu unashindwa kufanya upande wako, ni Mungu wa maagano. msingi wa hili ni kwamba, God is can be trusted, anaaminika, sio kigeugeu.

4. Muunganiko wa vyote tunapata kwa Mungu ni kwa njia ya "Imani", achana na maneno yaliyozoeleka ya watu wa dini wanayoyaongea mdomoni tu kwamba uwe na imani au sijui pasipo imani nakadhalika, ongea toka rohoni ukimaanisha kwamba, Mungu anataka umuamini kwanza kwamba yeye ni Mungu na pili kwamba chochote alichoahidi anao uwezo kukitenda na atakitenda kwasababu yeye huliangalia Neno lake alitimize. usipomwamini ni dharau kwake, it is as if huoni kama anaweza, unakuwa umemweka level na wanadamu wanaoahidigi vitu na hawatekelezi, yeye ni Mungu. Katika maombi yako, omba ukiwa na imani kwamba anaenda kutenda na ameshatenda, bila hofu yeyote, ndicho anachotaka.
 
Kwani huyo Mungu bila kugubikwa masifa na kumsemea huwa hawezi kuwa mungu et!!!
 
Kwani huyo Mungu bila kugubikwa masifa na kumsemea huwa hawezi kuwa mungu et!!!
kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema kwamba, Imani ni sawa na kutegemea kuwa kile Mungu alikisema kwenye Neno lake atakitenda, ni kuamini kwamba Mungu ni Mkweli kwa kile alichokiahidi katika Neno lake
 
kwa lugha nyepesi ni sawa na kusema kwamba, Imani ni sawa na kutegemea kuwa kile Mungu alikisema kwenye Neno lake atakitenda, ni kuamini kwamba Mungu ni Mkweli kwa kile alichokiahidi katika Neno lake
Sawa mkuu
 
Neno la Mungu kwao wapoteao ni upuuzi mtupu... Amani ya Bwana iwe nawe...uzidi kutukumbusha ukuu wake
 
fafanua zaidi hapo ndugu. natamani kufahamu unachomaanisa.

Mungu akisema kitu amesema, hakuna kubadilisha. katika kujifunza, nimegundua Mungu ana tabia kadhaa, nitataja chache sana zinazoendana na mada.
Kwahio ameshasema au hajasema ? Sababu kama ameshasema hapa tunapoteza muda tu (actually hatupotezi muda bali tunafuata script iliyopo) unachofanya wewe au mimi hakitabadilisha kilichoshasemwa..., Na kuwa na mtizamo huo ni kama kichaka cha kujificha kwenye mapungufu ya mtu husika (sababu mtu huyo kila anachofanya anatimiza kilichosemwa)
1. Yeye ni Mungu, zaidi yake hapana mwingine.

2. Mungu hasemi uongo, chochote alichokitamka huwa anakitimiza, na wakati wowote atamkapo hua anaweka masharti, ukitimiza tu hilo sharti unakuwa umemaliza upande wako inabaki upande wake, atatenda.
Sasa kama kuna masharti na ni mimi ndio nina uwezo wa kutimiza hayo masharti au nisitimize basi vitu havijasemwa..., ni mimi ndio mwanzo wa kesho yangu sababu utendaji wangu wa leo utaamua kesho yangu na sio kilichosemwa jana ndio kinaamua kesho na leo yangu.... Hapa natumia maneno yako mwenyewe mkuu hata bila kutumia mtizamo wangu...
3. Mungu habadiliki, akisema kitu huwa hakibadilishi,
Okay nimekuelewa unachoniambia
labda kama kwa makubaliano nawe upya
Sasa kama kuna makubaliano au kuna nafasi ya kukubaliana huoni kwamba hapo utakuwa umepinga sentensi yako ya mwanzo kwamba habadilishi kitu ?
labda baada ya kuona mwanadamu unashindwa kufanya upande wako,
Kama anajua mwanzo sasa na kesho basi angejua tangia jana kwamba leo nitashindwa..., unless unamaanisha hajui kesho ipoje ?
ni Mungu wa maagano. msingi wa hili ni kwamba, God is can be trusted, anaaminika, sio kigeugeu.
Ningekuelewa hapa sawa ila nashindwa kukuelewa sababu unajipinga mwenyewe....
Mkuu hapo kwa maneno mengine ni kama umemshusha Mungu.., hizo characters ulizoweka ni za kujali vitu petty..., yaani ni kama Binadamu wanavyopenda machawa, kusifiwa na wana hasira na kisirani usipowaheshimu na kuwasifia na kuwasujudia.... Sidhani kama unaamini hizo ndio characters za Mungu..., Yaani ukimsifia yeye ndio anafurahi ukipofanya hivyo anakasirika na anakutishia kukuangamiza (hio logically haiendeni na mpenda vyote na most powerful ambaye hajali vitu petty)
 
wewe hufai hata kujibiwa. hueleweki.
 
ungelikua umesoma vizuri ungeelewa kuwa nimesema nimeweka tabia chache tu zinazoendana na hoja ya leo, hoja ya Kuamini kile Mungu amekisema. ndio maana tunasema muokoke msiabudu dini, ili mpate Nguvu za Roho Mtakatifu awasaidie kutafsiri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…