Mungu Fundi; Baada ya kuwanyima wapinzani majukwaa, sasa CCM ndio wanafanya kazi ya upinzani na wanaofanya mpaka 2025

Mungu Fundi; Baada ya kuwanyima wapinzani majukwaa, sasa CCM ndio wanafanya kazi ya upinzani na wanaofanya mpaka 2025

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wao waliamini wakiwazuia wapinzani kufanya mikutano ya siasa na kukutana na makundi mbalimbali ya jamii, basi wao watakuwa salama kisiasa na upinzani utakufa/utadhhofika.

Hata hivyo, kwa jinsi Mungu aliyokuwa Fundi, kapundia meza/mkeka kama walivyofanya Yanga kule Tunisia hivi karibuni. na sass makada wanafanya kazi ya upinzani kwa faida ya wapinzani na watanzania masikini wa nchi hii.

Ni swala la muda tu kabla hawajaibuka makada wengine kuwasemea watanzania kuhusu matatizo ya mgao wa umeme na maji huku wapinzani wakibakiwa na kazi moja tu ya kuchochea moto kupitia mitandao.

Sisi tunawaangalia tu na kuwahesabia siku kwani siku zenu za kukaa madarakani zinahesabika. Mpaka ifike 2025, mtakuwa mmeparuana na kuparaganyika vya kutosha.

NB: Kwa jinsi Mungu alivyowanyima maarifa, mnafikiri kumshbulia Bashiru ndio mnamsaidia Mama na chama chenu kwa ujumla, kumbe kinyume chake ndio ukweli .
 
MPAMBANO NI MKALI LAKINI KWA KUANGALIA UMILIKI wa MPAMBONO MPAKA SASA BASHIRU ana miliki Mpambano kwa ASILIMIA 90% na CCM kupitia MAKADA wake wasio na HOJA ASILIMIA 10% Mchezo bado unaendelea
 
MPAMBANO NI MKALI LAKINI KWA KUANGALIA UMILIKI wa MPAMBONO MPAKA SASA BASHIRU ana miliki Mpambano kwa ASILIMIA 90% na CCM kupitia MAKADA wake wasio na HOJA ASILIMIA 10% Mchezo bado unaendelea
Waparuane Taifa lipone.
 
Back
Top Bottom