Mungu hajagawanyika katika nafsi tatu, Mungu ni nguvu Mungu ni energy

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
Mungu hajagawanyika katika nafsi tatu. Mungu ni nguvu, Mungu ni energy. Mungu amesambaa katika kila kona unayoijua. Roho zilizo ndani ya nafsi na miili yetu ni sehemu tu ya Mungu. Ndiyo maana hata maandiko yamekiri kuwa sisi ni Mungu, yaani tunaroho wa Mungu. Hivyo, masomo ya Kikushi yanatufundisha tujifahamu. Ukijitambua na kuweza kujiconnect na huyo Mungu mkuu, unavuka uwezo wa kibinadamu ukiwa bado ndani ya mwili wa nyama.

Manabii wanaosemekana kufanya makubwa kama kufufua watu au kufanya miujiza walikuwa katika level hii.

Ujumbe wa post hii ni huu:
Fahamu kuwa wewe ni Mungu, lakini unakosa muunganiko na Mungu mkuu. Unapaswa sasa kujiunganisha naye. Ukiacha mwili ukiwa umeungana naye, unaenda kuungana naye kabisa. Lakini ukifa bila muunganiko huo, utabakia kuwa mzimu na utarudi tena duniani.

Wafia dini, elimu hii acheni. Hamtaelewa wala kuambulia chochote katika post hii.
 
Sifa za Mungu.
1) Omnipresent (Yupo kila mahali) - - Zaburi 139:7-10
2)Omniscience (Anajua kila kitu) __Zaburi 139:1-4
3)Omnipotence Zaburi 115:3

Sasa nami nakuuliza binadamu ana hizo sifa?
Binadamu anaweza kuumba? Binadamu anajua kila kitu?
Binadamu yupo kila sehemu? Kama kweli ukifa umeungana naye unaenda huko Mbinguni je mhubiri 9:10 ina maana gani?
 
Wewe umesoma na kukulupuka Kwenye comment kujibu maswal Yako hayana mashiko napita ivi,yakiwa na mashiko nitakujibu
 
Mtu ni Roho anayo nafsi anaishi katika mwili.. Mtu akiweza kuishi kwa kuongozwa na Roho na sio mwili ndio anakuwa na huo uungu..

Kumbukizi: Mungu ni Roho amemtengeneza mwanadamu katika ufanano wake(Roho) akampa mwili ambao ndio nyumba ya Roho na nafsi ambao nimatokeo ya kuwepo kwa mwili na Roho.. Ni nafsi ndio inabeba taarifa,hisia na akili..
 
Sifa za Mungu.
1) Omnipresent (Yupo kila mahali) - - Zaburi 139:7-10
2)Omniscience (Anajua kila kitu) __Zaburi 139:1-4
3)Omnipotence Zaburi 115:3

Sasa nami nakuuliza binadamu ana hizo sifa?
Binadamu anaweza kuumba? Binadamu anajua kila kitu?
Binadamu yupo kila sehemu? Kama kweli ukifa umeungana naye unaenda huko Mbinguni je mhubiri 9:10 ina maana gani?
Kumfananisha Mungu na mwanadamu kwa hapa duniani ni kumkosea adabu
 
Ukijiweka karibu na Mungu utakuwa na roho ya Kiungu.

Ukijiweka karibu na shetani utakuwa na roho ya kishetani.

Kumbuka katika roho hizo mbili moja ya Positive na moja Negative.
 
Washirikina ndo wanasema mungu wao kajifanyia mtoto na kila wanachoomba wanaomba kupitia jina la huyo mtoto na kuna muda washirikina hao hujisahau na kumuita huyo mtoto mungu
 
Mungu hajagawanyika katika nafsi tatu. Mungu ni nguvu, Mungu ni energy. Mungu katika kila kona unayoijua wewe hizo roho zilizo ndani ya nafsi na miili yetu ni sehemu tu ya Mungu ndio maana hata maandiko ya kitapeli yamekiri sisi ni Mungu, yaani tuna roho wa Mungu

Hivyo basi ndio mana masomo ya kikushi yanatufunza tujitambue, ukijitambua ukaweza sasa kujiconnect na huyo Mungu Mkuu unakuwa umevuka uwezo wa kibinadamu ukiwa bado ndani ya mwili wa nyama

Manabii wanaotajwa kuwa walifanya makubwa sijui walifufua sijui walifanya miujiza gani maana yake walikuwa katika level hii.

Nini sasa maana ya huu ujumbe?
Ikiwa unataka ufahamu ya kuwa wewe ni Mungu ila unakosa muunganiko na Mungu Mkuu unapaswa sasa kujiunganisha na Mungu Mkuu ili ukiacha mwili unaenda kuungana nae lakini iwapo ukiacha mwili hujajiconnect ukifa utabakia kuwa mzimu na utarudi tena duniani

Wafia dini hii elimu achaneni nayo hamtaelewa wala kuambulia chochote katika post hii
Kama Mungu ni energy, TANESCO wakikata umeme wanakuwa wamemkata Mungu?
 
Huyo ni mungu wako aitwaye emergy. Mwisho utasema energy drink. Injili tuliyoipokea inasema Mungu ameganyika katika nafsi tatu, Mungu Baba, Mungu Mwana na Roho Mtakatifu. Hii inaitwa Utatu Mtakatifu. Usilete injili ya kigeni hutaeleweka
 
Mungu hajagawanyika katika nafsi tatu. Mungu ni nguvu, Mungu ni energy. Mungu amesambaa katika kila kona unayoijua. Roho zilizo ndani ya nafsi na miili yetu ni sehemu tu ya Mungu. Ndiyo maana hata maandiko yamekiri kuwa sisi ni Mungu, yaani tunaroho wa Mungu. Hivyo, masomo ya Kikushi yanatufundisha tujifahamu. Ukijitambua na kuweza kujiconnect na huyo Mungu mkuu, unavuka uwezo wa kibinadamu ukiwa bado ndani ya mwili wa nyama.

Manabii wanaosemekana kufanya makubwa kama kufufua watu au kufanya miujiza walikuwa katika level hii.

Ujumbe wa post hii ni huu:
Fahamu kuwa wewe ni Mungu, lakini unakosa muunganiko na Mungu mkuu. Unapaswa sasa kujiunganisha naye. Ukiacha mwili ukiwa umeungana naye, unaenda kuungana naye kabisa. Lakini ukifa bila muunganiko huo, utabakia kuwa mzimu na utarudi tena duniani.

Wafia dini, elimu hii acheni. Hamtaelewa wala kuambulia chochote katika post hii.
Dini ni fasihi

Na pale unapodhani uanielewa fasihi… Basi jua upeo wako ndio umeishia hapo

Mafunzo ya fasihi ni Marefu kuliko shimo lolote lile
 
Mungu hajagawanyika katika nafsi tatu. Mungu ni nguvu, Mungu ni energy.
Ulijuaje hiyo nguvu ni Mungu na si kitu kingine chochote kile?

Au umeamua tu kuitungia jina na kuipachika hiyo nguvu jina "Mungu"?
Mungu amesambaa katika kila kona unayoijua. Roho zilizo ndani ya nafsi na miili yetu ni sehemu tu ya Mungu. Ndiyo maana hata maandiko yamekiri kuwa sisi ni Mungu, yaani tunaroho wa Mungu.
Sisi ni binadamu.

Sisi sio Mungu.

Mungu ni jina uchwara mlilo jitungia vichwani mwenu tu lisilo na uhalisia wowote ule.
Hivyo, masomo ya Kikushi yanatufundisha tujifahamu. Ukijitambua na kuweza kujiconnect na huyo Mungu mkuu, unavuka uwezo wa kibinadamu ukiwa bado ndani ya mwili wa nyama.
Huyo Mungu mkuu si aje aji connect mwenyewe na sisi?

Au anasubiri sisi ndio tuanze kumshobokea kuji connect naye?

Aanze yeye kuji connect na sisi kama ana huo uwezo.
Manabii wanaosemekana kufanya makubwa kama kufufua watu au kufanya miujiza walikuwa katika level hii.

Ujumbe wa post hii ni huu:
Fahamu kuwa wewe ni Mungu, lakini unakosa muunganiko na Mungu mkuu. Unapaswa sasa kujiunganisha naye. Ukiacha mwili ukiwa umeungana naye, unaenda kuungana naye kabisa. Lakini ukifa bila muunganiko huo, utabakia kuwa mzimu na utarudi tena duniani.
Huyo Mungu mkuu kama yupo aanze yeye kujiunganisha na sisi.

Kwani huyo Mungu mkuu hajui kwamba anapaswa kuunganika na sisi binadamu?
Wafia dini, elimu hii acheni. Hamtaelewa wala kuambulia chochote katika post hii.
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu, Na wala huwezi kuthibitisha uwepo wake.

Huyo Mungu mkuu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajiunganishe na sisi kama ana huo uwezo.
 
Sifa za Mungu.
1) Omnipresent (Yupo kila mahali) - - Zaburi 139:7-10
Kila mahali wapi?

Huyo Mungu yupo vichwani mwenu tu kwenye mawazo yenu ya kufikirika.
2)Omniscience (Anajua kila kitu) __Zaburi 139:1-4
Kulingana na Biblia yenu hiyohiyo,

Huyo Mungu unayedai anajua kila kitu, Alishindwa hata kujua kwamba shetani atakuja kumuasi amdhibiti na kumzuia mapema, Hadi shetani akafanikiwa kumuasi.

Huyo Mungu wenu hajui kitu kabisa. Na ni msahaulifu sana.
3)Omnipotence Zaburi 115:3

Sasa nami nakuuliza binadamu ana hizo sifa?
Binadamu anaweza kuumba? Binadamu anajua kila kitu?
Binadamu yupo kila sehemu? Kama kweli ukifa umeungana naye unaenda huko Mbinguni je mhubiri 9:10 ina maana gani?
Binadamu anazaa watoto.

Binadamu hatujui kila kitu, lakini tunaendelea kupunguza tusivyo vijua Kwa utafiti, uchunguzi, udadisi na majaribio zaidi.

Huyo Mungu mmemtunga vichwani mwenu tu. Kwanza huwezi kuthibitisha uwepo wake.
 
Sifa za Mungu.
1) Omnipresent (Yupo kila mahali) - - Zaburi 139:7-10
2)Omniscience (Anajua kila kitu) __Zaburi 139:1-4
3)Omnipotence Zaburi 115:3

Sasa nami nakuuliza binadamu ana hizo sifa?
Binadamu anaweza kuumba? Binadamu anajua kila kitu?
Binadamu yupo kila sehemu? Kama kweli ukifa umeungana naye unaenda huko Mbinguni je mhubiri 9:10 ina maana gani?
Mmevulugana sehemu ndogo tu mkashindwa kuelewana....vitu vyote vipo ndani ya mungu na vimeumbwa ndani ya mungu ...sisi tupo ndani ya mungu ni sehemu ya utukufu wa mungu ..jamaa yupo sahihi ...hakuna mungu mmoja kisha awe na nafsi 3 kwa sababu umoja wa mungu upo kwenye nafsi
 
Ukijiweka karibu na Mungu utakuwa na roho ya Kiungu.

Ukijiweka karibu na shetani utakuwa na roho ya kishetani.

Kumbuka katika roho hizo mbili moja ya Positive na moja Negative.
NAJIWEKAJE KARIBU NA MUNGU? MAJIBU TAFADHALI..
 
Back
Top Bottom