Mikosi, Kila kitu kibaya Mimi. Dhambi zangu hazijai hata kikombe lakini niliyoyapitia ni magumu kuliko umri wangu.
Lakini ukitazama wengine kwenye matendo maovu yote huwakosi, Ila wamejaa neema tele. Kila kitu kizuri kwao.
Ninapoelekea naenda kutokumwamini huyu kiumbe wa kuitwa Mungu. Maana kama kweli yupo ni mtesaji na mnyanyasaji kweli.
NIMEMALIZA.
Mungu ana Kanuni zake Mkuu.
Unataka kula Mema ya Nchi Fata Kanuni zake, hutaki kufata Kanuni zake, then Mungu ana Roho Mbaya mno, ana hasira Mno...!
Kanuni za Mungu haziruhusu wewe Kujisifia na Dhambi zako ambazo hazijai kikombe...!
Mungu anaangalia Moyo wako Ndugu, kama Moyo wako umejaa Visasi, Hauna Upendo, Roho Mbaya, ukifanya Dhambi hujui kutubu, sahau kupokea Baraka za Mungu.
Kwani wewe usipotambua uwepo wa Mungu unadhani Mungu anapungukiwa na Nini, Yani ukubari uwepo wake, usikubari... BADO YEYE NI MUNGU NA ATABAKI KUWA MUNGU.
Sio Watu wote wenye Maisha Mazuri ni Baraka toka Kwa Mungu.
SHETANI pia anatoa Utajiri...!
Binadamu anapozaliwa na Baraka zake zinakua realised, tunapokua Watoto familia zetu ndo huamua hatima yetu ya Kiroho, Kwa kutukabidhi Kwa mizimu na mambo ya Matambiko, tunapokua Wakubwa, Mizimu ile ile inakwenda kinyume na sisi coz hatukujua namna ya kuiabudu...!
Chukua hii ya Mwisho...!
Ukiona Familia ya kiafrica hakuna mtu ametoboa, na ikitokea ni mmoja ama wawili ukoo mzima ama familia nzima, JUA KUNA UCHAWI KWENYE FAMILIA, na Wachawi siku zote wanajua future Yao tokea Ulimwengu wa Roho...!
Nadhani ushawahi kusikia Kuna Watu wanasemwa Walikua na Akili Sana, walikua na future, ghafla Wakawa Machizi, ghafla Wakawa walevi Mbwa, kila anayewajua atasema usimuone hivi hivi huyu, alikua na Akili Sana, ama ana Masters huyu, ila kawa mpevi Mbwa...! JUA KUNA UCHAWI KWENYE FAMILIA... hapo ndo utajua Kwa Nini waswahili walisema MCHAWI NI NDUGU...!
Kusuka ama kunyoa, inategemea na Maamuzi Yako uzuri kichwa no chako mwenyewe...!
"Eeeish, nadhani ningekua Pastor, hakuna mtu angekuja Kanisani kwangu, Watu wanataka kusikia ile Injili ya POKEA MAGARIIII!"