Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu


Nenda Kwa mangi kanunue oxygen ya elf mbili

Then urudi tena kuandika ujinga wako,

Unaweza kuwa na Simu, kulipia bando na kuandika maujinga then unalalamika?
 
Mungu anaweza akawepo lkn sio kama tunavyomfikiria kwamba anamiujiza..!
Ukishaanza kusema anaweza akawepo maana yake umekubali anaweza asiwepo. Hapo umeweka conjecture.

Unathibitishaje Mungu yupo?
 
Nimekuelewa sanaaa, future yako ni kubwa mnoo na vita yako imekuwa kubwa pia, hivyo moyo umefadhaika. Na utajua sio muda mrefu Kuwa Mungu yupo na anaishi. Hii haitakuja kama ushuhuda wa mtu, bali wewe mwenyewe utashuhudia. Maana utaona na kukiri kwa moyo wako.

Pole sana giza limeendelea sana sasa karibia kunakuchwaa.
 
Hata vilema bado wanashukuru Mungu
Sasa wewe unacholaumu hapa sijakiona bado
Umekosa ajira? Wengi hawana ila bado wanapambana
Huna kitu? Bado una watu wa karibu wanaweza kukusaidia au huna mda nao
 
Asipobadilika kupitia huu ujumbe atakuwa mfu anaetembea, kibaya zaidi ni kwamba hajui lengo la kuumbwa kwake.
 
Kama yeye hakusaidii, msaidie wewe; maisha ni kusaidiana.
 
Tuliza Moyo wako. Mungu ana haja nawe. Endelea kumwomba Mungu. Maana ni kitambo kidogo tu ataenda kutenda.
 
Mkuu shida ni wewe mwenyewe fikra zako juu ya mazingira yanayokuzunguka ndio zinachukua asilimia kubwa ya hali unayopitia.

Sasa kama unataka mabadiliko kwanza kabisa, Kamwe usimlaumu/usifikilie kua watu au Mungu ndio wamesababishia hali hiyo.

Amini kwamba hali iwayo yoyote ile unayopitia wewe ndio chanzo na hakuna mtu yeyote ataibadilisha kama wewe mwenyewe hautataka kubadilika.

Kwanini ni kwasababu wewe binafsi umepewa uwezo wa kuamua/ wakuchagua na ukiamua na kuchukua jitihada kwa Akili yako, mali zako na nguvu zako zote... Hilo jambo uliloamua litafanikiwa tu(kwa lugha nyingine ni unakua na IMANI) na yeyote aombaye kwa imani basi aamini amekwisha pokea)

Yaani binadamu yeyote yule (wewe) Ni sehemu ya Mungu/una Uungu ndani yako na nguvu unazo. Kiufupi wewe ni Mungu na kwa ujumla wetu watu wote tunaunda mtandao wa MUNGU. Sasa kama sisi ni miungu kwanini wengi wetu hatuna maajabu(nguvu) Ni KWASABABU hatujiamini(hatuna IMANI) hatujajiunganisha na mtandao wa MUNGU. Sasa kwanini umlaumu au ufikilie mbona kina fulani wako hivi mimi siko ilhali uwezo huo na wewe unao.

Sasa mimi nakushauri badilisha kabisa fikra zako uwe unajiwazia mambo mema ya baraka, mafanikio, huku ukiongeza Akili nguvu na mali zako zote(Uwekezaji) katika malengo ulio jiwekea katika utaftaji wako na ili nafsi yako ione uko serious*** nakushauri badili kabisa mazingira nenda sehemu ambako hujulikani na hauna msaada wowote kwako then ishi vizuri na watu.
 
Kwanini una hasira nami Ndugu yangu? Ndiyo ni kweli hajawahi kunisaidia
 
Kama ni kuomba niliomba sana.
Lakini bado hali tete kwangu
 
Kumbe kwa mantiki hiyo ni kuwa hayupo?
 
Kwahiyo hao wagonjwa waliopo huko hospitali ndiyo wanastahili kuteseka? Huruma ya Mungu ikowapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…