Mungu hana msemaji wala dalali huku duniani

Acha wajinga wapigwe tyuu
 
@mama D
 
Hakuna yeyote aliyekutuma wewe au manabi, mitume na makuhani wako. Waongo na matapeli wakubwa nyie.
 
Hii mistari inayoileta hapa ndiyo uliyofungiwa na hao wachungaji wenu,iweje mchungaji akuombee na kukubariki wewe upate mafanikio na ashindwe kuwapa ndigu zake maombi?

Hata Musa hakuweza kumfanikisha dada yake Miriam na kaka yake Haruni
Wala Yesu hakuweza kumfanya binamu yake Yuda kufanikiwa

Tumia akili kidogo kuelewa utendaji wa Mungu
 
Wanakusanya makundi makubwa ya watu wapumbavu na kuwachosha kwa ibada ndefu na kuwaaminisha kwamba wanawapa revelations au baraka za Mungu kwa imani ya kupata maisha ya furaha mbinguni au kwa njia ya kupata mali na heri hapa duniani.
Vichaa hawatoisha na ukitaka kufanikiwa kua tajiri tumia Maarifa uliyonayo kujitajirisha kupitia vichaa wachache, jilipue tumia hata vitabu vya dini hususani biblia kujitajirisha hakuna ataekataa maana vichaa kila siku wanaozaliwa

Inafahamika kila binadamu ana kiwango au kiasi au percentage fulani za ukichaa, Sasa wale ambao ukichaa wao umepitiliza ndio hao wanaomezeshwa udini wamekua watumwa wakubwa wa dini yaan yeye kutwa kucha kukesha kufuata mchungaji fulani sijui nabii fulan huku wenzao wanapiga pesa wanatajirika wanaongeza manyumba, magari, mashamba, viwanja, mahekari kwa mahekari, wengine wana mpaka mahoteli ya kifahari kupitia biashara ya dini

Shtuka!

Naongezea nje ya mada: kuna jamaa humu nilikua nasikia akilalamika oooh Azam hawaajiri watu wa Imani nyingine ooh Azam hawapigi jingle ya Christmas nikakaa nikatafakari, Sasa nikikaa nikisikiliza ile Jingle ya Azam 'burudani kwa wote' ni kwaya muundo wa Zabron Singer's, najiuliza how come ? Kumbe nimebaini ni namna ya kutumia Maarifa ya Marketing kuwadaka na kuwakamata wale wote wapenda kwaya waliowengi na waliowengi kweli kweli wanaopenda kwaya maana waimba kwaya wengi ni masikini, namaanisha waimba kwaya sio watumbuizaji wa kwaya maana hao ni watu wawili tofauti kuna waimbaji na watumbuizaji
 
Kila mtu ana role yake, hatuwezi wote kuwa wakulima au wote kuwa wanazuoni.

Sisi wenye familia (watoto) tunathamanini SANA uwepo wa watu wanaochukua role ya kufundisha mambo ya kiroho.

Wachugaji, mashehe, gurus n.k, wote tunawathamini SANA.

Otherwise watoto wetu tunakuwa tumewaachia watu wachafu wachafu wafundishe watoto wetu petty materialistic things na mengine ya kuchefua na kutia kinyaa.

Walimu wa kiroho kazi iendelee ❤️❤️
 
Hata Musa hakuweza kumfanikisha dada yake Miriam na kaka yake Haruni
Wala Yesu hakuweza kumfanya binamu yake Yuda kufanikiwa

Tumia akili kidogo kuelewa utendaji wa Mungu
Huyo musa,miriam na haruni au yesu na yuda wanahusika vipi na Afrika bwana mbona unakuwa JINGA kiasi hiki unvezaliwa ukakuta baba au mama yako ni muislam siungekuwa muislam?

Au hiyo dini uliyorithi kwa baba na mama yako walizaliwa nayo?

Utumwa wa kifikira ulionao ni mbaya kuliko ugonjwa wa ukoma,wanaojifanya wameikomnoa Afrika ni waongo bali wamewabakizia utumwa WA FIKIRA na kuiga maisha ya wazungu na kusahau maisha na mila za KIAFRIKA
 
Role ya kiroho kwa watoto ni ya baba na mama kuwafundisha mila na destuli za KIAFRIKA zenye kuwajenga kiroho kupitia maadili ya Kiafrika.

Mchungaji ameiga au kuambukizwa mafinzo ya kiroho na mila zankizungu sasa anawafundisha mafunzo ya kiroho yapi hayo yenye kiwajenga au ushoga?

Baba na mama wafunzeni watoto wenu MILA zenu na siyo wafundishwe na wachungaji mila za wazungu.
 
Uenda ujaipata tafsiri vizuri. Nini maana ya mtumishi wa Mungu. Viongozi wa dini ni wawakilishi wa wanadamu na Mungu. Msingi wa hoja ni pale mtu anapokwenda kinyume na maandiko na wewe ukamfuata bila kutazama maandiko.
 
Watumishi wa kweli wa Mungu wapo na wanatambulika na watumishi feki wa Mungu wanatambulika
 

Kama hujui wanahusikaje na Afrika tulia tukujuze
Musa, Haruni na Miriam walizaliwa Misri iliyopo Africa.
Mke wa Musa alitoka Sudani
Yesu alilelewa Afrika
 
Dunia imechoka sana kila mtu natumie akili yake kumuomba Mungu wake maana hawa madalali wamekuwa wengi sana na wamesababisha madhara mengi sana kwa watu, imagine ,JItu linatoa tako kabisa lkini linadiriki kusimama mbele ya watu na kuwahubiria habari za Mungu, haya mambo ni magumu sana , angalia lile la kule Kenya limeua watu neti waende kwa mungu, stupid kabisa limekamatwa bado majinga na mazuzu yake yanaacha hata kutafuta ugali kwasababu yana njaa yamezagaa na kumiminika nje ya mahakama eti liuaji lao liachiwe, kuna mahala unafika unaona kama kizazi cha sasa hivi cha wapenda maajabu na miujiza kimeshapotea kabisaaaaaaa hasa kina mama , hilo halina ubishi
 
Hakika mkuu, ni mambo mengi sana ya kujiuliza, yaani hawa watu usanii umekua mwingi
 
Kama ambavyo watoto wanaenda shule kupata elimu ya ulimwengu wa kimwili lazima waende shule ya kiroho kupata elimu ya kiroho, kutoka kwa watu walichagua hilo kuwa fungu lao, yaani kuwa walimu wa kiroho.

Mama na baba wata play part yao lakini umuhimu wa shule mahususi unabaki pale pale.

Wageni wamejenga institutions zao, wameandika vitabu vyao, wengine shule zao ni kukremisha maelfu ya mistari tena sio kuwa kusoma, kwa kumsikiliza mwalimu, wanaona kutoa elimu kwa mdomo ni muhimu zaidi kuliko kwa maandishi, na wamefanikiwa kurithisha elimu kwa vizazi na vizazi kwa maelfu ya miaka (naongelea Wahindu ).

Institutions zetu waafrika ziko wapi? Maandishi yetu yako wapi? Utamaduni upi wa kiafrika unarithisha elimu isiyobadilika kutoka kizazi mpaka kizazi?

Hata waganda wenyewe simulizi lao la Kintu (binadamu wa kwanza) sijui kama wanalijua. Isingekua huyo mzungu kuliandika lingepotea!


Me I'm not against "mila na desturi" but there's nothing much there, especially spiritual knowledge! Or rather wanaoijua hawaoni umuhimu kuwapa wengine!
 
Kabla ya wazungu kuleta madhebu ya dini za kijinga hizo shule za kiroho zilikuwa wapi na walimu wa kiroho walikuwa kina nani kama siyo WAZAZI?

Elimu ya kiroho na kidunia vyote vilisambazwa na WAZAZI kwa kuwarithisha watoto wao kupitia mila zao na desturi zao sasa huu ujinga wa kikristu kwanini usambazwe na wachungaji waliorithi kutoka kwa wazungu/wakoloni?

Ujinga huu wa ukristu na uislam umefikia mwisho ni swala la muda tu.
 
Hasa mitaa ya Kawe na Mwenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…