MUNGU HAWEZI KUKUOKOA MBELE YA MWANAMKE ALIYEAMUA KUKUANGAMIZA. UNAJUA NI KWA NINI?
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Hii ni siri hutokuja uambiwe popote. Na leo nitakuambia.
Mungu anaweza kukuokoa dhidi ya serikali.
Mungu anaweza kukuokoa dhidi ya majambazi yenye silaha.
Mungu anaweza kukuokoa na ajali kubwa, iwe ya moto, gari, ndege au meli.
Mungu anaweza kukuokoa na magonjwa makubwa, akakuponya kabisa.
Kiufupi Mungu anaweza kukuokoa na mambo mazito, sijui uchawi na ushirikina.
Lakini Kamwe Mungu hawezi kukuokoa dhidi ya mwanamke. Mwanamke wako uliyemchagua aliyeamua kukuangamiza.
Mungu hawezi kukuokoa na kitu unachokipenda kwa moyo wote.
Mwanamke.
Mungu hawezi kukuokoa na kitu unachokipenda na unachokitawala. Hilo Sahau.
Ni kwamba, Mungu hawezi kukuokoa na Mapenzi. Kwa sababu mapenzi ni hiyari yako. Ni upendo. Kitu unachokipenda kwa moyo wako wote Mungu hana ubavu wala nguvu ya kukidhibiti kisikudhuru.
Na katika kitu hicho usiombe kikawa mwanamke. Kwa sababu ndio kabisa hutookoka.
Mwanaume anapokutana na Mwanamke. Anakuwa na machaguo mawili.
Kumfuata Mungu(yeye) mwenyewe. Au kumfuata Mwanamke.(hisia zake).
Mwanaume unapokutana na mwanamke. Sharti lakwanza lazima ujue Wewe ni Mwanaume. Mtawala. Usichague Mapenzi dhidi ya mamlaka yako. Heshima yako. Kwa sababu hutookoka. Lazima utaangamia iwe leo au kesho.
Mwanaume ni mtawala. Na unaposema utawala unamaanisha kujidhibiti na kudhibiti yanayokuzunguka.
Unaposhindwa kujidhibiti moyo wako. Una anguka katika mapenzi. Tayari umekabidhi mamlaka yako(Ya Mungu) kwa mwanamke au mwanaume mwingine.
Unapomsikiliza mwanamke ujue unasikiliza sauti ya mwanaume mwingine ambaye unaweza ukawa unamjua au humjui.
Inaweza kuwa ni Ex zake, inaweza kuwa ni Baba yake, babu zake au shetani mwenyewe.
Mwanamke kazi yake ni kusikiliza tuu. Wewe kama mwanaume kazi yako ni kutoa maelekezo. Wewe ni mfano wa Mungu.
Hakuna namna utafanya Mungu akakusikiliza. Huna namna yoyote ya kumpa maelekezo Mungu. Kwa sababu yeye ndiye Mungu, mtawala. Mfalme wa yote.
Mwanaume unapomsikiliza mwanamke ndipo anguko lako linapoanzia. Mwisho wako. Na wote waliokaidi yaliwakuta makubwa.
Historia inatuambia hivyo.
Mwanamke anatakiwa akushauri kwa yale uliyokwisha kumwambia. Malengo yako dhidi ya familia na ufalme uwako. Na sio yeye kuja ma new idea. Hakuna New Idea kwa mwanamke.
Hiyo Idea yake lazima iwe na chanzo ambacho sio yeye.
Mwanamke hajawahi kuwa chanzo. Mwanamke sio chanzo cha chochote hapa Duniani
Mwanamke ni chombo cha kukuza na kulea vitu vilivyoanzishwa.
Mwanamke hajawahi kuwa chanzo cha Mabaya, dhambi.
Na hajawahi kuwa chanzo cha Wema na utakatifu.
Ndio maana falme zinazoanguka zinaangushwa na Wanawake lakini wanawake ni wanatumika tuu. Lakini chanzo halisi ni wanaume.
Ni kazi yako mwanaume kumtumia mkeo akukuzie mawazo, maono, ndoto zako. Kama ulimpa mbegu yeye akapata mimba, akakuletea watoto. Ndio hivyohivyo kwenye mambo mengine.
Sio kila mtu anaweza kunielewa.
Ndio maana wanawake mara zote hawakoseagi hata ukiwaona wana makosa. Wao hawakoseagi. Kwa sababu wao wanatumika tuu kama wabebaji na wakuzaji wa mambo ila chanzo cha yote ni Wanaume.
Tunasema kuanguka kwa Familia na maisha chanzo ni mwanaume yeye mwenyewe au mwanaume mwingine.
Ili mwanamke akuangushe hatakulazimisha. Utampenda wewe mwenyewe kwa hiyari yako. Utafanya kwa hiyari yako huku ukijua kwamba unalofanya ni kosa.
Mwanaume hakosei kwa bahati mbaya.
Ila wanawake sio wakati wote wanafanyaga makusudi kukosea.
Mara nyingine wao hujukuta wamekosea tuu.
Wana hali nyingi zinazowasababisha kufanya makosa.
Kimaumbile na kiroho. Ndio maana ukioa na kuishi mwanamke utagundua kwamba ni viumbe wazuri, lakini wanashambuliwa kiroho na kimwili. Na ni wepesi kufanya makosa, uzembe na kusahau
Kwenda Hedhi, kupagawa mapepo, na matatizo mengine ya kisaikolojia ni sehemu ya wao kuwa hivyo walivyo.
Itashangaza sana na wao hushangaa pale ambapo utawaamini kwamba wanauwezo. Wanashangaa.
Ingawaje miaka na miaka hujitahidi kuwa wakamilifu, kuonyesha uwezo lakini uhalisia unawakataa. Na wengi hujikuta wakichoka.
Ni jukumu la mwanaume kujilinda. Kwa sababu Mungu hatakulinda dhidi ya mwanamke ambaye ulitakiwa wewe ndiye umlinde na kumuongoza. Wewe unatumia hisia zako kumpenda na kumuongoza.
Nimemaliza.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam.