Mungu kaumba vyote lakini kasoro kitu kimoja

Mungu kaumba vyote lakini kasoro kitu kimoja

Nirvana G7

Member
Joined
Nov 5, 2024
Posts
35
Reaction score
66
Habar za jion wakuu,

I hope mko good.

Kama kichwa cha hoja kinavyojieleza, nilikua najihusisha sana na mambo ya dini na hiyo ilikua baada ya kuwa najikuta kuwa na doughts nyingi kuhusiana na uwepo wa mungu. Kwa sasa nimepata majibu lakin ndipo nikaja kugundua pia kwamba huyu Mungu niliekuwa na mashaka naye hakuyaumba maji

Kwanini ninasema hivyo?

Kwasababu katika kusoma Biblia sjaona mahali palipo andikwa kuwa Mungu aliyaumba maji (kama kuna mtu anaushahidi aulete). Hivyo kwa akili yangu nafikiri kuwa maji ni kitu ambacho ni cha kale katika dunia kwa kiasi cha kuwa yana kumbukumbu ya kila kitu kilicho tokea duniani tangu kale.

Pia nina imani maji yana nguvu za uponyaji alafu pia maji ni muhitajika muhimu sana wa viumbe vyote vilivyo hai ulimwenguni hivyo maji yana nafasi kubwa katika maisha ya hapa duniani.

Kama kuna mtu anahoja juu ya hili ailete tujuzane vizuri.

Asanteni nafungua mjadala.
 
Habar za jion wakuu
I hope mko good.

Kama kichwa cha hoja kinavyojieleza, nilikua najihusisha sana na mambo ya dini na hiyo ilikua baada ya kuwa najikuta kuwa na doughts nyingi kuhusiana na uwepo wa mungu. Kwa sasa nimepata majibu lakin ndipo nikaja kugundua pia kwamba huyu Mungu niliekuwa na mashaka naye hakuyaumba maji

Kwanini ninasema hivyo?

Kwasababu katika kusoma biblia sjaona mahali palipo andikwa kuwa mungu aliyaumba maji(kama kuna mtu anaushahidi aulete). Hivyo kwa akili yangu nafikiri kuwa maji ni kitu ambacho ni cha kale katika dunia kwa kiasi cha kuwa yana kumbukumbu ya kila kitu kilicho tokea duniani tangu kale.

Pia nina imani maji yana nguvu za uponyaji alafu pia maji ni muhitajika muhimu sana wa viumbe vyote vilivyo hai ulimwenguni hivyo maji yana nafasi kubwa katika maisha ya hapa duniani.

Kama kuna mtu anahoja juu ya hili ailete tujuzane vizuri.

Asanteni nafungua mjadala.
Hivi kwamfano nikichukua pure oxygen na pure natural Hydrogen.
Nikaenda maabara kutengeneza Maji.
Hapo nitakuwa nimeumba maji?

Kwasababu hyo oxygen na hiyo Hydrogen itakuwa ndiyo kwa mara ya kwanza vimekua maji, nitakuwa nimeleta maji mapya ulimwenguni
Je nitakuwa nimeumba maji?
 
Hauko mbali na ukweli Mwenyezi Mungu kitu cha kwanza kuumba ni maji, halafu akaumba vyote vilivyofuata kutoka katika maji. Na ni kweli maji yananguvu lakini kiumbe chenye nguvu na thamani zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni binadamu
 
Mithali 8:23-27

[23]Nalitukuka tokea milele, tangu awali,
Kabla haijawako dunia.
I was set up from everlasting, from the beginning, or ever the earth was.

[24]Wakati visipokuwako vilindi nalizaliwa,
Wakati zisipokuwako chemchemi zilizojaa maji.
When there were no depths, I was brought forth; when there were no fountains abounding with water.

[25]Kabla milima haijawekwa imara,
Kabla ya vilima nalizaliwa.
Before the mountains were settled, before the hills was I brought forth:

[26]Alipokuwa hajaiumba dunia, wala makonde
Wala chanzo cha mavumbi ya dunia;
While as yet he had not made the earth, nor the fields, nor the highest part of the dust of the world.

[27]Alipozithibitisha mbingu nalikuwako;
Alipopiga duara katika uso wa bahari;
When he prepared the heavens, I was there: when he set a compass upon the face of the depth:
 
Screenshot_20241117-102042_Biblia.jpg
 
Back
Top Bottom