Mungu kaumba vyote lakini kasoro kitu kimoja

Mungu kaumba vyote lakini kasoro kitu kimoja

Roho ya Mungu ilikua juu ya uso wa vilindi vya maji kabla hajaanza uumbaji kulingana na biblia..
Umewahi kujiuliza hivyo vilindi vya maji vilikuwa vimetuama juu ya kitu gani? Ni ardhi? Kama ni ardhi, nitakuwa nakosea nikisema ardhi ilitangulia kabla ya maji? Na kama ardhi ilitangulia... Material ya kuiumba hiyo ardhi yalitoka wapi
 
Hauko mbali na ukweli Mwenyezi Mungu kitu cha kwanza kuumba ni maji, halafu akaumba vyote vilivyofuata kutoka katika maji. Na ni kweli maji yananguvu lakini kiumbe chenye nguvu na thamani zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni binadamu
Hayo maji yalikuwa yanaelea angani?
 
Umewahi kujiuliza hivyo vilindi vya maji vilikuwa vimetuama juu ya kitu gani? Ni ardhi? Kama ni ardhi, nitakuwa nakosea nikisema ardhi ilitangulia kabla ya maji? Na kama ardhi ilitangulia... Material ya kuiumba hiyo ardhi yalitoka wapi
Roho ya Mungu kabla haijatulia juu ya vilindi vya maji ilitokea wapi?
 
Kwa Mungu. Na wewe jibu
Mungu alikua na Mungu wake, Na Mungu wake naye aliumbwa na Mungu wake na Mungu wake naye ana Mungu wake... mtiririko hauna kikomo ..!!

🔴Dax-Eternity
 
Habar za jion wakuu,

I hope mko good.

Kama kichwa cha hoja kinavyojieleza, nilikua najihusisha sana na mambo ya dini na hiyo ilikua baada ya kuwa najikuta kuwa na doughts nyingi kuhusiana na uwepo wa mungu. Kwa sasa nimepata majibu lakin ndipo nikaja kugundua pia kwamba huyu Mungu niliekuwa na mashaka naye hakuyaumba maji

Kwanini ninasema hivyo?

Kwasababu katika kusoma Biblia sjaona mahali palipo andikwa kuwa Mungu aliyaumba maji (kama kuna mtu anaushahidi aulete). Hivyo kwa akili yangu nafikiri kuwa maji ni kitu ambacho ni cha kale katika dunia kwa kiasi cha kuwa yana kumbukumbu ya kila kitu kilicho tokea duniani tangu kale.

Pia nina imani maji yana nguvu za uponyaji alafu pia maji ni muhitajika muhimu sana wa viumbe vyote vilivyo hai ulimwenguni hivyo maji yana nafasi kubwa katika maisha ya hapa duniani.

Kama kuna mtu anahoja juu ya hili ailete tujuzane vizuri.

Asanteni nafungua mjadala.
Maji yatakua yalijiumba yenyewe kwa kweli....
 
Mtume Paulo alielezea jinsi alivyoitwa kuwa mtume wa Yesu Kristo kupitia maandiko kadhaa katika Agano Jipya.

Hapa kuna baadhi ya maandiko muhimu yanayoelezea jinsi Paulo alivyoitwa katika utume:

1. Matendo ya Mitume 9:1-19

Hii ni simulizi ya kwanza kuhusu jinsi Paulo (akitajwa kama Sauli) alivyokutana na Yesu Kristo akiwa safarini kuelekea Damasko. Katika maono hayo, Sauli aliona nuru kubwa kutoka mbinguni, akasikia sauti ya Yesu ikisema:
"Sauli, Sauli, mbona unanitesa?"
Baada ya tukio hili, Sauli alipofika Damasko, alibadilika baada ya maombi ya Anania, kisha akabatizwa na kuanza kazi ya kumtumikia Mungu.

2. Matendo ya Mitume 22:6-16

Paulo alisimulia tukio la wito wake kwa viongozi wa Kiyahudi. Hapa alieleza jinsi alivyopofushwa na nuru kutoka mbinguni na jinsi Yesu alivyomtuma kwa Anania ambaye alimrudishia kuona na kumpa ujumbe wa kuwa shahidi wa Kristo.

3. Matendo ya Mitume 26:12-18

Paulo alieleza wito wake mbele ya Mfalme Agripa. Katika simulizi hii, anasema Yesu alimwambia:
"Nimekutokea kwa sababu hii, ili nikufanye uwe mtumishi na shahidi wa mambo haya ambayo umeyaona na ya mambo mengine nitakayokuonyesha."

4. Wagalatia 1:11-17

Paulo alifafanua kwamba injili aliyohubiri haikutoka kwa wanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Alieleza jinsi alivyoitwa moja kwa moja na Mungu na hakutegemea kufundishwa na binadamu:
"Lakini Mungu, aliyenitenga tangu tumboni mwa mama yangu na kuniita kwa neema yake, alipenda kumdhihirisha Mwana wake ndani yangu, ili niwahubiri mataifa..."

5. 1 Timotheo 1:12-16

Paulo alikiri kuwa kabla ya wito wake alikuwa mwenye dhambi na aliyewatesa Wakristo, lakini alihurumiwa na Mungu ili aonyeshe uvumilivu wa Kristo kwa watu wengine:
"Kristo Yesu alikuja ulimwenguni awaokoe wenye dhambi, ambao mimi ni wa kwanza."

Aya hizi zinaonyesha wazi kwamba wito wa Paulo ulikuwa wa kipekee na wa moja kwa moja kutoka kwa Yesu Kristo, na ulilenga kumfanya mtume kwa mataifa.
Hizo stori hata ZUMARIDI anazo.
Niambie wkt anaitwa alikuwa na nani
 
Kabla ya mwanzo wa anga na wakati Mungu (Elohim, Utatu) alizungumza na kuumba mbingu na dunia, na dunia iliyoumbwa kwayo ilikuwa bila umbo na utupu kabisa, rundo tu la gesi lililokuwa likizunguka katika weusi usio na kitu.

Mungu wetu asiyeonekana akielea juu ya ukungu mzito.

Kisha Mungu akaangaza mahali pale na kusema 'Dunia iwe pande zote!' Na ikawa hivyo. Naye akasema, 'Baadhi ya ukungu mzito utaning'inia duniani kote, na nyingine itatua juu ya nchi.' Na ndivyo ilivyokuwa.
Mkuu umeelezea story ya kuanzia Mungu ameanza kuumba...

Sisi tunahitaji story ya kabla hajaanza kuumba, Asili yake? Alitoka wapi?
 
Basi chukua na hii.
Mungu hakuumba dhahabu wala madini.
Maahana hakuna popote kwenye maandiko vilipoongelewa specifically
 
Iyo gharika sidhani kama maji yalitoka chini bali juu baada ya mifuniko ya mbingu kufunguka kwani mkuu bado unaamini kuwa dunia ni duara maana nnachojua mm dunia ni flat na ni closed system ambapo hakuna awezaye kutoka na ninichojua pia kuna mabara zaidi yaa 100.
Chini ya baharia kuna chemchem za maji nyingi Tu.Na zilichangia maji ya gharika.
 
Habar za jion wakuu,

I hope mko good.

Kama kichwa cha hoja kinavyojieleza, nilikua najihusisha sana na mambo ya dini na hiyo ilikua baada ya kuwa najikuta kuwa na doughts nyingi kuhusiana na uwepo wa mungu. Kwa sasa nimepata majibu lakin ndipo nikaja kugundua pia kwamba huyu Mungu niliekuwa na mashaka naye hakuyaumba maji

Kwanini ninasema hivyo?

Kwasababu katika kusoma Biblia sjaona mahali palipo andikwa kuwa Mungu aliyaumba maji (kama kuna mtu anaushahidi aulete). Hivyo kwa akili yangu nafikiri kuwa maji ni kitu ambacho ni cha kale katika dunia kwa kiasi cha kuwa yana kumbukumbu ya kila kitu kilicho tokea duniani tangu kale.

Pia nina imani maji yana nguvu za uponyaji alafu pia maji ni muhitajika muhimu sana wa viumbe vyote vilivyo hai ulimwenguni hivyo maji yana nafasi kubwa katika maisha ya hapa duniani.

Kama kuna mtu anahoja juu ya hili ailete tujuzane vizuri.

Asanteni nafungua mjadala.
hilo Neno doughts badala ya doubt linadhihirisha Bado elimu/maarifa na uwezo wa akili yako ni ndogo kufikia kuujua ukuu wa Mungu...D nne zinakuhusu
 
Back
Top Bottom