Mungu kutupa ubongo/akili huenda alimaliza kila kitu

Mungu kutupa ubongo/akili huenda alimaliza kila kitu

Habari gani wakuu?

Kama kinavyo jieleza kichwa Cha uzi hapo juu kwamba...

Kama ilivyo kwa gali mpya uinunuapo Basi lazima utapewa tool box ambayo itakuwa na vifaa vyote mhimu kwa ajili ya kuitengenezea gali yako itakapo pata tatizo la kiufundi

Basi hivyo ndivyo ilivyo kwa ubongo juu ya mwili wako

Kiumbe chochote chenye damu kina ubongo nahii nikwasababu muumbaji alijua kwamba Kama ataumba kiumbe akamkamilisha pasipo ubongo

Basi muumbaji angekuwa nakazi kubwa ya kuwaambia viumbe hao fanya hivi na hivi ili uepuke hili na hili

Fanya hivi nahivi ili upate hiki nahiki au ukwepe hiki na hiki

Hebufikilia huenda tusinge lala kama tungekuwa hatuna ubongo Wala kuamka Kama tungekuwa hatuna ubongo

Tusinge tafuta chakula bila ubongo Wala kujiskia njaa bila ubongo

Ubongo nikama dash board..

kwenye gali hutoa ishara Kama mafuta yameisha

Hutoa ishara pia kama mlango haukufungwa vizuli

Hutoa ishara pia kama hauku vaa mkanda wa usarama wako

Hivyo hivyo kwenye mwili wako ukiumwa kichwa haimaanishi unaumwa kichwa Bali tafsiri yake nikwamba ubongo una kupa taarifa kwamba

Kuna sehemu ya mwili wako Ina tatizo

Labda tumbo, joints,skio, ini,Figo nk

Ubongo wa mwanadamu ndiyo hukuambia kwamba hapa Panajua Kali kaa kivulini..

Ubongo ndiyo huupumzisha mwili kwa usingizi na huu amsha mwili baada ya kupumzika kwa kuutoa usingizi

Ubongo ndiyo unao miliki kumbu kumbu zote Kama za wanyama wakali,wapole, Wala majani,Wala nyama,nk

kwamfano...

utembeapo polini ukakutana na Simba chakwanza macho humwona Simba"..

.. baada ya kumwona Simba macho hupeleka taarifa ya taswira ya Simba kwenye ubongo

baada ya ubongo kuipokea taswila huingia kwenye chumba Cha ubongo Cha kumbu kumbu ili kuzipata taarifa za taswila iliyo onekana

Kupita Kumbu kumbu zake ubongo Hutoa taarifa kwamba taswila ya mnyama aliye onekana jina lake anaitwa Simba"

nimnyama mla nyama na huweza kuula hata mwili wa mwana damu

Ubongo hauishii hapo Hutoa sifa za Simba pia kwamba mnyama huyo Ana nguvu,nimjuzi wa kukimbia na udhaifu wake nikushindwa kupanda miti hasa iliyo simama wima

Baada ya hapo ubongo utakuwa umetoa tahadhali kwamba mwili upo sehemu hatari

Kitakacho fwata baada ya hapo ubongo huziamsha hormones/vimiminika maarumu vilivyomo ndani ya mwili kwa ajili ya ulinzi wa mwili kwa wakati maarumu

Kwa mfano Kuna hormone inaitwa adrenalin inayo tokana na adrenal

Baada ya ubongo kuona hatari ya Simba hormoni hii huamuliwa na mfumo wa ubongo kuvujia

Baada ya kuvujia hormone hiyo husafiri mpak kwenye Moyo ambako ikifika kwenye Moyo husababisha mapigo ya Moyo kwenda Kasi

Mapigo ya Moyo yakianza kwenda Kasi hupeleka mfumonwa upumuaji kwenda Kasi pia/kupumua haraka haraka

Kupumua haraka haraka hupeleka uingizaji wa Kasi wa oksjean/hewa safi kwenye mapafu

Kisha oksjean hiyo husafilishwa mpaka kwenye misuri ya mwili Kama misuri ya mikono,miguu,mapaja,shingo,macho,nk kwa ajili ya kiweka misuri imara ili kujiandaa na uvamizi/

Baada ya oksjean kujaa kwenye misuri misuri huanza kuumukakutanuka nakuwa tayali kwa lolote ambapo inaweza kuwa kupambana na Simba au kumkimbia Simba

Na chaajabu Mambo yote hayo hufanyika ndani ya sekunde tu na ubongo""

Hapa ndipo ninapo sema wanao sema mungu hayupo

Je! Wana dhani ninani alibuni uwezo huu wa ubongo kujiendesha wenyewe Tena kwa mda mfupi kiasi hicho?

Ukiumwa ubongo ndiyo hufanya mchakato mzima wa kupambana na ugonjwa hata kabla ya wewe ndugu na jamaa kujua kwamba unaumwa

Mpaka unakuja kujua ubongo tayali ulisha kupa tahadhali nyingi Sana pasipo wewe kujua..

na tahadhali zenyewe nikama ifwatavyo...

kichwa kuuma,misuri ya macho kucheza cheza,vichomi kwa mbali mbavuni,chini ya kitovu,miwasho sehemu za siri,chafya kuharisha ,kutapika,kusinzia mchana, nk

Hizo zote nanyingine ambazo sijaziandika ni ishara kwamba mwili uki ratibiwa na ubongo unapambana na Mambo mazito ndani ya mwili wako

Ndiyo maana wenzetu wazungu mafua huenda hospital,

chafya zikizidi huenda hospital kikohozi huenda hospital

kwani Wana jua kwamba hizo NI dalili za ugonjwa ambao hauja onekana nje

Wao huziita body internal effects

Hivyo ubongo nikiungo kibwa na mhimu Sana kwenye miili yetu

Huwezi amini kwamba..

katika zawadi kubwa ambazo mungu alitupa Basi ubongo ni number moja

Huwezi amini nikisema hivyo utasema vipi kuhusu Moyo?

Nami nitakujibu hata Moyo ili udunde una utegemea ubongo Tena ubongo wa nyuma

Ujasiri, uvumilivu,upole,ukali utulivu, vyote vipo ndani ya ubongo

Naweza kusema mwanadamu bila ubongo nikama simu yako hiyo with no settings ni bike kabisa

Mwanadamu bila ubongo nikama gali with no tool box that mean nothing

Ubongo ndiyo msingi wa kila vumbuzi unazo ziona Leo kuanzia Moto,umeme, phones,magari,x Ray's,robots,saa,majumba,hesabu, computers, guns, bomb's, nk

Kuna maajabu mengi ya ubongo ambayo ukiya fikia ukajua kuutumia ubongo wako vizuli utaishi Kama uko peponi

Je Usha wai kuskia kuhusu meditation?

Jifunze utakutana na mengi ya kustaajabisha haya yote yapo ndani ya ubongo

Nihitimishe kwa kusema...

Kuna usemi wanasema mungu hakupi jalibu usilo liweza

Huenda walimaanisha kwamba tatizo lolote litakalo kuja juu yako utatuzi wake mungu aliuweka katika ubongo wako

Nikama vile tatizo lolote litakalo tokea kwenye simu yako/computer yako Basi ingia settings utalitatua kwani mzungu aliu weka utatuzi wake huko

Ubongo ni body settings utumie vizuli utakusaidia na mengi Sana

Mungu yupo lakini katupa msaidizi mkuu badara yake ambaye ni ubongo na ndani yake naye yumo na hutenda kazi kupitia humo

Kama asemavyo Mimi ni ndani yenu nanyi mu ndani yangu
Bwana ni mwema.
 
Naona ya 2 na 3 zina uhusiano na ubongo na ya 1 inauhusiano na mwili, hivyo ukivichanganya ndio vinakuwa na impact kubwa
Wacha namie nijaribu Kutafakari labda naweza pata jambo... Lakini kwa fikra za haraka nimeona kama hizo ni sababu ndogo sana kuweza kumfanya mwanadamu awe kama ambayo yuko.

Embu jaribu kuangalia haya mabadiliko yanayoendelea duniani, katika namna mbili, tuseme chukulia kuanzia mwaka 1950 labda kwenda mbele na kuanzia mwaka huo kurudi nyuma.

Then jaribu kuchukua hizo sababu ziweke hapo
 
😅😅 nimekuelewa kwamba amendelea kwa kasi kipindi hicho wakati alishakuwa navyo vyote toka zamani au nakosea
 
Mu gu

Mungu hakuumba akili isipokuwa nyoka ndiye aliyewapa akili Adam na Eva wakajua baya na zuri

Ndio alimaliza kila kitu, ila ni kwa nini aliwapendelea wazungu?
Wazungu kiasiri si wajengaji niwa bomoaji

Mambo mengi ambayo wanayafanya

kwamtazamo wetu huyaona Kama ni maendeleo lakini kiukweli ni uharibifu
 
Ubongo hutatua matatizo yote ambayo sio mageni na mazingira yaliyopo kwasababu kazi kubwa ya ubongo ni kumuunga mtu na mazingira ya kidunia, kwahiyo unakariri namna mambo yanavyopaswa kwenda au kuwa kwa kuzingatia matokeo ya Kila yambo huko past, lakini jambo lolote ambalo ni geni na halina historia yoyote kuwepo huwa ubongo hauwezi kulitatua.

Umetolea mfano wa gari ila gari huwa halitoi sign kama halitaongozwa.

Andiko zuri.
🙏🙏🙏
 
Ubongo unapokea Kila unachoulisha🤣🤣🤣
Je! Usha pitia hii?

Kuna wakati una weza kusahau kitu na ubongo ukakuambia Kuna kitu umesahau lakini haujui ninini?

Je! Ushawai kaa sehemu ubongo ukakuambia ondoka hapa ni hatari/machale na baada ya mda mfupi tu kutoka likatokea jambo ambapo linge ku gharimu?

j! Usha wai sahau kitu afu ukagundua usicho kijua kupitia kusahau?

Kuna wakati mama anaweza akawa anafua nje wakati huo akamwacha mototo ndani mtoto akaanza ku sogelea jiko/Moto

Cha ajabu mama akili humtuma ghafra kuingia ndani na hukuta mtoto ana kalibia Moto kabisaa au kuungua"

Je hili nalo nila kujizoesha au niziada katika ubongo na uumbwaji wake?

Au tuseme Kuna uungu/uwezo kidogo wa kuweza kuhisi tusicho kiona mungu aliucha ndani ya bongo zetu?

Ubongo nizaidi ya ubongo Kama utaushughulisha vizuli Sana mkuu
 
Sasa mambo haya yote ambayo umeelezea ni ule uwezo usio wa kawaida ambao mtu yuko nao.

Ubongo huwa unapima uwezo wa akili ya mtu ila mambo hayo ambayo umeyaelezea hapo huwa hayaingii kwenye akili.

Mtu mwenye machale/ muonaji huwezi kumuita ako na akili sana kwakua kila anachokiona hisiani huwa kinatokea kwenye ulimwengu halisi.

Kwenye maisha kila mtu anahitaji mambo mawili tu ili aweze kufanikiwa, cha kwanza ni sauti ya ndani (ambayo hii mara nyingi huwa huwezi kuelezea kwa akili za kawaida) na cha pili ni uwezo wa kuchanganua mambo(ambayo hii mara nyingi huwa ni connection ya ubongo wako wa damu na nyama na ile sauti ambayo haielezeki).

Kwanini nakwambia hivyo, kwasababu swala la future huwa ni swala la kudra, kwahiyo surprise zote ambazo ziko kwenye lisaa lijalo huzijui hata ukiwa na akili kiasi gani hautakaa uzijue ila kitu pekee ambacho kitakuwesesha kujua ni ile sauti ongozi ambayo iko ndani yako.

Kwahiyo ukiwa na hiyo sauti itakufanya usizurure tu kwenye harakati zako bali uweze kupiga hatua za uhakika zaidi lakini ukiwa na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo utaweza kukabiliana na ulimwengu vizuri.

Trust me ubongo pekee hautoshi kukufanya uwe Bora, ila ubongo na ubongo vikiwa na muunganiko mzuri utakua bora sana.
 
Je! Usha pitia hii?

Kuna wakati una weza kusahau kitu na ubongo ukakuambia Kuna kitu umesahau lakini haujui ninini?

Je! Ushawai kaa sehemu ubongo ukakuambia ondoka hapa ni hatari/machale na baada ya mda mfupi tu kutoka likatokea jambo ambapo linge ku gharimu?

j! Usha wai sahau kitu afu ukagundua usicho kijua kupitia kusahau?

Kuna wakati mama anaweza akawa anafua nje wakati huo akamwacha mototo ndani mtoto akaanza ku sogelea jiko/Moto

Cha ajabu mama akili humtuma ghafra kuingia ndani na hukuta mtoto ana kalibia Moto kabisaa au kuungua"

Je hili nalo nila kujizoesha au niziada katika ubongo na uumbwaji wake?

Au tuseme Kuna uungu/uwezo kidogo wa kuweza kuhisi tusicho kiona mungu aliucha ndani ya bongo zetu?

Ubongo nizaidi ya ubongo Kama utaushughulisha vizuli Sana mkuu
Ukitaka uelewe vizuri chukulia mfano wa kawaida tu wa mwanafunzi na mwalimu, kwamba mwalimu anajua maswali ambayo ameyatunga kwenye mtihani ila mwanafunzi hajui maswali yaliyopo kwenye mtihani, licha ya kwamba amesoma notes zake vizuri ila anafanya kuotea otea tu like labda swali potatoes hapa au pale ila hajui exactly wapi swali litatokea.

kuna walimu ambao huwa wanakujaga darasani vipindi vya kuelekea mitihani na huwa wanagusia topic hii au topic ile na katika miguso yao huwa wanatoa ishara zisizo za moja kwa moja na ishara hizi huwa wale wanafunzi werevu wanazigundua na wanapita nazo then mwisho wa siku wakiingia kwenye chumba cha Mtihani wanakutana na yale yale.

Kwahiyo hiyo ihamishe kwenye ubongo wako ya kwamba kazi yake ni kupokea na kuhifadhi ajenda mbalimbali ila ajenda zote za kuhusu future yako hautakaa ujue itaenda kujibiwa na ajenda ipi kati ya hizo ambazo ziko kichwani mwako hadi pale utakapoamua kuwa mwanafunzi mwelevu au kuzingatia kila jambo ambalo lipo katika utaratibu wa ulimwengu (kama mwanafunzi anavyozingatia Kila topic ambayo ipo kwenye silabasi yake)
 
Trust me ubongo pekee hautoshi kukufanya uwe Bora, ila ubongo na ubongo vikiwa na muunganiko mzuri utakua bora sana.
Ila toka mwanzo hatujawa wazi ni nini tunaongelea hasa kumaanisha ubongo je ni Brain, Mind, au consciousness. Maana vyote vitatu vinaweza kuwa na kazi tofauti
 
Ila toka mwanzo hatujawa wazi ni nini tunaongelea hasa kumaanisha ubongo je ni Brain, Mind, au consciousness. Maana vyote vitatu vinaweza kuwa na kazi tofauti
Kulingana na muktadha wa andiko la jamaa ameainisha ubongo kwenye eneo la kumbukumbu zaidi ila all in all hata tukiongea sehemu zote hizo za ubongo bado Mimi nitabaki kwenye hilo eneo😅😅😅
 
Mkuu turekebishane kidogo.

Ubongo siyo msaidizi(Roho)ambaye Mungu ametupa.

Msaidizi ambaye tumeachiwa na Yesu(Roho) moja ya kazi yake(Kama utampokea) ni kuusaidia ubongo wako kuchukua maamuzi sahihi.

Unaposema ubongo ndiye Roho mwenyewe (you're very wrong) ila ukisema ubongo ni makao ya Roho(you're very right).

Roho si kitu touchable kama ubongo ulivyo.

Na pia kumbuka ubongo wa binadamu ni sehemu ya kazi ya Roho wa Mungu wakati wa uumbaji.

Kupewa ubongo haimaanishi Mungu alimaliza kila kitu, bado kuna kazi kubwa ya kufanya kupitia huo ubongo - Ni jukumu zito mno.

God bless you!!
 
Back
Top Bottom