Mungu kutupa ubongo/akili huenda alimaliza kila kitu

Bwana ni mwema.
 
Naona ya 2 na 3 zina uhusiano na ubongo na ya 1 inauhusiano na mwili, hivyo ukivichanganya ndio vinakuwa na impact kubwa
Wacha namie nijaribu Kutafakari labda naweza pata jambo... Lakini kwa fikra za haraka nimeona kama hizo ni sababu ndogo sana kuweza kumfanya mwanadamu awe kama ambayo yuko.

Embu jaribu kuangalia haya mabadiliko yanayoendelea duniani, katika namna mbili, tuseme chukulia kuanzia mwaka 1950 labda kwenda mbele na kuanzia mwaka huo kurudi nyuma.

Then jaribu kuchukua hizo sababu ziweke hapo
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… nimekuelewa kwamba amendelea kwa kasi kipindi hicho wakati alishakuwa navyo vyote toka zamani au nakosea
 
Mu gu


Mungu hakuumba akili isipokuwa nyoka ndiye aliyewapa akili Adam na Eva wakajua baya na zuri

Ndio alimaliza kila kitu, ila ni kwa nini aliwapendelea wazungu?
Wazungu kiasiri si wajengaji niwa bomoaji

Mambo mengi ambayo wanayafanya

kwamtazamo wetu huyaona Kama ni maendeleo lakini kiukweli ni uharibifu
 
๐Ÿ™๐Ÿ™๐Ÿ™
 
Ubongo unapokea Kila unachoulisha๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ
Je! Usha pitia hii?

Kuna wakati una weza kusahau kitu na ubongo ukakuambia Kuna kitu umesahau lakini haujui ninini?

Je! Ushawai kaa sehemu ubongo ukakuambia ondoka hapa ni hatari/machale na baada ya mda mfupi tu kutoka likatokea jambo ambapo linge ku gharimu?

j! Usha wai sahau kitu afu ukagundua usicho kijua kupitia kusahau?

Kuna wakati mama anaweza akawa anafua nje wakati huo akamwacha mototo ndani mtoto akaanza ku sogelea jiko/Moto

Cha ajabu mama akili humtuma ghafra kuingia ndani na hukuta mtoto ana kalibia Moto kabisaa au kuungua"

Je hili nalo nila kujizoesha au niziada katika ubongo na uumbwaji wake?

Au tuseme Kuna uungu/uwezo kidogo wa kuweza kuhisi tusicho kiona mungu aliucha ndani ya bongo zetu?

Ubongo nizaidi ya ubongo Kama utaushughulisha vizuli Sana mkuu
 
Sasa mambo haya yote ambayo umeelezea ni ule uwezo usio wa kawaida ambao mtu yuko nao.

Ubongo huwa unapima uwezo wa akili ya mtu ila mambo hayo ambayo umeyaelezea hapo huwa hayaingii kwenye akili.

Mtu mwenye machale/ muonaji huwezi kumuita ako na akili sana kwakua kila anachokiona hisiani huwa kinatokea kwenye ulimwengu halisi.

Kwenye maisha kila mtu anahitaji mambo mawili tu ili aweze kufanikiwa, cha kwanza ni sauti ya ndani (ambayo hii mara nyingi huwa huwezi kuelezea kwa akili za kawaida) na cha pili ni uwezo wa kuchanganua mambo(ambayo hii mara nyingi huwa ni connection ya ubongo wako wa damu na nyama na ile sauti ambayo haielezeki).

Kwanini nakwambia hivyo, kwasababu swala la future huwa ni swala la kudra, kwahiyo surprise zote ambazo ziko kwenye lisaa lijalo huzijui hata ukiwa na akili kiasi gani hautakaa uzijue ila kitu pekee ambacho kitakuwesesha kujua ni ile sauti ongozi ambayo iko ndani yako.

Kwahiyo ukiwa na hiyo sauti itakufanya usizurure tu kwenye harakati zako bali uweze kupiga hatua za uhakika zaidi lakini ukiwa na uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo utaweza kukabiliana na ulimwengu vizuri.

Trust me ubongo pekee hautoshi kukufanya uwe Bora, ila ubongo na ubongo vikiwa na muunganiko mzuri utakua bora sana.
 
Ukitaka uelewe vizuri chukulia mfano wa kawaida tu wa mwanafunzi na mwalimu, kwamba mwalimu anajua maswali ambayo ameyatunga kwenye mtihani ila mwanafunzi hajui maswali yaliyopo kwenye mtihani, licha ya kwamba amesoma notes zake vizuri ila anafanya kuotea otea tu like labda swali potatoes hapa au pale ila hajui exactly wapi swali litatokea.

kuna walimu ambao huwa wanakujaga darasani vipindi vya kuelekea mitihani na huwa wanagusia topic hii au topic ile na katika miguso yao huwa wanatoa ishara zisizo za moja kwa moja na ishara hizi huwa wale wanafunzi werevu wanazigundua na wanapita nazo then mwisho wa siku wakiingia kwenye chumba cha Mtihani wanakutana na yale yale.

Kwahiyo hiyo ihamishe kwenye ubongo wako ya kwamba kazi yake ni kupokea na kuhifadhi ajenda mbalimbali ila ajenda zote za kuhusu future yako hautakaa ujue itaenda kujibiwa na ajenda ipi kati ya hizo ambazo ziko kichwani mwako hadi pale utakapoamua kuwa mwanafunzi mwelevu au kuzingatia kila jambo ambalo lipo katika utaratibu wa ulimwengu (kama mwanafunzi anavyozingatia Kila topic ambayo ipo kwenye silabasi yake)
 
Trust me ubongo pekee hautoshi kukufanya uwe Bora, ila ubongo na ubongo vikiwa na muunganiko mzuri utakua bora sana.
Ila toka mwanzo hatujawa wazi ni nini tunaongelea hasa kumaanisha ubongo je ni Brain, Mind, au consciousness. Maana vyote vitatu vinaweza kuwa na kazi tofauti
 
Ila toka mwanzo hatujawa wazi ni nini tunaongelea hasa kumaanisha ubongo je ni Brain, Mind, au consciousness. Maana vyote vitatu vinaweza kuwa na kazi tofauti
Kulingana na muktadha wa andiko la jamaa ameainisha ubongo kwenye eneo la kumbukumbu zaidi ila all in all hata tukiongea sehemu zote hizo za ubongo bado Mimi nitabaki kwenye hilo eneo๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…
 
Mkuu turekebishane kidogo.

Ubongo siyo msaidizi(Roho)ambaye Mungu ametupa.

Msaidizi ambaye tumeachiwa na Yesu(Roho) moja ya kazi yake(Kama utampokea) ni kuusaidia ubongo wako kuchukua maamuzi sahihi.

Unaposema ubongo ndiye Roho mwenyewe (you're very wrong) ila ukisema ubongo ni makao ya Roho(you're very right).

Roho si kitu touchable kama ubongo ulivyo.

Na pia kumbuka ubongo wa binadamu ni sehemu ya kazi ya Roho wa Mungu wakati wa uumbaji.

Kupewa ubongo haimaanishi Mungu alimaliza kila kitu, bado kuna kazi kubwa ya kufanya kupitia huo ubongo - Ni jukumu zito mno.

God bless you!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ