Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Mungu maana yake ni nini? Au Mungu ni nini?

Hili swali , " Muumbaji aliumbwa na nani " inatakiwa lielekezwe kwa muumbaji mwenyewe ndio atakupa majibu sahihi, Lakini kumuuliza mtu aliyeumbwa swali kama hili logically muulizaji anaonekana ni mpumbavu.
.Sasa mbona umejibu wewe? Na mbona nyinyi wafia dini mda wote mnahubiri habari za Mungu! kwanini msikitulize kipira hiko mkaacha Mungu ahubiri habari zake yeye mwenyewe Kwa mujibu wa hiyo hoja Yako dhaifu!?
Je nyinyi wafia dini mnatupa majibu sahihi? Kwendeni zenu😁
 
Mi kwa mtizamo wangu. Huyu Mungu tunaemzungumzia atakuwa kaumba viumbe vingi sana na madunia mengi sana. Sasa kila dunia kaiwekea viumbe vyake tofauti tofauti na kanuni za asili zinazoviongoza hivyo viumbe.
Mfano wanyama kila mnyama unaemuona anaongea na mwenzie wa jamii yke kabisa wanautaratibu wa asili unaoongoza dunia yao. Na vile tunavyoona labda paka hana akili sio kweli wana akili zinazoishia kwenye levo yao. Sisi binadamu pia tunajiona tuna ufahamu sio kweli ni ufahamu unoishia levo yetu. Sasa sisi juu yetu utakuta tena Kuna malaika. wanatuona tunamapungufu na tu wadhaifu na levo yao iko juu kuliko sisi. Na ndio maana unakuta ukisoma Biblia unakuta kuna mahali Mungu anamtuma kunguru ampelekee Eliya chakula. Sasa utajiuliza tangu lin kunguru akatumwa. Ni kwamba Mungu kila kiumbe kakiwekea kinafuata kanuni ile ile ya asili bila kuingiliana japo yeye vinamjua japo kwa kuhisi na vikitumwa vinajua mamlaka ya Mungu na kutii. Ukimsikiliza Yesu anasema amepewa mamlaka juu ya wote wenye mwili yaan ishu ya kwenda Mbinguni kwa wnadam Yesu kaachiwa. Kingine viumbe vyote vya Mungu vinamjua kwa asilimia 00000.01. na tena utamjua tu kwa yeye kukufunulia katika ile levo anayotaka yeye. Tena ukisoma Biblia utagundua badhi ya siri nzito kwamb kuna wenye uhai wanne wamekizunguka kiti kikuu Mbinguni na biblia haijatuambia ni viumbe gan hivyo. So kma alivyosema mleta muda ishu ya Mungu ni kubwa mno kiasi kwamba uwezo wa mwanadam kuelewa ni mdogo sana. Bado hujaweka ule mstar Yesu aliosema nina kwenda kwa Baba kuwaandalia makao. It means kuna madunia kibao bdo unaendelea kujengwa. Hayo ni machache kuhusu ufahamu wangu. Ila kuhusu Mwenyezi Mungu ni kweli yupo. Ni kma vile giza na mwanga au mema na mabaya. So dunia imeumbwa kuwili hasi na chnya so kama unawez kuwaza au kutenda mema basi unaweza kufanya hivyo vibaya pia so huo ubaba wa huo ubaya ni shetan na ubaba wa huo wema ni Mungu. Asanten
Siwezi kumuelezea mtoto wangu hadithi za kipumbavu kama hizi upuuzi mtupu
 
Wewe uko vizuri hapo ulipo au tuje kukufunga kamba.

Haya uliyoyaandika inaweza tuyaongea bila kuyasoma.

Kama huwezi na uko mzima kabisa tuambie umeCnP kutoka kitabu au jarida gn. Nani author.

Kama ni wewe mwenyewe unapaswa kuwa mwandishi wa script ya series kama isidingo.

Nakuuliza hii script ni msaada wa AI. Nauliza hivyo kwa kuwa umeuliza maswali na kujijibu mwenyewe. Ndio maana nahisi wewe makazi yako ni milembe. Kwani si mtu wa kawaida.

Nikuulize na wewe. Je kuna wakati unajiongopa wewe mwenyewe.

Pili je kuna wakati inajihisi umetengana na mwili wako kama ambavyo mimi hunitokea.

Kama ni hivyo basi wewe ni kwa mtu wa unaetumia muda mwingi kujitenga na wengine ukisoma na kutafakari.

msingi wa swali hako ulijibiwa karne ya 18 na Fredrich Nietzsche.

Yeye alijibu imani ya kikristo kuwa Mungu ni yesu.

Akakana uwepo wa Mungu kwa mantiki kuwa kama yesu aliuwawa na baada ya hajaonekana tena; na kwa kuwa dunia imetapataa uovu basi ni hakika Mungu kauwawa.

Na kwa kuwa Mungu kauwawa. Na mambo yote aliyoyaleta ikiwemo dini hayana maana tena. Na ndipo akaintriduce serikali za kisekyula. Na Usekyula unaanza rasmi.

Kwa ufupi kama wewe inakubali mfumo wa Usekyula, kwa maana serikali au taifa lisilo na dini. Sio tu halina dini, bali ni kwamba unaamini Mungu hayupo, Mungu kauwawa. Sasa kwenda zako kanisani hakuna maana yyt zaidi ya kuweka kundi la watu wako contaminated na kuchanganyq mambo. Kwa jicho la mtu wa tatu anakuona uliyechanganyokiwa.

Hata hivyo binafsi msingi mkono Usekyula haya hivyo simuumgi mkono Fredrich.

Kwa ufahamu nilionao kwa kuongozwa na Quran maana ya Mungu ni Shetani.

Halafu kuna Mungu mwenye Enzi. Au Mwenyezi Mungu. Si akili bali ni uwezo wenye kuweza uliowezwa. Kwa ufupi ndio mnaita universe.

Halafu kuna universal law kwa maana guide au manual aliyoitoa mwenye Enzi Mungu kwa kile alichokiumba. Kama vile Microsoft walitengeza kompyuta na kuweka manual. Ndivyo Eloi alivyotengeza wanadamu na kuwapa universal law. Kwasasa ni Quran.

Kwanini kuna machafuko, na uhai una maana gn kwa mwanadamu.

Jibu no hili machafuko hutokea kwa sababu ya kuacha kutumia manual ya mwombaji. Inaanzia wapi.

Kwa mujibu wa Quran wanadami wote kuzaliwa wakiwa ni waislam lkn wazazi wao huwabadili na kuwa waabudu masanabu au waabudu moto. Jiulize kwanini unabatizwa. Ni kwasababu unabadilishwa kutoka kuwa muislam na kuwa kuabudu sanamu.

kuacha kutumia manual Eloi kasema ndani ya Quran 2:190-193 kuwa kinaleta mateso na mauwaji (percecution) au fitna.

Na kwanza ni haki ya kwanza kwa mwanadamu aww tayari kupoteza maisha kuliko kuiacha fitna itawale.

Karibu ndugu kutengeza hii script kama ya isidingo
Upeo wako unazunguka eneo unalo ishi tu. ndio maana umendika kwa kudhani dunia nzima imani ni mbili tu uislam na ukristo. Vipi kuhusu wa hindu nao wanabatizwa? Vipi Buddha shinto tao hizo zote ni dini nao wana batizwa?
 
Upeo wako unazunguka eneo unalo ishi tu. ndio maana umendika kwa kudhani dunia nzima imani ni mbili tu uislam na ukristo. Vipi kuhusu wa hindu nao wanabatizwa? Vipi Buddha shinto tao hizo zote ni dini nao wana batizwa?
Nao kuondolewa dini yao ya asili kwa kufanyiwa Dharma.

Ni sawa na ubatizo kwa wakiristo.
 
Kwa nini unadhani kwamba ulimwengu ulifanyika?

Kwa nini hudhani kwamba ulimwengu upo tu wenyewe pasipo kufanyika.

Una thibitisha vipi kwamba ulimwengu ulifanyika?

Eleza ni wakati gani kulikuwa hakuna ulimwengu, Kisha ulimwengu ukafanyika?

Na kabla ulimwengu haujafanyika, Huko ulikokuwa kulifanyika na nini?
Pale tunapoingia kwenye "infinite regress", hali inayozaliwa kwa kuweka assumption ya kwamba kila kitu kina mwanzo flan au kusababishwa na kitu flan kilichokitangulia kitu/jambo hilo.
 
Sayansi ni vivuli vya hekima za mbinguni . Mbinguni ndiko anakoishi Mungu . Dini huwa inajishughulisha kuwaambia watu mbingu ilivyo na kuwahimiza watu watende matendo mema ili wakifa waende mbinguni . Mungu anaishi mbinguni ila huwa anajidhihirisha duniani kupitia roho za watu .
Mbinguni ni wapi?
 
Uwepo huo wa hali ya juu wenye ufahamu ndio huo ulimwengu wenyewe.

Kuita uwepo huo mara sijui nguvu/ Akili/ Mungu ni kupachika pachika tu majina uchwara.

Uwepo huo wenye ufahamu wa hali ya juu ndio ulimwengu.
Nkipitia hoja zako au majibu yako, Naona kabisa ambavyo thinking capacity yako ipo chini mnoooo
 
Back
Top Bottom