Mungu mkubwa,hatimaye wameanza kutandanza mataaluma ya reli ya Standard gauge


Watu wa business as usual utawajua tu. Mipango inayoishia kwenye makaratasi tumechoka nayo. Miaka nenda miaka rudi, mipango mipango mipango. Sisi hatuna haja na planning. Bora kusiwepo na makaratasi lkn tukaona vitu.

Bravo JPM you are the best. No one can beat you.
 
Hapo ndio anatuchanganya kabisa. Lakini sisi bahati mbaya tunapiga makofi tuu.

Usichanganyikiwe JPM is doing the best. Anavyosema hivyo anawafanya wakopeshaji KUTOKUWA na mtazamo wa KWAMBA BILA wao mradi hautatekelezwa, hivyo hata mkienda KWENYE majadiliano hawawi wagumu na kandamizi kwenye kikao. MAANA wanajua ya kuwa mna m'badala. Lkn kama mnaenda kuongea na mkopeshaji wakati hamna m'badala. Hata kuongea mnakuwa hamna nguvu. Yule mkopeshaji hawezi kuwaleteeni masharti magumu na ya ajabu ikiwa mna sehemu nyingine ya kukimbilia. Nina uzoefu ndo MAANA nasema hivyo.

Mfano mzuri ni Kenya ambao wamejenga reli yao ya KISASA kwa bei ambayo haifikiriki.
 
Wamiliki wa mabasi ya abiria kwa upande wao hizi siyo habari nzuri kabisa, hii reli inakuja kuua kabisa biashara zao. Sio ajabu tukashuhudia vitendo vya kuhujumiwa kwa hii miundo mbinu siku zijazo itakapokuwa imekamilika.

Wengi wa hawa wamiliki wa mabasi wapo tayari hata kutoa watu kafara ili mradi tu mabasi yao yaingize faida. Kwenye swala la ulinzi Serikali inatakiwa kujipanga sana ili kuilinda reli hii.
 
Ilindwe hiyo kunawatu wanaweza kuja kuing'oa usiku usiku.
Kama wanaweza kushirikiana na wanaotudai ili ndege zisifike nchini ndani ya muda uliopangwa, watashindwa vipi kuhujumu kitu chenye faida kwa Tanzania nzima!!.

Inasikitisha sana kwa mtanzania mmoja kuihujumu nchi yake, kuhujumu mahali anapopaita nyumbani, kuhujumu kitu pekee ambacho ni cha kwake kwa asilimia 100.
 
Kazi kazi tu, hakuna muda wa kulemba kazini.
 
Inasikitisha sana kwa mtanzania mmoja kuihujumu nchi yake, kuhujumu mahali anapopaita nyumbani, kuhujumu kitu pekee ambacho ni cha kwake kwa asilimia 100.
Ndio yale ya Simba na Yanga mmoja akifungwa mwingine anang'oa viti vya uwanja wao.
 
Hakuna kinchoshndana hata tukisema tunaweka flyng over toka dar hadi mwanza au tulete bomba ya mafuta toka uarubuni.shda je ipo kwnye mkakati?athari yake ikoje kwnye uchumi?je nikapao mbele yetu?tunachangamoto mengi ya muhimu kuliko hayo.shule zetu hazina walimu wakutosha na madawati vitabu hosp zetu nayo hvyo tuna t scan moja nch nzima.maji ndyo tusiseme.mambo ni mengi sna.tungeboresha huduma za jamii kwanza
 
Acha unaa
 
JPM is the real deal
Kura yangu 2020.
 
Ndio yale ya Simba na Yanga mmoja akifungwa mwingine anang'oa viti vya uwanja wao.
Akili zetu zina matatizo katika utendaji kazi. Wajapan walifungwa na Belgium lakini mechi ilipomalizika wakasafisha mazingira ya majukwaa, ni watu wanaojielewa, sisi hatujielewi.

Kule Russia tuliona namna ambavyo mashabiki wa nchi mbili tofauti wanavyokaa pamoja kwenye majukwaa, pale uwanja wataifa mashabiki wenye mavazi ya rangi ya njano hawawezi kukatiza kule upande wa mashabiki wa Simba, ni upuuzi uliojificha ndani ya vichwa vyetu.
 
bado tupo nyuma sana .treni za umeme ni teknolojia ya zamani.teknolojia ya sasa hiv ni hyperloop,yaan ni transport system ambayo inafika speed ya 1000km/hr. mzee magu angeleeta hyperloop ningemkubali
teknolojia nyingine ambayo ni mpya ni ya kutumia laser technolgy for air transport hapa tunaweza safiri dunia nzima for just nusu saa tu, na tunaweza travell kwa spid ya 30 percent of the speed of light
mzee magu ukitaka nikupigie salute lete hyperloop, laser technology kwenye industry ya transportation
 
Mkuu unaonekana unapenda sana zile sinema za kisayansi. Upo very scientific, safi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…