Mungu, nakuomba uwaamshe Watanzania kutoka usingizini

Mushkov

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2024
Posts
357
Reaction score
686
Mungu, Watanzania wamepigika na wamechoka kweli kweli. Wakati Watanzania wanahangaika kila siku kutafuta angalau mlo wa siku, Mawaziri, Wabunge na waandamizi wengine wa serikali wanaishi maisha ya ANASA na hawajali hata kidogo shida za Watanzania.

Mungu, nakuomba uwaamshe Watanzania ili kila anayeitwa Mtanzania:
  • Asikubali kudanganywa tena.
  • Asiogope tena kuchukua hatua kali dhidi ya hawa wanyonyaji.
  • Athubutu kusema"sasa basi" bila kuogopa chochote.
Mungu, wape ujasiri wa pekee Watanzania wote ili kwa kauli moja wakaseme "sasa basi"

Utukuzwe Mungu mkuu usiye na upendeleo na usiyeshindwa jambo lolote.

Amina.
 
Kamwe Mungu awezi kuangaika na wapumbavu, elewa kuwa Mungu anasifa za mwerevu.

Ndiyo maana from the first place alitupa akili na maarifa ya kutawala viumbe hai vingine.

Kwa hiyo ndugu usipoteze muda wako na maombi yako kwa mtu asiyejitambua "MTANZANIA".
 
La kwanza kabisa tuache kuamini kuhusu kuwa siasa itakuletea maendeleo na tupambane na kazi zetu.

Tukiwa tunapambana na kazi zetu tutaacha kwenda kupoteza muda kwenye mikutano ya kisiasa, kupokea ndege airport, kujipanga barabarani na jua kali kumshangilia kiongozi fln n.k
 
kuna ile muvi ya tiers of the sun,mmissionary anaomba Mungu aibariki Africa,Bruce Wilis akajibu shombo sana kuhusu Mungu na Africa,,,😁
 
Ni kweli, lakini tusiwakatie tamaa Watanzania mapema hivi. Hawa hawa wanaoonekana hawajitambui, ipo siku utawashangaa na hutaamini kabisa maamuzi magumu watakayokuja kuyachukua dhidi ya haya MAJIZI yasiyojali shida za Watanzania.
Hakuna marefu yasiyo na ncha.
 
Mkuu,

Mungu hayupo, weka mkakati mwingine.

Angekuwepo, usingehitaji hata kuomba, angekupa tu unachohitaji, asingekuwa na roho mbaya hivyo kukunyima unachojitaji mpaka umuombe.

Kuhusi Watanzania na hali ya uchumi.

Nina notice kipimo changu cha kurekodi simu za mizinga kutoka bongo kikiongeza idadi ya simu za vilio kuliko hali ya kawaida.

Hiki kipimo huwa hakikosei kunipa data za haki ya uchumi Tanzania.
 
Tukapokee Ndege baadae Mkuu..
 
Hakuna Mungu wa hivyo. Mungu aliyepo ni yule tu ambaye unamuomba akupe ridhiki wewe. Yule wa kutaka mtu mwingine aharibikiwe ni Shetani tu.

Tanzania haiwezi kuharibikiwa kwa maombi ya mtu ambaye hajishughulishi anataka aletewe tu. Wewe mtoa mada tafuta shughuli ya ki-uchumi na ifanye acha ujinga
 
Tatizo lako hujui uchumi ni nini na unajengwaje.
 
Iweivo LAKINI kama maprofeki wenyewe wanajipapatisha kwa viongozi.... Saitakuwajee!!!
 
Amina. Mungu ni mwaminifu, atatenda lililo jema.
 
Unaongelea watanzania gani? Hawa walionyimwa elimu bora? Hawa wasio na upeo wa kuona yajayo? UNAPOTEZA MUDA
 
Tatizo lako hujui uchumi ni nini na unajengwaje.
Ninajuwa uchumi kwa kusoma, kufanya kazi na kuwekeza nilichochuma.

Toka huko njoo nikuajiri kama wenzio 20 nilionao kwenye shughuli zangu
 
Kuhusu uwepo wa Mungu na ishara ndogo kabisa ya kukuhusu! Ulipo lala ulikuwa mfano wa mtu mfu! Kwa nini umeamka mkuu,

Aliyekuwekea Damu na ndiyo hiyo inakufanya uishi ni nani?

Mbona hiki kipengele kidogo tu kimeshinda nguvu yenu ya Sayansi?

Je, kunakiwanda cha Damu au kitawezekana kuwepo soon?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…