Maana yeye anafahamu kwamba fulani ata uruke ruke vipi utaishia kufa katika uzinzi au ujambazi sasa kwa nini tena iwe anakuandalia adhabu wakati alijua huwezi mtii.
Iweje akulete duniani kuja kuhitimisha safari ya uhai wa watu wengi.
Tunaomba Mungu tujaailie tuwe na safari njema. Ila baada ya km 230 tunaanguka tunatoa sababu shetani kaingilia kati ya safari yetu. Inaleta maswali
Maswali ni mengi kuliko majibu kwakweli.
Soma hii warumi uniambie kama Paulo anamake sense
https://www.bible.com/sw/bible/1818/ROM.10.SRUV
WARUMI 9
10. Wala si hivyo tu, lakini Rebeka naye, akiisha kuchukua mimba kwa mume mmoja, naye ni Isaka, baba yetu, 12. aliambiwa hivi, Mkubwa atamtumikia mdogo 11.(kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, ili lisimame kusudi la Mungu la kuchagua, si kwa sababu ya matendo, bali kwa sababu ya nia yake Mungu),
13.Kama ilivyoandikwa, Nimempenda Yakobo, bali Esau nimemchukia.
14.Tuseme nini basi? Kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha! 15 Maana amwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiaye. 16 Basi, kama ni hivyo, si katika uwezo wa yule atakaye, wala wa yule apigaye mbio; bali wa yule arehemuye, yaani, Mungu.
17 Kwa maana Maandiko yasema juu ya Farao, ya kwamba, Nilikusimamisha kwa kusudi hili, ili nioneshe nguvu zangu kwako, jina langu likatangazwe katika nchi yote. 18 Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.
19. Basi, utaniambia, Mbona angali akilaumu? Kwa maana ni nani ashindanaye na kusudi lake?
20. La! Sivyo, Ee binadamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! Kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Kwa nini umeniumba hivi?
21. Au mfinyanzi je! Hana amri juu ya udongo, kwa fungu moja la udongo kuumba chombo kimoja kiwe cha heshima, na kimoja kiwe hakina heshima?