Mungu sio mwema

Mungu sio mwema

Kiukweli sijakuelewa kabisa na sitaki kuamini kama hueleweki maana umejitahidi kuandika kisomi sana lakini daaah sijaipata hoja yako.
Ana maanisha kwanini huyo Mungu asinge msamehe shetani wakakaa kitako wakayajenge yaishe ili wananzengo tule bata tu kama tupo peponi?
 
Mpangilio wa ustadi wa ulimwengu sio ushahidi kuwa kuna Mungu......sana sana kunaongeza uwezekano wa kutokuwepo kwa Mungu

Hebu fikiria kabla ulimwengu huu haujaumbwa ilikuaje?
Kwamba there’s nothing except God? Mungu alikua wapi? Alianzaje kuumba.... anga tupu?
Alitoa wapi materials ya kuumba ulimwengu wote huu?
Na baada ya kuumba ulimwengu huu ni nini wajibu wake?

Hakuna anayejua kuhusu ulimwengu ulifanyikaje
Utazaliwa utazaa utakufa..... hadithi yako itaishia hapo hii ni kwa viumbe wote

Wewe unapinga maandiko ya wenzako waamini Mungu(Bibilia/Quran) lakini na wewe unamuumba Mungu wako kwa fikra zako
Aisee.. Mimi ninajaji mambo kama yalivyo na Sio kama walivyo.

Haijalishi alitokea wapi lakini hii dunia kuna Something behind mpaka uwepo wake so Thats my God. He created me
 
najiuliza ukienda dukani ukanunua shati je ni kipi kati ya wewe na shati kinamuhitaji mwenzake....

kuna jamaa fb niliona clip yake kweli nikajiuliza nikacheka sana kama mungu kamuumba mwanadamu nani mwenye shida na mwenzake maana mwanadamu hakuamuomba mungu amuumbe bali ni mungu mwenyewe aliamua kumuumba mwanadamu...

nasikitika nikisikia eti mungu alituumba tumuabudu wakati yuko na malaika wazuri wenye kujua kusifu na kuabudu.
mwisho najiuliza afrika kusingekua na mali za kuchota wangetuletea dini kweli ili tuanze kumjua huyo mungu mwenye pande mbili mara wavaa suti mara wengine wavaa kanzu
 
Aisee.. Mimi ninajaji mambo kama yalivyo na Sio kama walivyo.

Haijalishi alitokea wapi lakini hii dunia kuna Something behind mpaka uwepo wake so Thats my God. He created me
Mkuu huyo Sir God unaye amini ameumba ulimwengu unadhani ana interfere maisha yetu au ameacha yanakwenda logically?
 
Mungu gani mwema anaacha maelfu ya watoto wasio na hatia yeyote ile wanakufa na kuteseka kwa njaa, vita, magonjwa na majanga ya asili?

Kama huyo Mungu yupo ni Mungu Muovu, Mbaya na Mkatili sana na hana hata chembe ya wema.View attachment 3040600
Shetani atakuponda kisigino na wewe utamponda kichwa ....ndiyo sababu
 
Mkuu huyo Sir God unaye amini ameumba ulimwengu unadhani ana interfere maisha yetu au ameacha yanakwenda

Alitupa akili na utashi wa kufanya Tutachofikiri ni sahihi kufanya..

Kwahiyo hakuna kanuni yeyote,
Kila mtu anaishi The way akili yake inafikiri ni sahihi..

Ukimuamini atakupa Nguvu sababu ananguvu Ukizingatia uumbaji wake.

Usipomuamini hana shida na maisha yako ishi utakavyo .

Thats what i think..
 
Hakuna maandiko yanasema Mungu kasema tumchukie shetani! Mbona shetani saa nyingine huwa anaenda kuomba kibali kwa Mungu kwa ajili ya kumpa majaribu mwanadamu!.
Na Mungu anakubali kumpa shetani hicho kibali?
 
Binadamu acheni uoga, mlio jazwa huko Sunday school, madrasa
Juzi tumesikia hapa MTU akisema ( MTU anaye mwamini Mungu hawezi kumtukana kiongozi)

Dini iliwekwa ili kuwatawala binadamu, ndio Hata baada ya kupata Uhuru , still Dini ziliachwa ziendelee Ku operate bila pingamizi,

Wakati Dini zote zilikuwa chachu ya ukoloni Kwa vipindi tofauti.
 
_Watu wengi inawachanganya sana hii. Mi naamini Mungu ndo mwanzo wa uhai na Kila tunachokiona.

_Lakini dini na simulizi za vitabu tofauti kumuelezea Mungu ni utashi wa watu binafsi.

_Nguvu na uweza wake vinajieleza na kuthibitika vyenyewe kupitia kutafakari Alichofanya.

_ Mfano: Fikiri mfumo wa mwili wako jinsi unavyojiendesha, Fikiria unapopona vidonda, Viungo vyako jinsi vilivyoundwa ndani na nje, Mtu ananenepa na kukonda bila viungo kupishanaa. Fikiria kuhusu nguvu ya Jua, Umuhimu wa mvua, Vyanzo yofauti vya maji, Kubadilika kwa majira ya Mwaka, mpangilio wa Nyota angani.

_ Hata kuelea kwa dunia hewani, Namna mimea inakua na vingine vingi havihitaji sisi kukesha kanisani, kutoa sadaka kujua kua yupo.

_Dini ni na vitabu vya dini ni Uzushi na utapeli.
Of coz, hayo unayoeleza Ni ambayo yanathibitisha kwamba aliumba lkn si kwamba yupo. Swali Mara nyingi lilitakiwa liwe Ni vipi uthibitishe kwamba yupo?

Hapa ndipo wengi tunamkosa Mungu na kuanza kuwa wapingaji. Ni uhayawani tu unatusumbua, maana hatujui gharama ya uhai huu Ni kiasi gani. Pia hatuelewi utaratibu na miiko ya kitu kinachoitwa uhai.

Mara nyingi tunawaza kwamba ile miiko ya uhai ndiyo itupeleke kwenye uthibitisho wa uwepo wake, Jambo ambalo haliwezekani.

Na kumbe njia pekee yakutupeleka kwenye uthibitisho ule ndio hii hii inayotuvuta kwenye ukosoaji.

Jambo la msingi hapa Ni kumuamini yeye Mungu. Lkn wale ambao hawamuamini inabidi tumuachie mwenye watu wake maana atakuwa anawajua vizuri kuliko sisi.
 
Hasa huyu wa Waisraeli, aliyemtoa mwanae kafara bila huruma, akashindwa kumuangamiza shetani.
 
Nina hoja ningependekeza kuileta mbele yenu wanajamvi..

Kama kichwa na habari kinavyojieleza "Mungu sio mwema"
Je ni kwanini ninasema haya.

Zingatia hili, katika mafundisho yote ya kiimani tunafundishwa kumchukia shetani na mabaya yake yote ili tumpokee kristu, ni kweli Jamaa ni muovu, wewe sasa!! maana yupo ndani yako...hii chuki tunayoieneza dhidi ya shetani inatutengenezea nini sisi kama wanakondoo?!

Ukiangalia Kwa ndani zaidi chuki dhidi ya shetani, inaleta nini zaidi ya visasi, malalamiko na kukata tamaa ?! Sasa je, sisi kama wanadamu tunanufaika vipi na hii chuki tunayoieneza dhidi ya shetani, zaidi ya kutuumiza kihisia na kufifisha silka ya kupambania uhai.

Au Kuna faida ambayo mimi siioni?
Haya sasa tuangalie matendo yaliyopo kwenye wema wa Mungu, submission, compassion, respect and unity.....haya matendo tuliyatoa Kwa Mungu au Kwa kondoo?!

Je haya matendo mema yana faida gani kwetu?! Mbona ni kama hatutaki kutumia macho na kukaa hapa Duniani. Na pia ukienda mbali zaidi utaona ni Kwa namna gani yanaendelea kudidimiza silka ya kupambania uhai, hakuna zawadi nyingine inayotolewa na haya matendo ya kondoo zaidi ya utukufu(udhaifu).

Tukimuona shetani mbaya tunaumia na wema wa Mungu unatupa udhaifu, matokeo yake tunaishia kuwa sick and perishing, ndio maana Kila mkristu na muislamu unayekutana nae barabarani anaumwa either Kwa kufikiria au Kwa mawazo, na moyo pia unaumia.

Je Kuna haja gani ya kuendelea na hii kelele ya mema na mabaya kama Kila upande unaharibu, Kuna haja?!!!!!!!
Yesu alikuwa mchunga kondoo,
Next time try to be there- budha teachings, terrestrial head, beyond good or evil
tumaini la waisrael kwa Yesu alipokuja kuwakomboa walidhani anawatoa kwenye utumwa wa warumi
lakini yeye alisisitiza kuwa malengo yake ni ya juu ya zaidi ya hapo , ni kukomboa ulimwengu wote from anguko lake na kuwatupeleka mbinguni na siyo kufanya ulimwengu huu kuwa bora
 
Back
Top Bottom