Baba wa mbinguni, Tunakuja mbele zako kwa unyenyekevu na shukrani, tukikuomba umlinde mtumishi wako Daktari Nchimbi.
Mfunike kwa damu ya Yesu Kristo, na umzungushe kwa ulinzi wako mchana na usiku.
Bwana, mlinde na mabaya yote, ajali, magonjwa, hila za adui na kila hatari ionekanayo na isiyoonekana.
Mpe afya njema, nguvu za mwili na amani ya moyo.
Mpe hekima katika kazi yake, baraka katika mikono yake, na neema katika kila hatua anayoichukua.
Ee Mungu, malaika wako wakae pamoja naye kila mahali aendapo.
Kila silaha itakayoinuliwa dhidi yake na isifanikiwe,
na kila neno baya lililonenwa dhidi yake lirudishwe bure kwa jina la Yesu.
Tunakuachia maisha yake, familia yake, na kazi yake mikononi mwako,
kwa maana wewe ndiwe mlinzi wetu wa kweli, sasa na milele.
Amina.