Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Mungu wa kweli hahitaji haya tunayoaminishwa

Kuna mtu alichukua muda wake na kukufundisha kama Mungu yupo na ukapata akili ya kupambanua hili baya na hili zuri, je angekuwa kama wewe hivyo ungejua nini kuhusu Mungu? Jina lako nalo linachangia hayo uongeayo

Kwani wale swala kule serengeti au na tembo wa pale mikumi wamefundishwa na nani kuwapenda jirani yao ..!?
 
Wamekukosea nini watumishi wa mungu mbona unaonekana kama una chuki nao.


Sina chuki na mtu Mkuu. Naongozwa na kanuni ya upendo. Ila ninachosisitiza hapa ni kuwa wachungaji wengi kama sio wote wamejimilikisha Mungu na kujifanya wao ndio kila kitu na huweza kulaani au kubariki wakati ni uongo wa mchana
 
Naona unataja tu "Mungu wa kweli Mungu wa kweli" hebu tuelekeze na sie jinsi na ya kuwasiliana nae ili tujirizishe haya uliyosema isije ikawa na wewe unafanya kilekile unachopinga kuhusu wafanyavyo hao viongozi wa dini.

Mungu wa kweli hakuna atakayekuelekeza kwakwe. Mungu wa kweli yupo moyoni mwako.Huyo ambaye ukifanya jambo baya unajisikia vibaya msikilize huyo huyo. Tumia akili kwani Mungu ndio hutumia akili yako kujidhihirisha katika maisha yako na si akili ya mtu mwingine. Ikitokea hatari kubwa itakatayo kuhusu wewe peke yako ndipo utamjua Mungu wa kweli.
 
Dini zina kila sababu ya kutimiza matakwa ya wanadamu

Hewezi kushindwa kujua kuwa ni kazi za njemba fulani wachache yenye matokeo chanya
 
Kwa Muktadha wa "maandiko matakatifu" nyoka mkubwa au (Joka) maana yake ni "shetani", na shetani maana yake mtu au kitu kiovu, kibaya nk.


Muktadha wa maandiko. Njoo sasa na yule aliyeangikwa kwenye mti na Musa kule jangwani aliashiria Shetani. Embu mwaga nondo hapa tujifunze alafu nami nimwage vyombo
 
Unadhani misikiti na makanisa yataendeshwa vipi tusipotoa zaka na sadaka?
masheikh na mapadre watakula wapi?


Mimi sijakataa wao wasipewe sadaka Mkuu. Ninachokataa ni wao kusema Mungu ndiye anataka sadaka tena wameenda mbali zaidi kwa kusema fungu la kum(9zaka) ni la Mungu jambo ambalo si kweli. Tunajua umuhimu wa huduma yao lakini isiwe sababu ya wao kumsingizia Mungu eti anahitaji zaka. Tena ni lazima.
 
Wewe tangulia kuzimu kwa Mungu wako Ibilisi


Ibilisi hajawahi kuwa Mungu Mkuu. Tabia ya watu kujiinua na kujipa madaraka wasiyonayo ndio tabia za kishetani. Mwanadamu ni mwanadamu bila kujali kazi afanyayo hivyo kila mmoja amheshimu mwenzake kwani hakuna aliyebora ya mwenzake
 
Huyo mungu anahitaji hayo mambo kwa sababu hayupo!Mungu tunaeaminishwa kuwa ana upendo wote,huruma yote na ni mweza wa yote angekuwepo asingehitaji huo uchafu!Kuhadhitiana kuwa mungu anahitaji vitu hivyo ambavyo ni non-sense ni uthibitisho kuwa mungu huyo hayupo!!


Mungu yupo Mkuu. Ila wajanja ndio wanamfanya asiwepo kwa kumshushia heshima na kumfanya aonekane Mungu mwenye shida, Mungu asiye na huruma ilhali anahuruma.
 
Kuna mtu alichukua muda wake na kukufundisha kama Mungu yupo na ukapata akili ya kupambanua hili baya na hili zuri, je angekuwa kama wewe hivyo ungejua nini kuhusu Mungu? Jina lako nalo linachangia hayo uongeayo


Ni jukumu lake kunifundisha hayo lakini si jukumu lake kumsingizia Mungu kama anashida ya zaka na sadaka wakati sio kweli. By way maisha ni kutegemeana kwa kusudi la Mungu. Kila mtu ni kusudi la Mungu na kwa Mungu hakuna kusudi kubwa na dogo
 
Basi viongozi wapunguze michango. Kuna mchango wa ujenzi, kila Jumapili upo,lakini hakuna ujenzi unao endelea. Fungu la kumi kila wiki bahasha lazima ijazwe hela, siku ya kilele bado unaambiwa utoe fungu la kumi maana huko nyuma ulikuwa unatoa kwa kujibana bana. Na vitisho vya vifungu juu .... aaaghh!!!


Michango iendelee kuwepo lakini kelele zangu ni wao kumsingizia Mungu kuwa atawalaani endapo hutatoa sadaka. Uliona wapi Mungu akifanya hayo
 
Wafanye kazi nyingine ya kuwaingizia kipato.
Tena paulo katika moja ya nyaraka zake anajitapa jinsi alivyokuwa si tegemezi kwa ndugu wa miji aliyoitembelea

alikuwa anajikimu kwa kujichanya na wenyeji na mambo ya kanisa yanaendea kivyake

Nikikumbuka mistari nitaiweka hapa_hawana sababu yakuwa wezi
 
Back
Top Bottom