Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mimi sijakataa wao wasipewe sadaka Mkuu. Ninachokataa ni wao kusema Mungu ndiye anataka sadaka tena wameenda mbali zaidi kwa kusema fungu la kum(9zaka) ni la Mungu jambo ambalo si kweli. Tunajua umuhimu wa huduma yao lakini isiwe sababu ya wao kumsingizia Mungu eti anahitaji zaka. Tena ni lazima.
Yameandwika wapi hayo?Habari wakuu!
Mungu wa kweli, mwenye uweza wote, na aliyeumba kila kitu hahitaji mambo yafuatayo:-
1. Hahitaji Zaka wala Sadaka
Mungu wa kweli si mhitaji, uhitaji ni karba ya viumbe. Mungu hana anachohitaji kutoka kwa kiumbe. Yeye ndiye huamua nini kiwe na nini kisiwe. Mungu wa kweli hahitaji sadaka kama watu wengi wanavyoaminishwa. Hahitaji zaka kama wachungaji wanavyosema. Wachungaji wanamsingizia Mungu mambo mengi ikiwemo hili la zaka na sadaka. Wanachoshindwa kusema ni kuwa wao ndio wanahitaji hizo zaka na sadaka kama sehemu ya huduma yao. Ni uongo na dhambi kubwa kusema Mungu anataka sadaka na zaka jambo ambalo linamdhalilisha Mungu muweza wa yote.
Wachungaji, mashehe na viongozi wote wa dini kwa majina yao. Muache kuhadaa watu na kumdhalilisha Mungu. Tutatoa sadaka na zaka kwa kujua kuwa mnatupa huduma za kiroho na si kusema kuwa Mungu anahitaji sadaka na zaka tena fungu la kumi. Kama tunawalipa waalimu, madaktari, wanasheria na kada zingine iweje tusiwalipe nyie. Kwa nini mumsingizie Mungu mambo ya uongo. Eti fungu la kumi ni la Mungu. Si kweli. Mtu atatoa zaka na sadaka kulingana na umuhimu wa huduma anayoipata na si kumtishia vitisho vya uongo.
2. Kafara si ondoleo la dhambi
Watu wameaminishwa kuwa eti ili mtu asamehewe dhambi basi sharti amwage damu. Zamani walimwaga damu ya wanyama lakini sasa hivi wanaamini kuwa Yesu(mtu ninayemheshimu sana) alikufa kwa ajili ya watu jambo ambalo ni uongo. Mungu wa kweli hawezi kufikiri achilia mbali kutenda jambo kama hilo. Hiyo ni mila za kuabudu miungu ya Kiyahudi ambayo msingi wake mkuu umetokana na Abrahamu aliyechukua baadhi ya mila za Kiashuru( kwa sasa ni Syria). Miungu ya Abrahamu ndiyo ilimtaka amtoe Isaka kafara kama ilivyodesturi.
Mungu wa kweli hahitaji mchakato huo kusamehe dhambi, na kumwaga damu si suluhu ya dhambi kuishi. Kwa kutambua hili jambo hili moja kwa moja linaonekana ni wazo la kibinadamu zaidi kuliko la Mungu.
3. Maombi hayabadili chochote kwa Mungu mwenye uweza.
Wachungaji, mashehe na viongozi wa dini wengine kwa majina yao wanawadanganya watu kuwa ukimuomba Mungu jambo lolote anaweza akakupa kitu ambacho si kweli hata kidogo. Vile Mungu alivyopanga kabla hajakuumba ndivyo itakavyokuwa. Kusema kuwa ukimuomba Mungu anabadili mipango yake ni kujidanganya na kupoteza muda. Kumuomba Mungu ni kumfundisha namna ya kufanya mambo yake. Hakuna ushahidi wa moja kwa moja unaoonyesha kuwa mtu akiomba jambo kwa Mungu hupewa isipokuwa ushahidi uliowazi ni kuwa Mtu akifuata maagizo ya Mungu na sheria zake ndio hupata akitakacho. Mungu anataka watu wafuate sheria zake na si kuomba omba tuu.
Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini jukumu lao ni kuwafundisha watu sheria za Mungu na si kuwadanganya waombe au kuwaombea. Kuwaombea watu ni kuwafundisha uvivu. Na kuamini katika hamna.
Ukitaka uamini nikisemacho, kaa ndani omba alafu usiende kufanya kazi uone kama Mungu atakupa ukitakacho, alafu mwenzako asiombe aende kufanya kazi uone nani atapewa/atapata. Hakuna sheria ya Mungu mahali popote kwenye torati inayomtaka mtu aombe. Tafsiri yake nadhani mnaelewa ni nini. Usishangae kwa nini bara la Afrika ni masikini ilhali ndilo linaloongoza kwa waumini wenye kuomba makanisani na misikitini. Jibu unalo.
4. Wachungaji/mashehe na viongozi wa dini si watu pekee wanaotakiwa kuheshimiwa.
Kuna dhana watu huaminishwa kuwa kundi fulani la watu ndilo linalotakiwa kupewa heshima kuliko kundi jingine. Huu ni uongo mkubwa. Mchungaji ni mtumishi kama walivyo watumishi wengine. Anahudumia watu kama wanavyohudumia wengine. Hana uspesho wowote zaidi ya wao kuwahadaa watu wenye akili ndogo na wasioujua ukweli ndio maana wamegeuka watumwa wa makuhani na mashehe. Kila mtu duniani anahitaji heshima ikiwa anafanya kazi ya kuhudumia wengine. Iwe ni fundi nguo, fundi magari, mbunge, mwalimu, muuguzi, mhandisi wote wapo sawa na wote wanategemeana. Kumpa mtu fulani heshima kuliko mwingine si tu kwamba ni ukosefu wa maarifa bali ni kuonyesha hali ya kutoujua ukweli.'
Viongozi wa dini wamejipa hadhi kubwa na kujiona wao ndio wenye mamlaka. Usishangae kiongozi wa dini mjinga akisema kuwa anakulaani kwa Mungu. Nikisiaga hivi huwa nacheka sana. Mtu hupata laana kwa kuacha sheria za Mungu na si maneno ya Mchungaji au mzazi. Kwa ujumla ni kuwa mtu hujilaani yeye mwenyewe ikiwa ataacha sheria za Mungu.
Hivyo watu wamejikuta wakiwaogopa wanadamu wenzao kwa kutoujua ukweli. Unamuogopa mtu aliyezaliwa na mwanamke? Mtu anayehitaji chakula ili apate nguvu ya kuishi. Unakuta mtu anaenda kanisani anaitwa na mchungaji mbele ya kanisa na kutabiriwa vitu vya uongo na yeye anasema kweli wakati sio kweli. Kwa mfano;
Mchungaji: wewe unatatizo la ugumba
muumini: Kweli
Mchungaji: Mama yako anakuloga
Muumini: Kweli
wakati yote ni uongo, anasema kweli kwa uoga na utumwa wa kifikra.
Wito wangu, lazima watu waishi kwa kupendana na kuzishika amri na sheria za Mungu ili wapate kuwa huru na maisha. Vinginevyo tutabaki kuwa watumwa na kuona sisi ni wasindikizaji wakati wengine ndio walioumbiwa huu ulimwengu jambo ambalo si kweli
Haswaa mkuu_hawa jamaa wanajaza sana watu hofu mpaka wanakuwa mazezetaNi kama vile elimu, siasa na michezo.
Joka ni kiumbe wa Mungu kama ulivyo wewe, mbuzi, paka na ngedere. Acha kukariri maisha Mkuu. Kila kiumbe kimheshimu kiumbe mwenzake
Haloooo,!!!, Nyoka mweusi, vipi??, unashindwaje kuelewa hekima ya zaka??, unapotoa sadaka na ikatumika katika njia ya Mungu kwa namna yoyote, mfano kumlipa mshahara kiongozi wa dini au kumpatia mwenye shida hiyo ni sawa na kumpa sadaka Mungu, kwa maneno mengine hao watu ndio njia ya Mungu kupokea sadaka.
Au wewe ulitaka umuone Mungu mwenyewe "physically" na umpatie mkononi??!!, hilo halitawezekana.
Kama ni hivyo kila kiumbe kimuheshimu mwenzake, kwanini wewe unachinja (unaua), kuku, bata, mbuzi, samaki, ng'ombe nk halafu unapika nyama zao na unawala "heshima" iko wapi hapo, mbona wao hawakuchinji.
Kwani kabla ya Abraham/ibrahimu na kizazi chake kuwepo watu waliishi vipi..!?Nenda hata kwa wasiojua ukristo au Uislam uniambie wao wanaishije. Amri za Mungu ni amri za asili
Huo ni utaratibu kama ulivyowekwa. Na kumbuka nimetolea mfano. Mkuu nitakupa elimu zaidi maana naona kuna mambo huyaelewi
Na ndio maana tumeamua kuwa vegeterian kwa kuwa mahindi maharage na Matunda yapoKama ni hivyo kila kiumbe kimuheshimu mwenzake, kwanini wewe unachinja (unaua), kuku, bata, mbuzi, samaki, ng'ombe nk halafu unapika nyama zao na unawala "heshima" iko wapi hapo, mbona wao hawakuchinji.
Na ndio maana tumeamua kuwa vegeterian kwa kuwa mahindi maharage na Matunda yapo
vikikosekana sio samaki tu hata simba ni supu nzuri tu
Labda hujaeleweka unakazia niniWewe nawe vipi???!, mbona unachekesha, kwani umeambiwa na nani kwamba Maharage, Mahindi, na matunda au mimea haina UHAI??!,
Huwezi kula mchicha hadi uuchume kutoka shambani kabla hujauchuma unakuwa ni KIUMBE HAI. soma Biology mkuu.
Labda hujaeleweka unakazia nini
kwahivyo hutaki chenye uhai kiguswe..!?
Na wewe soma HESABU 21:6 kisha uniambie kwa nini Mungu amtumie shetani kwenye kazi zake ?Soma , Ufunuo 12:9, 20:2, Mwanzo 3:14.
Wewe una pepo sio bure inaelekea hata kitabu chako cha dini yako husomiMimi nakula kila kifaacho kuliwa mimi sio vegetarian, na wewe nakushauri ule nyama pia achana na vegetarianism.
Mkuu ukweli wa mambo Mungu ana sifa zote ANAANGAMIZA na KUPONYA , hili lazima mlikubali ndio ukweliMungu yupo Mkuu. Ila wajanja ndio wanamfanya asiwepo kwa kumshushia heshima na kumfanya aonekane Mungu mwenye shida, Mungu asiye na huruma ilhali anahuruma.
Wewe una pepo sio bure inaelekea hata kitabu chako cha dini yako husomi
Nanalolifanya mimi hata mungu wako analilidhia kwa kuwa anajua ndio asili ya mwanadamu
Sasa kama umeamua kula vyote kwanini iwe kasoro kitimoto..?Vipi mkuu ManchoG, mbona umegeuka mbogo!!, umesema wewe ni vegetarian kwa sababu unaona "huruma" kutoa roho za wanyama na kula nyama zao kinyume chake huwa unakula maharage, mahindi na matunda, mimi nikakuambia hata hivyo navyo vinao UHAI yakupsa uwe na "huruma" kwao, ukataka kujua kiliwe kitu gani!!, mimi nikakuambia nakula chochote kinachofaa kuliwa kasoro kiti moto. Halafu nikakuusia uachane na "vegetarianism". Sasa mkuu nimekosea wapi hadi useme nina pepo!!??. Likemee basi [emoji16][emoji16][emoji16]