Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwandishi Yuko sawa.ni kwamba umekosa tu ufahamu. Kwa desturi za kiyahudi miaka ile, asingeweza. ila sio kwa desturi ya Mungu.
Matendo 2:17 - 18, na Yoeli 28, utakuta imesema;
Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, nitawamwagia watu wote Roho yangu, na wana wenu na binti zenu watatabiri; na vijana wenu wataona maono; na wazee wenu wataota ndoto. 18 Naam, na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri.
LUKA 2:36 INASEMA: Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. huyu alijitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wanautarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
kwa kifupi, kwa desturi ya middle east, mwanamke hathaminiwi, ila Mungu ana desturi zake. pia, Roho Mtakatifu amekuja kututia kweney kweli yote, ukiwa naye leo atakufunuliwa kama mwanamke anaweza kuwa mchungaji/mhubiri/nabii au la. kama huna utakuwa mshika mafundisho ya sheria tu kama ulivyo na hayatakusaidia hata ukikariri Biblia nzima.
Kuna baadhi ya vitu ni kweli nakubaliana navyo kama hilo la mwanaume kuruhusu mkeo achukue wajibu wako kama kiongozi ni hatari sana itafika wakati familia inaweza palaganyika ingawa si wote, katika wengi hutokea hivyo.... Ila la mwanamke kuwa askofu, nabii au ntume nakubali, ila kuwa mchungaji (kasisi) nakataa maana mchungaji ama kasisi ni mtawala kwa ninavyo fahamu.. maana mchungaji ama kasisi anatachunga kondoo wa Mungu sasa utachungaje bila kuwa mtawala?MUNGU WA WAYAHUDI "YEHOVA" hawezi HATAMBUI MWANAMKE KAMA MCHUNGAJI, NABII AU MTUME. WANAWAKE WANAOJIITA WACHUNGAJI au MANABII WANA mungu MWINGINE
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
YEHOVA kama Mungu wa wayahudi hatambui cheo cha mwanamke kuwa mchungaji, Nabii, au Mtume.
Unapozungumzia Mungu, unazungumzia kitu kinaitwa sheria. Kwa sababu Mungu ni utawala, na hakuna utawala usio na sheria. Sasa unapomtaja Yehova lazima uzingatie sheria zake.
Yehova hamtambui Mwanamke kama Kiongozi. Yehova hamtambui Mwanamke kama mtawala. Zingatia Mchungaji, mtume au nabii ni cheo cha kiuongozi katika masuala ya kiroho.
Mchungaji wa nini? Anachunga kina nani anatumwa ña nani? Ujumbe wake anautoa kwa misingi ipi?
Ingawaje kwenye Biblia wapo wanawake waliotajwa na waandishi kama Manabii lakini ni kwa maoni na hisia tuu za waandishi na wala haiwi maana kuwa kuna manabii au mitume au wachungaji wakike.
Yehova sheria zake zimekaa kiitifaki.
Sio kwamba Yehova kamdharau Mwanamke, hapana bali yeye mwenyewe anasababu zake ambazo sisi hatuzijui.
Kwa sisi Watibeli pia, Wanawake hawawezi kuwa viongozi au watawala katika masuala ya kiimani(kiroho), kimwili, na kiakili na hata kihisia.
Mwanamke ataongoza na kutawala pale ambapo mwanaume hayupo.
Na Mwanamke atapewa nafasi ya kutawala na kuongoza lakini kwa sharti kuwa nyuma yake yupo au wapo wanaume wanaomuoñgoza.
Kiimani mwanamke hapaswi kuongoza mahali palipo na wanaume au mwanaume. Nazungumzia mwanaume mwenye umri kuanzia miaka ishirini na moja. Ila akiwa nyumbani anaweza kutoa huduma za mafundisho, maombi akiwa na watoto wake. Baba akiwepo ndiye ataongoza mambo yote,
Kuanguka kwa Nyumba au familia kutatokana na udhaifu wa kiongozi(Baba) kwa kushinda kuongoza familia hasa kwènye ishu za msingi ikiwemo suala la kiimani.
Mwanaume lazima aandaliwe kuongoza maisha yake, familia na jamii katika ñyanja zote.
Mwanaume anaweza akawa mahiri wa kutafuta mali lakini kama atashindwa kwenye kipengele cha imani, lazima familia itamsumbua.
Wanaume lazima waelewe kuwa huwezi kuongoza familia kama huna uelewa wowote na mambo ya kiimani.
Na Mwanamke hawezi kukuheshîmu kama hujamtiîsha roho yake yaani imani yake haujaitawala.
Sio ajabu unaweza ukawa na pesa au cheo kikubwa lakini Mkeo akawa anamsikiliza na kumheshimu mchungaji au padri au askofu wake kuliko wewe. Au anamsikiliza mganga wake kukuliko.
Taikon kila mara naeleza kuwa, future ya Utawala na uongozi wa familia upo katika namna ulivyomjenga na kumtawala mkeo na familia yako kiimani.
Na hakuna mchungaji,nabii wala mtume mwanamke. Iwe kwenye familia yako, jamii au taifa.
Mke akiwa mchungaji, au nabii au mtume automatically amejipa nao ujiingiza katika nafasi ya mwanaume. Yaani hapo tunasema kama mkeo ni mchungaji au nabii au mtume basi umeoa mwanaume mwenzio. Na naturally lazima mtaachana tuu.
Hivyo simshangai Christina Shusho kwani hivyo ndivyo ilivyo.
Mwanamke anaweza kuwa Mwalimu lakini sio mchungaji, nabii au mtume.
Mwanamke atakuwa mchungaji, nabii au mtume kama ametumwa na Mungu asiyeitwa Yehova, Allah na yule Mungu wa Tibeli.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kuna baadhi ya vitu ni kweli nakubaliana navyo kama hilo la mwanaume kuruhusu mkeo achukue wajibu wako kama kiongozi ni hatari sana itafika wakati familia inaweza palaganyika ingawa si wote, katika wengi hutokea hivyo.... Ila la mwanamke kuwa askofu, nabii au ntume nakubali, ila kuwa mchungaji (kasisi) nakataa maana mchungaji ama kasisi ni mtawala kwa ninavyo fahamu.. maana mchungaji ama kasisi anatachunga kondoo wa Mungu sasa utachungaje bila kuwa mtawala?
Mfano dhehebu ninalo sali tuna askofu yeye ndo kiongozi mkuu wa Jimbo, kuna viongozi wengine chini hadi inafika kwa makasisi wa parishi au parokia, hivyo viongozi wa juu wanachunga viongozi walio chini yao iwe kwa mujibu wa taratibu na kiroho pia, na viongozi wa parishi wanachunga waumini.... Waumini ni wengi kuliko hata viongozi wa Jimbo, na waumini kiroho ni watoto kwa kasisi au mchungaji wao parishi,, ili umuongoze mtoto lazima uwe na nidhamu kama mzazi, iwe mama au baba... Na ndiyo maana kwa Jimbo nililopo ilisumbua sana kuwaweka wanawake mikono kuwa makasisi isipokuwa walihudumu kama mashemasi,, lakini baadae wakapima wakaona wawe makasisi tu, ila sasa nadhani ndo ipo inajadiliwa kuona kama inafaa....
Kama huafiki leta hoja yako kwa rejea ya maandiko.....
Pia bwana mtibeli acha kiburi, kuna kipindi nilikutag kwenye Uzi wangu ukapita kwa speed ya train ya SGR ambayo inafanyiwa majaribio kuelekea dodoma..... Sio vyema aiseh!
Ooh!! Sawa kaka!Mkuu nitag tenà. Kuna wakati hakuwa busy. Hasa nyakati hizi
Mungu unamseti tu upendavyo kuendana na wakati husika , karibu kanisa la nabii uwoya mku
Ni dini ya kiyahudi haitambui hiyo ila injili ya Yesu Kristo inatambua watu wote ni sawa katika kuhubiri injili
Hakwani Biblai inaposema "na siku zile nitawamwagia watumishi wangu wanaume na wanawake Roho yangu, nao watatabiri", wewe unaelewa nini?
kumbuka kichwa cha habari umesema mwanamke hawezi kuwa mchungaji, na hawezi kutabiri.
na unasema mwanamke hawezi kua nabii, wakati hata Yesu alipozaliwa Ana alikuwa nabii na alitabiri. pia, hao "watumishi wangu" ni wa aina gani? mwanamke hawezi kuwa mtumishi wa Mungu?
That's why sio muweza wa yote.Mungu habadiliki yeye ni yeye yule jana lel na hata milele
OUNASEMA, MUNGU WA ISRAEL HAWEZI NA HATAMBUI MWANAMKE KUWA MCHUNGAJI AU NABII, NA MIMI NAKUWEKEA MANABII WANAWAKE HAPA CHINI, MUNGU HUYO ALIWAFANYA MANABII.
KUTOKA 15:20 Na Miriamu, nabii mke, ndugu yake Haruni, akatwaa tari mkononi mwake; wanawake wakatoka wote wakaenda nyuma yake, wenye matari na kucheza.
WAAMUZI 4:4 Basi Debora, nabii mke, mkewe Lapidothi, ndiye aliyekuwa mwamuzi wa Israeli wakati ule.
2WAFALME 22:14 Basi Hilkia kuhani, na Ahikamu, na Akbori, na Shafani, na Asaya, wakamwendea Hulda, nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tikva, mwana wa Harhasi, mtunza mavazi ya mfalme; (naye alikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili😉 wakasema naye.
2NYAKATI 34:22 Basi Hilkia, na hao waliotumwa na mfalme, wakamwendea Hulda nabii mke, mkewe Shalumu, mwana wa Tohathi, mwana wa Hasra, mtunza mavazi; (naye alikuwa akikaa Yerusalemu katika mtaa wa pili); wakasema naye kama hayo
ISAYA 8:3 Nami nikamwendea huyo nabii mke, naye akapata mimba, akazaa mtoto mwanamume. Kisha BWANA akaniambia, Mwite jina lake Maher-shalal-hash-bazi.
LUKA 2:36 – 38 Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. 37Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. 38Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake.
MATENDO 21:8 – 12 Asubuhi yake tukaondoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa Injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake. 9 Mtu huyu alikuwa na binti wanne, mabikira, waliokuwa wakitabiri. 10 Basi tulipokuwa tukikaa huko siku nyingi, nabii mmoja jina lake Agabo akashuka kutoka Uyahudi. 11Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paulo, akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemu watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa Mataifa.
Kutoka 15:20MUNGU WA WAYAHUDI "YEHOVA" hawezi HATAMBUI MWANAMKE KAMA MCHUNGAJI, NABII AU MTUME. WANAWAKE WANAOJIITA WACHUNGAJI au MANABII WANA mungu MWINGINE
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
YEHOVA kama Mungu wa wayahudi hatambui cheo cha mwanamke kuwa mchungaji, Nabii, au Mtume.
Unapozungumzia Mungu, unazungumzia kitu kinaitwa sheria. Kwa sababu Mungu ni utawala, na hakuna utawala usio na sheria. Sasa unapomtaja Yehova lazima uzingatie sheria zake.
Yehova hamtambui Mwanamke kama Kiongozi. Yehova hamtambui Mwanamke kama mtawala. Zingatia Mchungaji, mtume au nabii ni cheo cha kiuongozi katika masuala ya kiroho.
Mchungaji wa nini? Anachunga kina nani anatumwa ña nani? Ujumbe wake anautoa kwa misingi ipi?
Ingawaje kwenye Biblia wapo wanawake waliotajwa na waandishi kama Manabii lakini ni kwa maoni na hisia tuu za waandishi na wala haiwi maana kuwa kuna manabii au mitume au wachungaji wakike.
Yehova sheria zake zimekaa kiitifaki.
Sio kwamba Yehova kamdharau Mwanamke, hapana bali yeye mwenyewe anasababu zake ambazo sisi hatuzijui.
Kwa sisi Watibeli pia, Wanawake hawawezi kuwa viongozi au watawala katika masuala ya kiimani(kiroho), kimwili, na kiakili na hata kihisia.
Mwanamke ataongoza na kutawala pale ambapo mwanaume hayupo.
Na Mwanamke atapewa nafasi ya kutawala na kuongoza lakini kwa sharti kuwa nyuma yake yupo au wapo wanaume wanaomuoñgoza.
Kiimani mwanamke hapaswi kuongoza mahali palipo na wanaume au mwanaume. Nazungumzia mwanaume mwenye umri kuanzia miaka ishirini na moja. Ila akiwa nyumbani anaweza kutoa huduma za mafundisho, maombi akiwa na watoto wake. Baba akiwepo ndiye ataongoza mambo yote,
Kuanguka kwa Nyumba au familia kutatokana na udhaifu wa kiongozi(Baba) kwa kushinda kuongoza familia hasa kwènye ishu za msingi ikiwemo suala la kiimani.
Mwanaume lazima aandaliwe kuongoza maisha yake, familia na jamii katika ñyanja zote.
Mwanaume anaweza akawa mahiri wa kutafuta mali lakini kama atashindwa kwenye kipengele cha imani, lazima familia itamsumbua.
Wanaume lazima waelewe kuwa huwezi kuongoza familia kama huna uelewa wowote na mambo ya kiimani.
Na Mwanamke hawezi kukuheshîmu kama hujamtiîsha roho yake yaani imani yake haujaitawala.
Sio ajabu unaweza ukawa na pesa au cheo kikubwa lakini Mkeo akawa anamsikiliza na kumheshimu mchungaji au padri au askofu wake kuliko wewe. Au anamsikiliza mganga wake kukuliko.
Taikon kila mara naeleza kuwa, future ya Utawala na uongozi wa familia upo katika namna ulivyomjenga na kumtawala mkeo na familia yako kiimani.
Na hakuna mchungaji,nabii wala mtume mwanamke. Iwe kwenye familia yako, jamii au taifa.
Mke akiwa mchungaji, au nabii au mtume automatically amejipa nao ujiingiza katika nafasi ya mwanaume. Yaani hapo tunasema kama mkeo ni mchungaji au nabii au mtume basi umeoa mwanaume mwenzio. Na naturally lazima mtaachana tuu.
Hivyo simshangai Christina Shusho kwani hivyo ndivyo ilivyo.
Mwanamke anaweza kuwa Mwalimu lakini sio mchungaji, nabii au mtume.
Mwanamke atakuwa mchungaji, nabii au mtume kama ametumwa na Mungu asiyeitwa Yehova, Allah na yule Mungu wa Tibeli.
Acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Kama unayo maana tofauti na ile iliyoandikwa kwenye Biblia basi bandiko lako halikupaswa kumtaja Mungu YEHOVA.Unajua maana ya Nabii? Nazungumzia maana ya msingi.
Desturi zipi na za jamii ipi ambazo zamani Mwanamke alithaminiwa?
Mûngu ni sheria. Unaposema mtu asiwe mshika sheria unamaanisha Mtu asimshike Mungu?
Embu eleza ni kwa namna ipi umuabudu Mungu pasipo kushika sheria?
Mûngu ni mtawala, na kwenye utawala kuna sheria. Utatengaje sheria na utawala? Au mambo ya utawala huyaelewi?
Maana ya kwenye biblia ndio hiyohiyo niliyoitoa mimiKama unayo maana tofauti na ile iliyoandikwa kwenye Biblia basi bandiko lako halikupaswa kumtaja Mungu YEHOVA.
Vv
Tofautisha karama ya unabii na nabii.
Unaongelea karama za unabii.
Nabii mkuu huja mmoja kwa wakati,ila karama zipo nyingi.
Mwanamke anaweza akawa anaota ama akaona ono lakini hawezi kwenda uweponi mwa Mungu kama nabii mkuu akapokea neno la Mungu
O
soma na kwingine, wote waliompoke wamekuwa wana wa Mungu. Nyie watu wa nuru ya jioni na wasabato mnaleta mafundisho yenu humu kana kwamba nyie ni watakatifu sana. Acheni kubagua wanawake katika kumtumikia MunguIo unayoisema wewe sio injili ya Bwana Yesu.io ya mwanamke kuhubiri ni nyingine ya ibilisi
1 Timotheo 2:11-12
[11]Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
Let the woman learn in silence with all subjection.
[12]Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe katika utulivu.
But I suffer not a woman to teach, nor to usurp authority over the man, but to be in sile
nce.
mimi naongelea manabii, siongelei huyo nabii wenu mkuu sijui katoka kwa shetani au kwa nani anajua mwenyewe. Miriam alikuwa nabii, ndivyo Biblia iansema, Debora alikuwa nabii. Ana alikuw anabii. na wengine hao nimeweka hapo. naweza kukubaliana na wewe kwenye watoto wa Filipo waliokuwa wanatabiri. ila siwezi kukubaliana na wengine ambao Biblia kabisa imewataja kama manabii. hawakuwa na karama ya unabii, walikuwa manabii. na ni wanawake. hiyo kujifanya nabii anakujaga mmoja tu ni mambo yako, weka mistari ya Biblia kuthibitisha hilo. ya kwangu hii hapa.Tofautisha karama ya unabii na nabii.
Unaongelea karama za unabii.
Nabii mkuu huja mmoja kwa wakati,ila karama zipo nyingi.
Mwanamke anaweza akawa anaota ama akaona ono lakini hawezi kwenda uweponi mwa Mungu kama nabii mkuu akapokea neno la Mungu
O
Biblia inasema hao walikuwa manabii, ila wewe unasema hao walikuwa na karama ya unabii. hebu soma hapa.Tofautisha unabii na karama ya unabii. Ni vitu tofauti
Ha
kwahiyo hauamini kama hao walikuwa manabii wanawake, wakati pameandikwa walikuwa manabii? soma tena.Mkuu hayo maelezo na hizo Aya ànayesimulia ni mwandishi.
Ni kama vile wale wanaosema Yesu ni Mungu kwa Mujibu wa waandishi lakini kiuhalisia jambo hilo halipo hivyo.
Nimekuambia Nabii ni mtu ambaye ni mjumbe au kijumbe cha Mungu. Ingefaa ûweke Aya ambayo kuna kuna mwanamke ambaye aliwahi kuwa kijumbe au mjumbe wa Mungu.
Kwenye andiko langu nimeelèza kuwa kwenye biblia wapo waandishi kwa maoni yao waliwahi kuwaita baadhi ya wanawake kuwa ni manabii lakini kiuhalisia sio kweli,
Ni kama ilivyo baadhi ya waandishi kwa maoni na hisia zao kumchukulia Yesu kama Mungu alafu Watu wasio na uelewa wakasema Yesu ni Mungu ndicho ambacho wewe na uelewa wako unakifanya