Mungu Yuko wapi?

Inaelekea haujawahi kusikia habari za Mungu kiufasaha. Ndiyo maana una mitazamo yako binafsi ambayo ni potofu. Nakushauri fanya kama wafanyavyo wasomi wenye akili.

Chukua QURANI uisome mwanzo hadi mwisho.

FANYA hivyo na kwa Biblia, isome Mwanzo hadi Ufunuo.

Hapo ndipo utakapokuwa na uhalali wa kubisha au kukataa.

Tofauti na hapo, itakuwa ni sawa na kumshindanisha kipofu na mtu anayeona katika shindano la kubaini aina za rangi.
 
Inaelekea haujawahi kusikia habari za Mungu kiufasaha. Ndiyo maana una mitazamo yako binafsi ambayo ni potofu. Nakushauri fanya kama wafanyavyo wasomi wenye akili.

Chukua QURANI uisome mwanzo hadi mwisho.

FANYA hivyo na kwa Biblia, isome Mwanzo hadi Ufunuo.

Hapo ndipo utakapokuwa na uhalali wa kubisha au kukataa.

Tofauti na hapo, itakuwa ni sawa na kumshindanisha kipofu na mtu anayeona katika shindano la kubaini aina za rangi.
 
Jibu swali...usiniletee vitabu viwili kati ya dini 3000 duniani just coz hizi dini mbili zipo mtaani kwenu. Jibu swali maumivu unayasikiaje.. huwezi kaa kimya
 
Acha kurudia texts usipanic relax
 
Vitu ambavyo Nina amini bila ushahidi
1. Kwamba wewe ni mtoto wa fulani...

2. Kwamba wewe ulizaliwa tarehe fulani kisa tu uliambiwa hivyo na mzazi wako

3. Kwamba unao utumbo na huku hujawahi kuuona

4. Kwamba unao ubongo kwa vile ulishaaminishwa hivyo

... orodha ni ndefu...
 
Jibu swali...usiniletee vitabu viwili kati ya dini 3000 duniani just coz hizi dini mbili zipo mtaani kwenu. Jibu swali maumivu unayasikiaje.. huwezi kaa kimya
Katika hizo 3000 unamwamini Mungu wa dini ipi?
 
1. Kwamba wewe ni mtoto wa fulani...

2. Kwamba wewe ulizaliwa tarehe fulani kisa tu uliambiwa hivyo na mzazi wako

3. Kwamba unao utumbo na huku hujawahi kuuona

4. Kwamba unao ubongo kwa vile ulishaaminishwa hivyo

... orodha ni ndefu...
1. Documents zipo hata video ukitaka zipo
2. Same again official documents na video zipo
3. Naona kazi ya utumbo na Kuna binadamu Kama Mimi utumbo wao umeonekana so why shouldn't I trust the science telling me Nina utumbo.
4. Ninaona kazi ya ubongo, ninaona madhara ya watu wenye matatizo ya ubongo, Kuna CT scan technology mahospitalini, pia Kuna binadamu kama Mimi wameonekana ubongo wao ..
The evidence goes on
 
Si lazima uwe na ubongo kwa sababu tu wengine wanao ubongo. Kuna mtu alishawahi kufanyiwa upasuaji wa kichwa, kukakutwa maji tofauti na ilivyokuwa ikiaminika kuwa mtu asiye na ubongo hawezi kuishi.

Kama unaamini documents zilizoandikwa na mwanadamu ambaye yupo susceptible to errors, kwa nini usiziamimi na nyaraka zinazoweza kukusaidia katika maisha haya ya sasa na baada ya kuondoka duniani.
 
Siamini yoyote coz wote ni fikra...ila we unaamini ambae umekuta wazazi wako au jamii yako imeamini na wao wameamini kwa sababu ya ukoloni...
Siyo kweli. Sijafuata mkumbo. Nafahamu, bila chembe ya mashaka kuwa Mungu yupo. Nafahamu, pasi na shaka yo yote kuwa Mungu ni Halisi, Naam, ni Halisi hata kuzidi ngozi ya mwili wangu.

Nimejithibitishia pasipo shaka yo yote ile, kuwa Mungu Yupo na ananifahamu kwa jina langu. Hata wewe anakufahamu, na angefurahi kujidhihirisha kwako kama utamruhusu.

Katika hilo la uwepo wa Mungu, sihitaji kushawishi. Ninafahamu.
 
Jibu swali...usiniletee vitabu viwili kati ya dini 3000 duniani just coz hizi dini mbili zipo mtaani kwenu. Jibu swali maumivu unayasikiaje.. huwezi kaa kimya
Wewe ni mvivu wa kusoma?

Fuata maelekezo niliyokupa. Ukifanya hivyo, utagundua kuwa ulikuwa umedanganywa.
 
God dwell in light !...
 
Biblia ni Jibu la kila Swali katika maisha yako;Hivyo basi soma Biblia.
Biblia ina contradictions kibao ambazo nikikupa hapa huwezi kuzitengua, hilo linaonesha Biblia ni kitabu kisicho na mantiki, kilichoandikwa na watu tu, tena zama za ujinga.

Kama unabisha naweza kuziweka hapa tuzichambue.
 
Kama mtu anaamini kweli Mungu yupo, na anahesabu dhambi, na atatoa adhabu, hawezi kufanya kinyume na maagizo ya Mungu huyo.Mungu huyo alivyojengwa kidhana ni mkubwa sana na ana nguvu sana kumuasi.

Watu kufanya dhambi ni aina fulani ya kupiga kura ya kutokuwa na imani ya uwapo wa huyo Mungu.

Bado actions speaks louder than words, whether consciously or subconsciously.

Yani hata wewe ukifikiri unaamini Mungu yupo, ukajua kakataza kuiba, halafu ukaiba, hiyo ni rebellion inayotoa statement kwamba huamini sana kwamba Mungu yupo na atakuadhibu kwenda kwenye moto wa milele kwa dhambi zako. Watu wengi sana hawaamini Mungu yupo, wangeamini, dunia ingekuwa tofauti sana na ilivyo sasa.

In any case, huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Kama unabisha, thibitisha Mungu yupo.
 
Mkuu maelezo yako ya mwanzo yanafikirisha sana na yana ukweli mtupu.
Hitimisho lako ni ngumu kumeza.
By the way mimi ninaamini kuwa Mungu yupo, kuthibitisha ndio siwezi.
 
Mkuu maelezo yako ya mwanzo yanafikirisha sana na yana ukweli mtupu.
Hitimisho lako ni ngumu kumeza.
By the way mimi ninaamini kuwa Mungu yupo, kuthibitisha ndio siwezi.
Mimi sina tatizo na imani ya kuwepo Mungu.

Ni sehemu ya haki za binadamu, ipo katika "Universal Declaration of Human Rights" tangu December 10 1948.

Haki hii imetambuliwa na wasomi wengi wa tamaduni mbalimbali kwa maelfu na maelfu ya miaka.

Na mimi binafsi, ingawa siamini kuwa Mungu yupo, nitatetea vikali sana haki ya watu wanaoamini Mungu yupo kuamini hivyo, kwa uhuru.

Rais Paul Kagame wa Rwanda aliposema kwamba ana mpango wa kusajili wachungaji wote wa makanisa Rwanda, na wote wawe na angalau degree ya chuo, kama kigezo cha kuwa wachungaji, nilipinga wazo hilo vikali kama serikali kuingilia dini kinyume na kanuni za kidemokrasia za "separation of religion and state".

Sina tatizo na imani ya dini, kwa kweli, naona haki ya kuamini Mungu unavyotaka ni sura moja tu ya sarafu ile ile ambayo ina upande wa pili nilipo mimi, upande unaobeba haki ya kutoamini dini yoyote wala Mungu yeyote.

Kwa hivyo, najiona kwamba, nikifikiri kwa kina, kumkataza au kumnyanyapaa mtu kwa sababu anaamini dini au Mungu fulani ni sawasawa kabisa na kumnyanyapaa mtu asiyeamini dini au Mungu yeyote.

Imani ya dini/ Mungu (au kutokuwa na imani ya dini/Mungu) ni kitu kinachotakiwa kuwekewa ngao kikingwe, kama kitu cha faragha ya mtu kinachotakiwa kulindwa dhidi ya ubaguzi au unyanyapaa wowote.

Kitu muhimu kabisa kuelewa ni kwamba, ngao hii ya kuiweka kwenye imani ya dini/Mungu, watu waamini au wasiamini wanavyotaka, inafanya kazi wakati dini ikifanywa kama kitu cha faragha tu.

Kwa hivyo, kwa mfano, mkikaa msikitini mnapeana mawaidha ya Kiislamu, halafu akaja mtu msikitini kuwashambulia akisema Mungu hayupo na Uislamu ni uongo, huyo mtu hata mimi ambaye siamini Mungu yupo, nitamuona si mstaarabu na nitamlaani kwa kuingilia fragha ya uhuru wa watu kuabudu Mungu wanavyotaka.

Lakini, ukija JF na kuanzisha thread kuhusu uzuri wa dini ya Uislamu kama dini ya Mungu wa kweli, hapo umeshajiondolea ngao ya faragha ya kuachiwa, kwa sababu umeleta mjadala wa hadhara uwanja wa wazi, hapo utapingwa kwa facts and figures, logic and history, theory and practice, philosophy and scholarship, bila huruma, na ukisema kila mtu ana uhuru wa kuamini anavyotaka, utaonekana huelewi nuance ya jambo hilo, kwamba ukishavuka faragha ulizopewa, umeruhusu watu kukuhoji, kukukatalia, kukupiga maswali na mara nyingine hata kukukashifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…