Mungu Yuko wapi?

Kumbe Mungu ana hasira?

Hii inadhibitisha kuwa si mkamilifu,
Ahsante kwa kunipa somo jipya
 
Acha kumtisha mpe hoja
 
Kenya watu wamefunga kula chakula mpaka wamekufa ili waende mbinguni, waliaminishwa hivyo na pasta wao
 
Bac Kama yupo Rohoni kwa kila mtu hatuhitaji Biblia, kanisa, wachungaji, papa na maujinga mengine. Tunahitaji kutumia akili zetu kuishi
Unaihitaji sana Biblia, sisi binadamu huzaliwa tukiwa na ubongo uliowazi (ombwe) tunahitaji maarifa ili kuujaza.

Nguvu ya ndani ya mwili,vipaji,utashi umahiri unajitokeza pale mtu anapoongeza jitihada, vivyo hivyo kwa kumfahamu muumba sharti usome miongozo yake (Biblia) upate kumfahamu vizuri.
 
Hizi story za kumuambia mtoto ili asiwe anaiba pipi Ila sio mimi. Nenda kasome biology nervous system form 2 alafu urudi.
 
Nimesoma Biblia na inamakosa kuhusu dunia, viumbe, historia, Sayansi na utu kuliko kitabu chochote katika historia ya binadamu. Ukitaka uache ukristo soma Biblia. Hata mtoto wa la pili anaweza akatengeneza storybook na ikaeleweka kuliko Biblia. Kama unabisha nitajie Babu yake Yesu mzaa baba ni nani?
 
Mungu ni mada pana sana maana kuna miungu mingi mno mengine ikiwa watu, vitu na roho, nafsi ila aliyeumba kila kitu ni MMOJA.

Ndo maana ikaandikwa katika Yeremia 10:11 kuwa wakati ukifika Miungu isiyoumba mbingu na nchi lazima iangamizwe.

Je, kwanini kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu aliyeumba vyote, wote na yote kuwepo ama kutokuwepo?

Kwa sababu uumbaji wote ulitekwa nyara baada ya aliyekasimiwa uumbaji kuvamiwa (Moyo Wa Mwanzo, Mwanzo 1:1)ndo maana ukija soma katika 1korintho 15:24-28 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.”

“Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.”

Tuki soma hapo tunaelewa kwamba kumbe Ufalme, mamlaka na nguvu havikuwa kwa muumba baada ya uumbaji kutekwa, ndo maana hata ibilisi alikuwa na uwezo wa kumpandisha Yesu kwenye kinara na kumwambia hii yote unayoona ni miliki yangu nisujudie nikupe yote katika Luka 4:6 “Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.”


Kitu ambacho wengi hawajui ni kuwa aliyetuumba anaenda kwa majira na wakati na habaki palepale kila lango (siku). Mfano habari za Yesu ziliandikwa tangia kipindi cha nabii Isaya lakini alipokuja wayahudi wakamkataa na kusema ni mtoto wa seremala tu wao wanamsubiri masihi paka leo 90% ya waisrael hawamkiri Kristo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…