Mungu Yuko wapi?

Mungu Yuko wapi?

Usitake kuonekana mwelevu kufanya kufuru ili ufurahishe watu au kikundi fulani nakushauri usijitafutie laana kwa haya maandiko yako maana hasira ya Mungu ni kali sana tubu jiepusha na hizi kauli (acha kumfanyia kazi shetani kupotosha kondoo wa Mungu ) usipo sikia ipo siku na saa utakumbuka maandishi haya
Kumbe Mungu ana hasira?

Hii inadhibitisha kuwa si mkamilifu,
Ahsante kwa kunipa somo jipya
 
Usitake kuonekana mwelevu kufanya kufuru ili ufurahishe watu au kikundi fulani nakushauri usijitafutie laana kwa haya maandiko yako maana hasira ya Mungu ni kali sana tubu jiepusha na hizi kauli (acha kumfanyia kazi shetani kupotosha kondoo wa Mungu ) usipo sikia ipo siku na saa utakumbuka maandishi haya
Acha kumtisha mpe hoja
 
Mi najiuliza maswali mengi. Mungu Ni Nini, anataka Nini na Yuko wapi.

Ukifuatilia historia ya binadamu tokea tukiwa wawindaji maporini miungu ilikuwepo. Wazee walikuwa wanaongoza vijana kwa kuwaambia kuwa Mungu anataka mfanye hivi, na hio miungu ilikuwepo pangoni ambapo wazee tu wanaingia, baadae vijana wakajitoa akili kwenda wakaona wazee ni waongo na hamna kitu mule. Wagiriki wakaja na miungu yao wakasema ipo ya milima ya Olympus, Leo hii watu wamepanda milima yote ugiriki hawajaona miungu hio.

Wakaja wayahudi, wakasema Mungu yupo mawinguni. Ukifuatilia hata Yesu alipaa mawinguni, Mungu alifungua madirisha ya mbinguni kuleta mafuriko, alichungulia kutoka mawinguni kwenye mnara wa babel, etc. Waislamu nao wakaja na mbingu Saba sijui. Anyways wazungu wametengeneza ndege na rocket zimeenda mawinguni, nje ya dunia, mpaka mwezini. Sasa hivi watu wa dini wanasema yupo nje ya ulimwengu.

So nikagundua trend, wanamficha, wanamweka mbali ili watu wasiweze kumfikia, why? Kwa sababu hayupo? Kwa sababu hajasema hizo sheria? Why wanamficha. Afu wanakuambia anataka uamini yupo ndo utapona usipoamini unaunguzwa. Ukiuliza nikimwona afu nikamwamini, anasema no, lazma usimwone ndo uamini. Na wanaweka kifo mwisho wa kumuani ili waweze kuendelea kutunga sheria kwa jina lake na kuweza kuendelea kutawala watu kwa sababu hamna mtu Ashawahi kurudi akasema baada ya kifo kipo hivi.

Mwanasayansi mi nauliza Mbinguni Kuna Nini. Hamna njaa hamna maumivu hamna ndoa hamna chochote zaidi ya kumuabudu Mungu. Watu kanisani na msikitini hawapendi kwenda unategemea watapenda milele ya Ibada. So wakaamua kuanzisha motoni kutishia watu kwamba wataunguzwa milele. Sasa, ukifa unaacha mwili wako hapa, wanasema una roho, roho ni Nini, hoo mawazo sijui pumzi, ukiuliza unajua kazi ya ubongo ni Nini mtu hajui, haya tufanye roho ni ka upepo kanaenda motoni ehe kanaunguaje, hakana nyama, hakana nervous system hakana ngozi, hakana pain receptors, hakana ubongo au spinal cord, maumivu unayasikiaje, na bado hatujauliza huu Moto upo wapi, walisemaga chini kisa mavolcano lakini now hawasemi Tena coz of elimu.

Tukienda kwenye sheria zenyewe sijui usivae nguo tofauti, usile shellfish, usichanganye mazao, usimwage nje, usiabudu sanamu lakini abudu kitu Cha kufikiriwa na myahudi, hivi kwa Nini mtu atengeneze nyota billion 60 na sayari trillion afu aje kujali binadamu wewe ambae ni Kama vumbi kwa huu ulimwengu unamwaga wapi. Na kwa Nini sheria hizi zinaonekana Kama sheria za kabila ya la zamani huko kwenye majangwa na haziendani na sheria za binadamu kuishi na watu vizuri. Na Wanavyosema tumuabudu siku ya Saba.

Siku zimekuja kutengenezewa baadae Sana na zimebadilika badilika Mara kwa Mara katika historia ya Mayans na Romans. Na wamechagua sun day coz ni siku ya pagans kuabudu jua. Ila yote haya tuyaache, why Mungu muweza yote anataka hela, mwisho wa siku wote mnabidi mgundue kuwa binadamu walitengeneza miungu ili kujibu maswali magumu yasiyojibika kipindi kile na ku
Kenya watu wamefunga kula chakula mpaka wamekufa ili waende mbinguni, waliaminishwa hivyo na pasta wao
 
Bac Kama yupo Rohoni kwa kila mtu hatuhitaji Biblia, kanisa, wachungaji, papa na maujinga mengine. Tunahitaji kutumia akili zetu kuishi
Unaihitaji sana Biblia, sisi binadamu huzaliwa tukiwa na ubongo uliowazi (ombwe) tunahitaji maarifa ili kuujaza.

Nguvu ya ndani ya mwili,vipaji,utashi umahiri unajitokeza pale mtu anapoongeza jitihada, vivyo hivyo kwa kumfahamu muumba sharti usome miongozo yake (Biblia) upate kumfahamu vizuri.
 
Kuna mtu alisema ubongo ni receiver tu, kuna master brain ipo ambayo inatunza kumbukumbu zako na ikifika siku ya mwisho ndo tutajua hatujui pale utakaposhangaa una mwili mpya na ubongo mpya usioungua ukaisha ila maumivu hayazoeleki.

INASIKITISHA MNO.
Hizi story za kumuambia mtoto ili asiwe anaiba pipi Ila sio mimi. Nenda kasome biology nervous system form 2 alafu urudi.
 
Unaihitaji sana Biblia, sisi binadamu huzaliwa tukiwa na ubongo uliowazi (ombwe) tunahitaji maarifa ili kuujaza.

Nguvu ya ndani ya mwili,vipaji,utashi umahiri unajitokeza pale mtu anapoongeza jitihada, vivyo hivyo kwa kumfahamu muumba sharti usome miongozo yake (Biblia) upate kumfahamu vizuri.
Nimesoma Biblia na inamakosa kuhusu dunia, viumbe, historia, Sayansi na utu kuliko kitabu chochote katika historia ya binadamu. Ukitaka uache ukristo soma Biblia. Hata mtoto wa la pili anaweza akatengeneza storybook na ikaeleweka kuliko Biblia. Kama unabisha nitajie Babu yake Yesu mzaa baba ni nani?
 
Mungu ni mada pana sana maana kuna miungu mingi mno mengine ikiwa watu, vitu na roho, nafsi ila aliyeumba kila kitu ni MMOJA.

Ndo maana ikaandikwa katika Yeremia 10:11 kuwa wakati ukifika Miungu isiyoumba mbingu na nchi lazima iangamizwe.

Je, kwanini kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusu aliyeumba vyote, wote na yote kuwepo ama kutokuwepo?

Kwa sababu uumbaji wote ulitekwa nyara baada ya aliyekasimiwa uumbaji kuvamiwa (Moyo Wa Mwanzo, Mwanzo 1:1)ndo maana ukija soma katika 1korintho 15:24-28 “Hapo ndipo mwisho, atakapompa Mungu Baba ufalme wake; atakapobatilisha utawala wote, na mamlaka yote, na nguvu.”

“Maana sharti amiliki yeye, hata awaweke maadui wake wote chini ya miguu yake.”

Tuki soma hapo tunaelewa kwamba kumbe Ufalme, mamlaka na nguvu havikuwa kwa muumba baada ya uumbaji kutekwa, ndo maana hata ibilisi alikuwa na uwezo wa kumpandisha Yesu kwenye kinara na kumwambia hii yote unayoona ni miliki yangu nisujudie nikupe yote katika Luka 4:6 “Ibilisi akamwambia, Nitakupa wewe enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo.”


Kitu ambacho wengi hawajui ni kuwa aliyetuumba anaenda kwa majira na wakati na habaki palepale kila lango (siku). Mfano habari za Yesu ziliandikwa tangia kipindi cha nabii Isaya lakini alipokuja wayahudi wakamkataa na kusema ni mtoto wa seremala tu wao wanamsubiri masihi paka leo 90% ya waisrael hawamkiri Kristo.
 
Back
Top Bottom