Mungu Yuko wapi?

Ulikutana na kibano? Nami nilikuwa hivyo, sasa mtu hanidanganyi wala haniambii kitu kuhusu Mungu.
haha, nilikutana na kibano ndugu niliingia kijiji flan kigoma kijijini.imefika usiku nimeingia kulala ni kakalibishwa kwa shoti ukutaani kama za radi, siku ya pili nilikuwa naota ile kuamuka nakuta wazee wangwasuma wamenizingira geto natoa sauti ikawa haitoki ndipo nikajitoa ufahamu nikasema kwa jina la yesu wanga wakapotea pale pale.
 
Na ndio maana nakwambia sasa wapo madaktari kabisa ambao wanaamini Mungu na kuamini story zilizoelezwa kwenye vitabu vya dini.
Sababu ni zile zile uoga au kuaminishwa tokea utotoni na mazingira uliyokulia,
 
Nimetaja waarabu kama watu ambao ni matajiri ila wanaamini Mungu, waislamu wapo hata afrika ambako ni masikini kwahiyo ni wewe tu mwenye umekurupuka.
Sio waarabu wote matajiri, Kuna nchi uarabuni Kama Lebanon, Jordan, Yemen, west bank, Libya ni maskini, waarabu sio Dubai tu
 
Duh! Mkuu jaribu kuwa muelewa sijui kwanini bado umekazania kushindanisha? Waafrika elimu wanayo ndio maana kuna mahospitali na kuna madaktari sio waganga wa kienyeji.
Waganga wa kienyeji wapo wengi bongo kuliko ulaya, so huwezi prove chochote
 
Kwanini anitokee mimi? Kwa nini hauulizi hajakutokea wewe?
Coz hayupo ndo maana, Ila ubongo wangu ungeamua kumuota ningesema kanitokea, si ka watu wanaotokewa na Bikra maria chumbani, Kama we sio mkatoliki huwezi tokewa nae why asa, it shows ni mind imeamua kuamini na kutengeneza thoughts za Mungu Ila sio reality
 
Umechagua bible na sio kitabu Cha wahindi why? Kwa nini Biblia isieleweke directly mpaka mtu asome in a way kila kitu kimake sense, kwani vitabu vingine vyote huvisomi hivyo ila Biblia inapokosea unafosi kuipatisha
 
Sijasema kukuaminisha ila nachokuuliza kwanini unakimbilia uthibitisho? Ina maana unaogopa kuaminishwa ndio maana unakimbilia kudai uthibitisho kama kinga ya kuzuia usibadilishiwe mtazamo uliyonao sasa?
Siogopi Mimi, nikikuambia mama Ako kafa lakini we unamwona afu nakuambia we unaona yupo coz huamini Kama hayupo, we si utaniona chizi, lakini comes to God ambae hamna mtu Ashawahi kumwona Ila tunaambiwa yupo
 
Sio elimu ya darasani ya kujua mitochondria is the powerhouse of the cell, elimu ya kureason na logic na kugenerate ideas, hamna scientific discoveries au philosophical ideas za mtanzania, si kazi yetu ni kusoma kilichogunduliwa na wenzetu so huwezi linganisha elimu yetu na ya kwao
 
Swali langu kwanini unakimbilia kudai evidence? Sio kwamba nataka kulazimisha ukubali uwepo wake ila nachouliza ni huko kukimbilia kwenye hitimisho la kudai evidence, unaogopa nini? Nasema hivyo kwa sababu kudai evidence imekuwa kama kinga.
Why kila aspect ya maisha unataka uthibitisho wowote uwe convinced Ila kwenye swala la Mungu unajitoa akili?
 
Unajuaje nguvu ni ya Mungu
 
huamini kwa sababu haijakutokea,so waliopata shida kwa hayo ambayo huya amini sasaivi wana kuchukulia fara tu,kwanza hujitambui, nyindo wale mkifanikiwa ubisho mwingi munaona wengine hawajui kutafuta
Wewe unaweza ukawa na matatizo yako ukasema ni uchawi mwingine akatafsiri kilogic na akalitatua bila uganga Wala mwamposa, we kusema umetokea na mapepo ni we kushindwa kutafsiri natural phenomena ukaassume ni mapepo. Mi nililala usiku nikaganda Ila sikupanic coz najua ni sleep paralysis ila mtu mwingine atajua ni jinamizi ataanza kutafuta mganga au mchungaji. Knowledge is power, ukielewa circumstances za ubongo vizuri huwezi kuamini uchawi
 
Hope sio sawa na faith. Kiswahili ni lugha pungufu imefanya neno liwe moja. Hope ni kutamani kitu fulani litokee...Imani ni kuamini kitu bila udhibitisho... Kuna uthibitisho mkubwa kuwa mtu akilala anaamka, lakini hamna uthibitisho wa Mungu kuwepo
Hiyo tafsiri ya kusema imani ni kuamini kitu bila uthibitisho umeipata wapi? Hebu nipe mfano wa jambo moja la kuamini kwa uthibitisho.

Kutokuwa na uthibitisho wa kuwepo Mungu ni jambo moja na wewe kudai kwa uhakika kuwa hakuna Mungu ni jambo lengine, uhakika wa kwamba hakuna Mungu we umeupata wapi?
 
Hujiulizi why vinatokea kigoma a place ambao Ina watu wenye low level of economic status na low level of education. Why not Moshi, dar, Arusha na bukoba. Why places za tanga, sumbawanga, shinyanga na kigoma places zenye watu wenye maisha duni na wasio na elimu
 
Google maana ya faith halafu urudi.
Hauna uhakika kwamba Babu Christmas, fairies, goblins, vampires, were wolves, dragons, unicorns, easter bunny etc hawapo, Ila huwaamini kuwa wapo, same as me, Sina uhakika Kama Mungu yupo au hayupo, nyie mnasema mna uhakika ndo maana naomba uthibitisho kuwa Mungu yupo na ndio aliyeandikwa kwenye Biblia au Quran na sio wa kihindi au kigiriki
 
 
Hayo mambo yapo. Shetani yupo, na Mungu Yupo, lakini Mungu anao uweza wote.

Wanaobisha ni kwa sababu ama hawajahusishwa kukutana na hayo mazingits au wanakusudia kufanya hivyo kwa lengo la kuwapotosha wasio na ufahamu sahihi.

Matukio ya kishirikina na ya Mungu pia yanafahamika kote duniani, kuanzia Afrika, Ulaya, Amerika na Asia, n.k.

Kipindi Magufuli akiwa Rais, alisimulia tukio lililotokea alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kulikuwa na ujenzi wa daraja pande za Sumbawanga ambapo kila daraja liliposetiwa, setting ilibadilika tofauti na ilivyosetiwa. Tukio hilo liliwafanya maingeneer kuogopa kuendelea na kazi maeneo hayo, ikabidi Magufuli na baadhi ya viongozi kwenda kuonana na wazee wa huo ukanda, na baada ya kufuata masharti yao, ndipo zoezi lilipoweza kuendelea.

Ushirikina upo, na Mungu yupo. Ni wazi kuwa kilichokuwa kikiwakwamisha hao mainjinia ni nguvu za giza, na tatizo likatatuliwa kwa nguvu za giza vile vile.


Mwaka fulani, tulienda Singida na timu ya watu kadhaa kwa jambo fulani. Tukiwa tumelala Usiku kwenye chumba tulichokifikia ambapo tulikuwa tukikitumia kama kambi, huku mlango ukiwa umefungwa, nilimshuhudia mtu akiwa ameingia ndani na kuanza kutembea taratibu kuelekea tulikolala. Mlango ulikuwa umefungwa, lakini aliweza kuingia ndani bila mlango kufunguliwa.

Nilinyanyuka na kukaa kitandani kwa muda nikimtazamza, lakini bila hofu hata kidogo. Baada ya muda, nilimpuuzia kwa kusema "SHAURI ZAKE". nikalala kama hakuna kilichotokea.

Muda mfupi baadaye, mmoja wetu alipaza sauti, "KWA JINA LA YESU", kisha karibia wote tukaangua kicheko.

Kumbe nao pia walimwona lakini wakaamua kumpuuzia. Mpaka alipokuwa amekaribia kabisa tulikolala, karibia wote walikuwa wamemwona. Lakini baada ya kutamkiwa, "KATIKA JINA LA YESU", alitoweka.

Sasa mtu mwingine anaweza asiamini kwamba kuna ushirikina kwa vile tu, labda hajakutana na hiyo changamoto. Mtu anawezaje kuingia ndani ya nyumba iliyofungwa mlango?

Uchawi upo, na nguvu za Mungu zipo, lakini nguvu za Mungu zina nguvu zaidi kuliko nguvu zingine zozote.
 
Kwahiyo hiyo tafsiri ya imani ni kuamini bila uthibitisho umeitoa google? Mimi sijaiona huko google nipe link, halafu nipe na mifano ya kuamini kwa uthibitisho.

Wanasema kuna Mungu wanaamini hivyo inajulikana ni imani, wewe unasema(sio imani) hakuna Mungu na kama yupo tukupe uthibitisho.
 
Umechagua bible na sio kitabu Cha wahindi why? Kwa nini Biblia isieleweke directly mpaka mtu asome in a way kila kitu kimake sense, kwani vitabu vingine vyote huvisomi hivyo ila Biblia inapokosea unafosi kuipatisha
Ulishawahi kusafiri kwa basi toka Dar hadi Mwanza, au kwingineko ambako ilikuwa ni safari ya mbali? Labda ilikuwa ni safari yako ya kwanza kwenye hiyo route, ulipotea kwa vile hujawahi kuipita?

Naamini hukupotea. Na sababu ni kwa vile ulipanda gari sahihi. Haikukusumbuka kufika mkoa ulioulenga kwa vile ulipanda gari linaloenda huko.

Biblia haijakosea hata kitu kimoja. Biblia ni gari la maisha. Ukikaa nje yake hautaelewa kulivyo kwa ndani, wala inakoweza kukufikisha.

Neno la Mungu ni NJIA YA KWELI NA UZIMA. Kila aipitaye hiyo Njia hawezi kupotea.

Kama unataka kuifahamu, ingia ndani. Panda, itakfikisha unakopaswa kufika.

Nimelionja NENO la Mungu, najua lilivyo na ladha nzuri na afya Bora. Hakuna wa kunidanganya kuhusu uhai Wake.

Najua BIBLIA ilikonitoa, najua ilivyonisaidoa na hata sasa inavyonisaidia. Najua ilikonivusha baada ya kila kitu kushindwa, ikiwemo degree yangu na ya walionizidi kwa Elimu.

Sasa kwa nini nikisome kitabu kingine, wakati hiki nilichojiridhisha kuwa kinanisaidia kuliko kitabu kingine chochote nilichowahi kukisoma, bado sijala vya kutosha?

Vingine naweza kuvisoma nikipata muda, lakini acha niendelee kuibugia kwanza Biblia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…