Hayo mambo yapo. Shetani yupo, na Mungu Yupo, lakini Mungu anao uweza wote.
Wanaobisha ni kwa sababu ama hawajahusishwa kukutana na hayo mazingits au wanakusudia kufanya hivyo kwa lengo la kuwapotosha wasio na ufahamu sahihi.
Matukio ya kishirikina na ya Mungu pia yanafahamika kote duniani, kuanzia Afrika, Ulaya, Amerika na Asia, n.k.
Kipindi Magufuli akiwa Rais, alisimulia tukio lililotokea alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kulikuwa na ujenzi wa daraja pande za Sumbawanga ambapo kila daraja liliposetiwa, setting ilibadilika tofauti na ilivyosetiwa. Tukio hilo liliwafanya maingeneer kuogopa kuendelea na kazi maeneo hayo, ikabidi Magufuli na baadhi ya viongozi kwenda kuonana na wazee wa huo ukanda, na baada ya kufuata masharti yao, ndipo zoezi lilipoweza kuendelea.
Ushirikina upo, na Mungu yupo. Ni wazi kuwa kilichokuwa kikiwakwamisha hao mainjinia ni nguvu za giza, na tatizo likatatuliwa kwa nguvu za giza vile vile.
Mwaka fulani, tulienda Singida na timu ya watu kadhaa kwa jambo fulani. Tukiwa tumelala Usiku kwenye chumba tulichokifikia ambapo tulikuwa tukikitumia kama kambi, huku mlango ukiwa umefungwa, nilimshuhudia mtu akiwa ameingia ndani na kuanza kutembea taratibu kuelekea tulikolala. Mlango ulikuwa umefungwa, lakini aliweza kuingia ndani bila mlango kufunguliwa.
Nilinyanyuka na kukaa kitandani kwa muda nikimtazamza, lakini bila hofu hata kidogo. Baada ya muda, nilimpuuzia kwa kusema "SHAURI ZAKE". nikalala kama hakuna kilichotokea.
Muda mfupi baadaye, mmoja wetu alipaza sauti, "KWA JINA LA YESU", kisha karibia wote tukaangua kicheko.
Kumbe nao pia walimwona lakini wakaamua kumpuuzia. Mpaka alipokuwa amekaribia kabisa tulikolala, karibia wote walikuwa wamemwona. Lakini baada ya kutamkiwa, "KATIKA JINA LA YESU", alitoweka.
Sasa mtu mwingine anaweza asiamini kwamba kuna ushirikina kwa vile tu, labda hajakutana na hiyo changamoto. Mtu anawezaje kuingia ndani ya nyumba iliyofungwa mlango?
Uchawi upo, na nguvu za Mungu zipo, lakini nguvu za Mungu zina nguvu zaidi kuliko nguvu zingine zozote.