Mungu Yuko wapi?

Wakristo mmekuta dini ya wayahudi mmeiba mmeongeza story zenu mnajigamba. Ukimaliza uniambie aliyemuumba Mungu Ni nani?
 
Wakristo mmekuta dini ya wayahudi mmeiba mmeongeza story zenu mnajigamba. Ukimaliza uniambie aliyemuumba Mungu Ni nani?

Ukikaa kwenye kituo cha dini sijui ukristo na uislam au dini yeyote hutamwelewa aliyeumba maana yeye hana dini wala dhehebu. Na aliyeumba yeye hajaumbwa bali yeye ndo CHANZO HALISI (Real Source) wa kila kitu.
 
𝐓𝐡𝐞𝐫𝐞 𝐢𝐬 𝐒𝐮𝐩𝐞𝐫 𝐍𝐚𝐭𝐮𝐫𝐚𝐥 𝐏𝐨𝐰𝐞𝐫(𝐄𝐱𝐚𝐥𝐭) 𝐟𝐨𝐫 𝐞𝐚𝐜𝐡 𝐚𝐧𝐝 𝐞𝐯𝐞𝐫𝐲𝐭𝐡𝐢𝐧𝐠 𝐭𝐡𝐢𝐧𝐤 𝐡𝐨𝐰 𝐢𝐬 𝐡𝐞𝐦𝐢𝐬𝐩𝐡𝐞𝐫𝐞 𝐚𝐧𝐝 𝐭𝐡𝐞 𝐞𝐧𝐭𝐢𝐫𝐞 𝐩𝐥𝐚𝐧𝐞𝐭𝐬.
 
Usimtishe mueleweshe ila kwa mwenye akili na vilivyomo humu duniani mwenye akili lazima ajue vina mwenyewe
 
Tatizo lako una soma Biblia kama story book.

Biblia ni kitabu kilichokamilika tena kwa matukio mengi haswa..Jibu lako lipo kitabu cha Mathayo 1:1-17
 
Attachments

  • Screenshot_20230514-213746.png
    48 KB · Views: 19
Pole sana!
 
Tatizo lako una soma Biblia kama story book.

Biblia ni kitabu kilichokamilika tena kwa matukio mengi haswa..Jibu lako lipo kitabu cha Mathayo 1:1-17
Umejiona mjanja ee ndo maana nakuambia soma Biblia nzima ndo urudi. Haya nenda kasome luka 3 23 mpaka 38 uniambie Babu yake Yesu Ni nani. Jacob au Heli. Ukija na jibu moja nishtue
 
Hii simulizi na hekaya umeitoa wapi ? Uliwahi kua na huo mwili mpya ukaonja joto ya jiwe au umesimuliwa na waliowahi kufanywa hivyo ? Mda mwingine tuwe na kiasi Cha kuogopeshana jaman, usiwajaze watu uoga swali ni kwamba ukifa unaenda wapi ?
 
Ushaambiwa ukiondoa DINI hakuna MUNGU, kwa hio jiongezee unataka kua mpagani au unataka kua mtu wa dini zilizoletwa na Majahazi ?

Sio kweli maana hata kipindi cha Ibrahim ambapo wakristo kwa waislam wanaamini ndo Baba yao kila mtu akivutia kwake hakukuwa na DINI na Ibrahimu hakuwa na DINI.

Dini zimeanza baada ya Isaka na Ishamael kumzika baba yao Ibrahim na kila mmoja kwenda njia yake akifundishwa namna ya kuabudu na mama yake ndo ukatokea ukristo na uislam kabla ya hizi zengine zote.

Muumba wa vyote, wote na yote hana DINI.
 
Ndio maana nikasema ukiondoa DINI hakuna MUNGU, wewe hizo habari kusingekua na Biblia au Qur'an ungezijulia wapi ?
 
Umejiona mjanja ee ndo maana nakuambia soma Biblia nzima ndo urudi. Haya nenda kasome luka 3 23 mpaka 38 uniambie Babu yake Yesu Ni nani. Jacob au Heli. Ukija na jibu moja nishtue
Wapi pamekuchanganya hapo. hakuna ujanga wowote hapo ni kuelimishana
 
Attachments

  • Screenshot_20230514-215411.png
    44.6 KB · Views: 23
  • Screenshot_20230514-213746.png
    48 KB · Views: 24
Hakuna ambaye haabudu chochote yaani wapagani kama wanavyoitwa,ndo maana ikaandikwa hazina ya mtu ilipo ndipo na moyo wake ulipo.

So kama unaabudu sana hela basi huyo ndo mungu wako maana hela ni Roho.
 
Wapi pamekuchanganya hapo. hakuna ujanga wowote hapo ni kuelimishana

Usisome Kitabu (biblia) kama historia ndo maana kuna majira na wakati wa kila jambo katika Kitabu mfano, Katika 1Korintho 15:28 inasema mwana naye yaani Yesu atawekwa Chini ya Muumba wa vyote,wote na yote “Basi, vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake, ndipo Mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiishia vitu vyote, ili kwamba Mungu awe yote katika wote.”

Na katika Zekaria 14:9 inasema Majira ikifika “Naye Bwana atakuwa Mfalme juu ya nchi yote; siku hiyo Bwana atakuwa mmoja, na jina lake moja.”

Lakini wengi wanaamini aliyeumba anamajina meeengiiii but hayo majina yote ni nafsi zinazojitegemea katika majira husika ilikuwa sawa.
 
Ndio maana nikasema ukiondoa DINI hakuna MUNGU, wewe hizo habari kusingekua na Biblia au Qur'an ungezijulia wapi ?

Biblia sio kitabu cha dini ndo maana nakiita KITABU but kupitia mabadiliko ya majira na wakati mbalimbali ikafanywa ya dini ila hata kabla ya ukristo kilikuwepo kipindi cha Mussa ambaye ndie ameandika kitabu cha MWANZO,Isaya na manabii wengi tu wakubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…