Mungu Yuko wapi?

Zikiondolewa hizo contradictions ndio itakuwa uthibitisho kuwa Mungu yupo? au itafanya kuwa hiyo story ni ya kweli? au itakuwa zimeondolewa contradictions tu kwenye hiyo story?
Ukiondoa contradiction utakuwa umeweka uwezekano wa Mungu huyo kuwepo.
Unaelewa hilo.

Mungu hayupo.

Mungu ambae ni muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ambae kaumba ulimwengu huu wenye mabaya kuwezekana hayupo na hawezekani kuwepo.

Nisawa na wewe nikwambie kuwa UHURU JR ni mwanaume bishoo halafu pia ni mwanamke mrembo.
Katika uhalisia UHURU JR wa design hiyo hayupo na hawezekani kuwepo sawa kabisa na Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote katika ulimwengu huu wenye mabaya kuwezekana.
 
Mungu wa design hiyo hayupo sawa, haya je yupo Mungu wa design gani? Bila ya shaka jibu lako litakuwa hakuna Mungu kabisa maana huo ndio msimamo na ndio uliyokusukuma kwenye hiyo contradiction kupata jibu la kuwa hakuna Mungu tu na si vinginevyo.
 
Unapataje uhakika wewe kwamba Atheists hawana jibu hilo?

Huo msingi wa kukataa uwepo wa Mungu hujauelewa wewe au nawao hawauelewi?

Unaweza ondoa contradiction katika dhana ya uwepo wa Mungu?

Unaweza thibitisha Mungu yupo?
Kama wewe unayo majibu yalete hapa nipo hapa nayasubiri.
 
Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;

Zaburi 14:1
Yaani umejibu vizuri sana Man. Kwa binadamu yeyote anayepambana anajua uwepo wa Mungu. Mungu amenitoa mbali sana mpaka hapa aliponifikisha. Nipo nchi za watu naona vizazi vyao vinavyoangamia kwa kukosa maarifa. Wahindi wanawapiga bao, hawajui kuwa wahindi wanatenga chumba maalumu cha kuabudu majumbani mwao. Vijana wa kizungu wameacha kusali, wanaamini wao wana nguvu juu ya vyote. Nchi kama Ujerumani inajaribu kuwabeba vijana wake lakini hawabebeki. Wanawaza ngono na kulewa tu. Aissee we acha tu angalau hiki kizazi kingesikiliza wakongwe kingefika mbali.
 
🤣🤣
 
Mungu wa design hiyo hayupo sawa, haya je yupo Mungu wa design gani? Bila ya shaka jibu lako litakuwa hakuna Mungu kabisa maana huo ndio msimamo na ndio uliyokusukuma kwenye hiyo contradiction kupata jibu la kuwa hakuna Mungu tu na si vinginevyo.
Mkuu,
Embu tuelewane, wewe umekuja na madai kuwa kuna Mungu.

Lakini katika uhalisia hayupo.

Sisi wanadamu tumeumba dhana hii ya Mungu ili kujificha pindi tunapoishiwa maarifa.
Miungu wako wengi sana, kwahyo naposema Mungu wa design ile (Mwenye sifa ya uwezo wote ujuzi wote na upendo wote)

Kwani unajuaje kama kitu flani kipo?

Unaweza thibitisha kuwa Mungu yupo kweli katika uhalisia na sio mawazo yenu tu katika kuelezea vitu?
 
Kama wewe unayo majibu yalete hapa nipo hapa nayasubiri.
Mkuu,
Msingi wa mjadala huu unatokea hapa ulipohoji
Kwanza ajabu sana mtu ambaye ni atheist anapokuja na hoja ya kudai kwamba et hakuna Mungu kwa sababu ya contradictions kana kwamba hiyo contradiction ndio iliyomfanya asiamini Mungu.

Ki hakika hilo swali hata atheists wenyewe hawana jibu, maana huko kutokuamini katika Mungu/miungu ni msimamo ambao haujaeleweka msingi wake ni upi.
Msingi wa kutokuamini katika Mungu unatokana na kwamba Mungu hayupo.

Kitu kisichokuwepo ni hakipo tu.

Kama yupo, bhasi thibitisha uwepo wake.!
 
Nakwambia hivi issue sio Mungu wa design ile bali ni huo msimamo wako wa kwamba hakuna kabisa Mungu, ndio maana katika hiyo contradiction kwako wewe inakupa jibu moja tu la kuwa Mungu hayupo na si vinginevyo.
 
Nakwambia hivi issue sio Mungu wa design ile bali ni huo msimamo wako wa kwamba hakuna kabisa Mungu, ndio maana katika hiyo contradiction kwako wewe inakupa jibu moja tu la kuwa Mungu hayupo na si vinginevyo.
Unadhani kwanini nina huo unaouita wewe ni msimamo!?

Kwanini unataka kulazimisha Mungu awepo ilihali hayupo tu.

Mifumo yote ya mwili inayohusika na utambuzi haioneshi kivyovyote vile Mungu yupo zaidi ni kwamba hayo ni mawazo ya watu tu kama sio hadithi za uongo za kutungwa na watu tu.

Tunaelimishana tu hapa, kuna mambo tumeshindwa kuyaelewa kwasbabu ya dhana hii ya miungu.

Je unaamini Mungu yupo au ni unauhakika kuwa Mungu yupo?
Kama una uhakika Unaweza kunielezea ulitambuaje kuwa kuna Mungu na ukajiridhisha?
 
Mkuu,
Msingi wa mjadala huu unatokea hapa ulipohoji



Msingi wa kutokuamini katika Mungu unatokana na kwamba Mungu hayupo.

Kitu kisichokuwepo ni hakipo tu.

Kama yupo, bhasi thibitisha uwepo wake.!
Umethibitisha nilichokisema kuwa contradiction sio sababu yenye kuwafanya atheists waseme hakuna Mungu.

"Kusichokuwepo hakipo tu"

Hapa hatubishani kwamba kisichokuwepo kipo au hakipo bali tunachotofautiana hapa ni kipi hicho ambacho hakipo? Umejuaje hakipo?
 
Mimi silazimishi na ndio maana suala la Mungu ni katika masuala ya imani, hivyo siwezi kukulazimisha.

Sio muhimu kwa nini wewe una huo msimamo maana kila mmoja anaweza akawa na sababu yake ila tatizo ni msingi wa huo msimamo ndio kitu kisichofahamika.
 
Kwasababu hatuwezi kutambua uwepo wa Mungu kwa milango yetu ya utambuzi si busara kupinga tu kuwa Mungu huyo hayupo.

Kinachofuata huwa ni kujaribu kutizama dhana ya uwepo wake imekaa vipi.

Hivyo bhasi Contradiction ni sababu mojawapo katika kukataa uwepo wa Mungu.

Kwasababu katika kumuelezea Mungu huyo hutoweza pasipo kujipinga kimantiki.

Na contradictions kuu huanzia hapa


Ila Unakubali kuwa huwezi kuthibitisha uwepo wa Mungu!?
 
Hata imani, kuna iliyo kweli na imani ya uongo, unatambua hilo.

Uwepo wa Mungu ni uongo au ni kweli!?
 
Sio muhimu kwa nini wewe una huo msimamo maana kila mmoja anaweza akawa na sababu yake ila tatizo ni msingi wa huo msimamo ndio kitu kisichofahamika.
Kwanini wewe unamsimamo wa kwamba Mungu yupo ili hali huwezi kumthibitisha!?

Je ni fear?
 
Umethibitisha nilichokisema kuwa contradiction sio sababu yenye kuwafanya atheists waseme hakuna Mungu.
Ukweli ni kwamba Mungu hayupo kwasababu hayupo tu.

Hivyo katika kutaka kujifunza zaidi, kuna muda huwa inabidi kufanya immanent critique katika dhana ya uwepo wa Mungu.

Katika kufanya zoezi hilo, logical consistency huwa haipo.
Na kitu cha uongo siku zote huwa kinajipinga chenyewe.

Kwahyo, suala la kuonekana kwa contradiction huwa linakuja baada ya kuchunguza dhana kwa mujibu wa mzungumzaji wa upande wa pili.

Ukikataa kwamba contradiction sio sababu ya kukataa uwepo wa Mungu inakuwa sio kweli, kwasababu licha ya kufanya busara kwa kufanya uchanganuzi kwa kuvaa dhana ya Mungu (Kwa mujibu wa waamini) bado unakuja kupata jibu kuwa Mungu huyo hayupo.

Kwasababu psychology ya waamini walio wengi hawawezi kukubali kufikiri nje ya kile wakiaminicho, hivyo hulazimu kuchambua dhana ya kile wakiaminicho wao (Immanent critique)

Sasa nijibu hapa pasipo ushabiki.
Wewe ukiambiwa kuwa John ni mwanaume bishoo na pia ni mwanamke mrembo sana utakubali?
 
Nakwambia hivi issue sio Mungu wa design ile bali ni huo msimamo wako wa kwamba hakuna kabisa Mungu, ndio maana katika hiyo contradiction kwako wewe inakupa jibu moja tu la kuwa Mungu hayupo na si vinginevyo.
Nikweli hayupo angekuepo asinge ruhusu contradiction kuwepo
 
Sasa ni bora mngesimamia hapo hapo kuwa hamuwezi kutambua uwepo wa Mungu kupitia milango ya utambuzi na tukajadili hilo maana ndio msimamo wenu, kuliko kuingia kwenye masuala ya contradictions ambapo ubaya wake mnajikuta mnalazimisha huo uwepo wa contradiction utoe jibu moja tu kuwa hakuna Mungu na si vinginevyo.

Kuna miungu mingi sana na katika yote hiyo hakuna hata mmoja mnayekubali uwepo wake na hiyo nadhani ni kwa sababu iliyoitaja kuwa hamuwezi kutambua uwepo wa mungu kupitia milango ya utambuzi.
 
Nitakuuliza John yupi unamzungumzia kwanza?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…