Mungu Yuko wapi?

Nikweli hayupo angekuepo asinge ruhusu contradiction kuwepo
Mbona kama unazungumzia kitu ambacho unajua kiliwahi kuwepo na sasa ndio hakipo? Maana ni sawa mimi niseme Magufuli angekuwepo asingeruhusu huu mkataba wa bandari kutokana na jinsi nilivyomjua huyo Magufuli.
 
Nitakuuliza John yupi unamzungumzia kwanza?
Mfano huo ni toshelezi na hauhitaji kitu cha kuongezea.

John unayeuliza kuwa ni yupi, ni huyo mwenye sifa ya kuwa mwanaume bishoo halafu ni mwanamke mrembo.
 
Mbona kama unazungumzia kitu ambacho unajua kiliwahi kuwepo na sasa ndio hakipo? Maana ni sawa mimi niseme Magufuli angekuwepo asingeruhusu huu mkataba wa bandari kutokana na jinsi nilivyomjua huyo Magufuli.
Hapo ni kwamba unataka kubadili mantiki katika framework anayotumia.

Anaposema kwamba Mungu huyo mwenye sifa ya uwezo wote ujuzi wote na upendo wote (ambae ndiyo anazungumzwa hapa) anayesimuliwa kila siku angelikuwepo kweli kusingelikiwa na utata katika dhana ya uwepo wake.

Ubaya wa contradiction hizo haziwezi kuondolewa na muumini yeyote labda tu abadilishe storyline nzima.

Ukikiri Mungu si wa upendo wote, si muweza wa yote ama si mjuzi wa yote atleast unakuwa umepunguza kitu,

Huyo Mungu hayupo, ukitaka kujua kwa hakika kama hayupo, jaribu kuthibitisha uwepo wake.
 
Hujanielewa nlichokwambia hapo juu.

Nmekwambia kwamba katika mjadala, kuna muda pia inabidi uzame ndani ya dhana kwa kuassume ni kweli, yaan unaassume ni postive tu walau ili kuielewa zaidi dhana hyo (immanent critique / kwa mujibu wa mzungumzaji)

Sasa hata tukiassume ni postive kuwa Mungu yupo(for the sake of mjadala)
Bado unaona contradiction hzo zenye kukuonesha Mungu huyo hayupo.

Hivyo huwezi kuondoa kuwa uwepo wa contradiction sio sababu ya kudhihirisha kutokuwepo kwa Mungu.

Ama hujui kuwa kuna logical proof?

Can you prove that God exists even in logical form?"
 
Wewe umetambua vipi kama kuna Mungu huyo anaexist kama huwezi hata kuthibitisha?
 
Mfano huo ni toshelezi na hauhitaji kitu cha kuongezea.

John unayeuliza kuwa ni yupi, ni huyo mwenye sifa ya kuwa mwanaume bishoo halafu ni mwanamke mrembo.
Kuna wanaume wamejigeuza wanawake.
 

Attachments

  • images (1).jpeg
    20.8 KB · Views: 5
Hilo ndio tatizo la kulazimisha kutumia hiyo unayoita contradiction kuhalalisha huo msimamo wako kuwa hakuna Mungu, wewe unaleta hoja ya contradiction na hapo hapo unatoa hitimisho la hiyo contradiction kuwa hakuna Mungu na hapo hapo unataka na uthibitishiwe uwepo wa Mungu.
 
Mtu anayesema kwamba naamini kuwa jua kesho litachomoza mashariki na kuzama maghribi,

hiyo ni imani ya kweli
Umetoa mfano wako binafsi pasina kutoa maelezo imani ya kweli ina sifa zipi maana kwa hapo mie sijaelewa bado.
 
Ingekuwa hivyo usingekuwa unatoa jibu moja tu la kuhitimisha kuwa hakuna Mungu kwa sababu ya hiyo contradiction, mara kadhaa nasema hili suala.
 
Wewe umetambua vipi kama kuna Mungu huyo anaexist kama huwezi hata kuthibitisha?
Kwanza ina maana kila tunachojua lazima kiwe na uthibitisho au kujua kumeaambatana na uthibitisho tu?
 
Kwa dhana ya kitu ambacho ni chenye ukweli, logical proof ni njia mojawapo ya kuthibitisha uhalali wa dhana hiyo

Mimi nakutaka uthibitishe tu kwa logic.
Weka logical consistency kwenye dhana ya uwepo wa Mungu, ukifanikiwa kwenye hilo utakuwa umeproof.

Je waweza kufanya hivyo!?
 
Umetoa mfano wako binafsi pasina kutoa maelezo imani ya kweli ina sifa zipi maana kwa hapo mie sijaelewa bado.
Imani ya kweli siku zote inajengwa na facts + logical consistency.

Jua kuchomoza Mashariki na kuzama Magharibi kila siku, hata kama kesho haijafika mtu anaweza kuamini hivi kwasababu imani yake inakuwa imejengwa na fact kwamba siku zote za nyuma jua limekuwa na tabia hiyo ya kuchomoza Mashariki na kuzama magharibi,

Hapo kuna facts hapo hapo logic tu haijawahi kujipinga na imetulia

Je waweza kuonesha facts ama kutokujipinga kimantiki katika dhana ya uwepo wa Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…