Mungu yupo, fikiria kuhusu mambo haya, usiseme hakuna ushahidi

Mungu yupo, fikiria kuhusu mambo haya, usiseme hakuna ushahidi

hermanthegreat

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,274
Reaction score
3,282
Hello wanaJF,

Nimepata thread ama post nyingi Sana zikihofia kuhusu uwepo wa Mungu. Unapozidi kujifunza na kufahamu zaidi sayansi tunategemea uwe shuhuda mkubwa kuhusu uwepo wa Mungu lakini unexpectedly ndio unaanza kusema sayansi haiamini Mungu yupo.

Ona hizi facts za kisayansi
👉. 1..MCHAKATO WA UTENGENEZAJI WA PROTEIN KWENYE MWILI (protein synthesis)
Mchakato huu ni wa kushangaza kidogo kwani Kuna enzymes zinazofanya kazi Kama Zina akili Kama Mtu .
Kuna enzymes inaitwa helicase ambayo inachana Kati Kati DNA kwenye strand mbili ili kuanza mchakato.
Kisha Kuna enzyme inaitwa polymerase 3 ambayo inatengeneza RNA kutoka kwenye moja ya hizo strand. Yote haya yanatokea kwenye nucleus ya seli.

Kisha RNA ambayo ni messenger RNA inatengenezwa kwenye nucleus kutoka kwenye moja ya strand inatoka kwenye nucleus ikiwa imebeba taarifa kwa mfumo wa Code.

Enzyme inayoitwa Ligase inaishona DNA iliyo kwisha chanwa na Helicase.

Taarifa zikiwa zimebebwa na mRNA kwa mfumo wa code zinapelekwa kwenye Ribosomes RNA ambayo imo kwenye cytoplasm ili kutafsriwa ieleweke Kama mtoto anayepatina awe na kichwa kikubwa, mweupe mnene nk.

Kisha RNA nyingine inayoitwa Transfer RNA inabeba amino acid inazipeleka kwenye Ribosomes kutengeneza amino acid ikiifikikisha tu inaondoka na kurudia nyingine Hadi chain ndefu hatimaye protein inakunjwa kunjwa na kuwekwa kwenye golg apparatus.

Mambo haya hayatokei automatically lazima kutakuwa Kuna mzee wa siku anayasimamia kwani mchakato huu haukosei hata kidogo na Kama ikitokea makosa Kuna enzymes zinahusika na kufanya proofreading and repairing au correcting. Kuna Mungu Lazima

2. UPATIKANAJI WA MWANADAMU
Hebu FIKIRIA kutoka kwenye seli yenye mkia na kichwa Hadi kiumbe chenye mifupa na damu na mifumo inayofanya kazi bila kukosea, yaani mfumo wa upumuaji, mfumo wa mmengenyo wa chakula , Neva , na kadhalika.

Kuna watu wanasema MWANADAMU ni matokeo ya BIG BUM yaani Kama ka mlipuko tu kichwa , macho na masikio vikajiweka ghafla, however not kwanini basi macho yasiwe kiunoni au mikono iwe tumboni , lazima kutakuwa na fundi wa haya naye ni MUNGU.

3. MAAJABU YA ANGA NA SAYARI ZOTE
SAYARI zimepangiliwa kulinguka jua na zinavutana kwa nguvu ya asili inayozifanya zisianguke , sayansi iliyotumika kulitandaza ANGA hili haichunguziki ni ajabu mno , lazima Kuna Mungu nyuma ya haya.

4. MAAJABU YA NDEGE WANAOSAFIRI BARA MOJA HADI JINGINE
Pacific golden plover ni ndege wenye uwezo wa kusafiri umbali mrefu zaidi ndege Hawa hula chakula sawa na umbali wanakoelekea yaani hawapelezi ni Kama gari ambalo lazima lijaze mafuta kiasi Fulani ili kukamilisha safari, ni nani anayewaelekeza kula mlo huo?

Mungu Lazima atajwe hapa lakini uliwahi kujiuliza kwanini ndege Wanaotembea kwenye makundi huwa wanapaa kwa kutengeneza umbo la V , au U?, wanafanya hivi ili kupunguza kiasi Cha nishati au nguvu wanayotumia , wamejuaje kua wanaweza ku minimize energy consumption kwa kutengeneza V shape? FIKIRIA.

5 . UWEPO WA UCHAWI NA MAPEPO
Tumeshuhudia watu wakirogwa , Uchawi upo amini Kama unabisha unaweza anzia utafiti wako makaburini nyakati za usiku. Amini nakwambia Kuna ulimwengu wa giza unaishije ambao sisi hatuuoni. Hii ipo wazi , Kama unaamini Kuna shetani basi lazimi Kuna Mungu.


Note: Akili ya Mungu haichunguziki.

Unakaribishwa pia kuongezea facts za kisayansi 👇👇
 
Mungu ni kichaka cha watu kujificha pindi wanapoishiwa maarifa.

Usipoweza kujibu swali, huo ni ushahidi wa kutokujua tu.
Haimaanishi kivyovyote vile kuwa lazima kuna Mungu.

Hivyo bhasi yatupata kutafuta majibu yaliyo sahihi kuliko kujificha kwenye dhana ya Mungu.

Note : Akili ya Mungu haichunguziki.
Unakaribishwa pia kuongezea facts za kisayansi
Akili ya Mungu haichunguziki kwasababu hayupo.

Unawezaje kuchunguza kisichopo!?
 
Mungu ni kichaka cha watu kujificha pindi wanapoishiwa maarifa.

Usipoweza kujibu swali, huo ni ushahidi wa kutokujua tu...
Nina uhakika hujasoma na kuelewa vizuri nilichokiandika
 
Sayari hazizunguki dunia kama ulivyosema,sayari yetu(dunia) ni moja kati ya sayari ndogo kwenye Milk way galaxy achilia mbali ulimwengu wote.

Kuitoa Dunia kwenye ulimwengu ni sawa na kutoa punje moja ya mchanga ufukweni.

Halafu theory ya asili ya ulimwengu inaitwa Big Bang sio Big Bum.

Kuhusu hoja yako kuu ya uwepo wa Mungu nakubaliana na wewe katika imani kwamba Mungu yupo japo siwezi kuthibitisha.
 
Hapa Kuna ka mechanism kabisa mkuu , kama una mda waweza search Google ukajifunza zaidi kwa manufaa yako.
 
Uchawi na mapepo viko wapi? Nataka kurogwa.

Anyway, mungu hayupo ni hadithi tu za alinacha. Uchawi haupo.
Nimeelezea vizuri hapo nimesema Kama huamini kuhusu uchawi na mapepo unaweza anza utafiti wako kwa kutembelea maneno ya makabulini nyakati za usiku kwani huko zinaishi roho za watu na mizimu Yao, Kisha nenda vijijini ulizia eneo lipi Lina uchawi nendapo usiku kajihakikishie. Yakikupata na ukijikuta uko hatarini kumbuku kumuomba Mungu kwani ndiye pekee atayekuwa msaada wako
 
Nimeelezea vizuri hapo nimesema Kama huamini kuhusu uchawi na mapepo unaweza anza utafiti wako kwa kutembelea maneno ya makabulini nyakati za usiku kwani huko zinaishi roho za watu na mizimu Yao, Kisha nenda vijijini ulizia eneo lipi Lina uchawi nendapo usiku kajihakikishie. Yakikupata na ukijikuta uko hatarini kumbuku kumuomba Mungu kwani ndiye pekee atayekuwa msaada wako
Hizo ni hadithi tu za alinacha. Hakuna kitu kama hicho.
 
Kuna msemo unasema Mungu achunguziki
Ni pale ambapo unajaribu kuchunguza mambo yalivyosukwa na vile yanavyoenda na unajaribu kupata jibu ni akili gani iliunda hiyo mifumo na usione namna unavyoweza kuipima

Waza kuhusu bahari na vurugu zake
Waza kuhusu magalax yote ili ukute icho kibahari ni kama tu kidutu flani hivi
Mambo ni mengi
 
Back
Top Bottom