Mungu Yupo: Majibu kwa Wasioamini

Status
Not open for further replies.
Unachekesha kweli wewe!
Eti mwanadamu awe na maarifa Zaidi ya Mungu!
Eti unatoa na mifano Kama hiyo?!

Hebu toa ya kwako tuone! Sioni kabisa nafasi ya mungu katika maisha ya kila siku, ni sawa na kuweka chakula mezani halafu mnaanza kutoa shukrani kwa Mungu, mnasahau kuwa hustle zenu ndiyo zinaleta ubwabwa huo, ukiwa kwangu mke wangu aweke ugali mezani uanze kushukuru mungu mbona itabidi usiumege hata huo ugali, mshukuru mke wangu kwa kupika!
 

Unaona unavozidi kuvuruga!?
 

Swali hilo hapo juu halijapewa jibu.

Swali haliwezi kuwa imani, kwa sababu ni swali, linangoja jibu.

Halijajibiwa, nimeona ubabaishaji tu.

Kama vile, mungu karuhusu maovu ili wanadamu wawe na uchaguzi, kwa sababu mungu anapenda sana uchaguzi huru, hataki kulazimisha watu kufanya kama anavyotaka.

Nikauliza, kama mungu anapenda uchaguzi huru, na hapendi kulazimisha, mbona mimi sijapewa uchaguzi niamue nizaliwe au nisizaliwe?

Sijapata jibu mpaka sasa.

Huo ubabaishaji mnaouita majibu, unazaa maswali zaidi ambayo hamjayajibu
 
Hilo swali mbona ameshaliuliza na akapewa majibu kwenye ile thread nyingine, wewe nadhani umedandia tu, kachungulie kule usome kwanza ndiyo uje huku, wenzio wamekimbia uzi kule walivyoona reasoning kwao imeshindikana!

busara ya kawaida hata kama sio wewe uliyejibu,badala ya kuandika sentensi yote hiyo, ungenonyesha hilo jibu, huo ni ubabaishaji,huwezi kuwa swali hilo limejibiwa kwenye uzi fulani, wewe toa jibu,yawezakuwa hata unayoyauliza wewe kuna wakati yameweza jibiwa,kwa kuwa wewe sie wa kwanza kumchukia Mungu,Mungu amekuwa anachukiwa tangu enzi,na maswali unayouliza wewe si mapya sawa na ninayo kuuliza mimi na wengine,hakuna aliyevumbua swali jipya,sana sana tunaongezea maelezo kwa kuwa tunajua kuna vichwa ambao wao kuelewa ni kichina zao kunukuu kama ndege kasuku.
Toa jibu la hilo swali, nimepitia uzi nyingi nimeona kama sio H1N1 ni Eiyer ama Jingalafalsafa wameuliza kuhusu akili na kuomba ushahidi,ninacho kiona ni maelezo ya swali limejibiwa bila kuonyesha jibu lilipo.
kukata mzizi wa fitna jibu sasa na uoneshe ushahidi wa wazi kwamba wewe na wachukia mungu wenzako mnazo AKILI na Muweke ushahidi niusome kwenye uzi huu. Stop bla bla
 

Haya ni mawazo ya mtoto wa darasa la tatu...JF kama kokoroo
 

Kusubiri ushajidi WA wao kuwa na akili utazeeka utakufa zaidi sana watakwambia hilo limekwisha uibiwa... Wakijibu wanajua watakuwa wanadharirisha imani yao.
 

Haya kaka mkubwa, naona mjani umepanda kichwani. "Akili ni uwezo wa mwanadamu kujifunza ujuzi na maarifa, na kuweza kuvitumia kutatua changamoto iliyo mbele yake!" Kwa maana hiyo basi kama wewe una akili timamu unaweza kuona mtu atumiaye maarifa katika kutatua changamoto kama ana akili. Mfano, ukimpa mwanao hesabu nyumbani ukamwambia asolve 2x4 akaanza kuhesabu vidole ujue hiyo ni evidence ya akili!
'
 
Kila mjadala huwa una mwisho wake, na kwangu mimi naona inatosha. Lengo langu limetimia kwa asilimia zote.
Ya kuwa Wasioamini uwwepo wa Mungu wanafanya hivyo kwa sababu za kiimani na sio kisayansi au kimatiki. Ya kuwa Imani katika Mungu wa Biblia ndio pekee "reasonable" na kuwa wakana Mungu na dini yao sio tu wako kinyume na sayansi, bali pia wako kinyume na Mantiki na hata fikra za kawaida.

Lengo limetimia kwa kuwa waliokuwa wakisombwa na mafundisho ya dini hii potofu ya Hakuna Mungu hata wakadhani ndio sayansi wameujua ukweli kuwa ni dini ambayo inapingana na sayansi na mantiki. Kipekee niwashukuru wote mliosoma na mliochangia, hasa Kiranga na wafuasi wote wa dini hii kongwe kabisa kwa kunisaidia kuthibitisha madai yangu pasipo na shaka. pia niwashukuru wote mliojadili kwa kuheshimiana na kwa staha.

Sijafunga mjadala huu (utaendelea kuwepo mpaka utakapoacha kuwepo) lakini kwa kuwa kusudi langu limetimia ninatundika daluga. Nitakuwa nikipita na pengine kujibu hapa na pale lakini sio kwa kiasi cha kwanza. Kama kuna boiling issue nai miss, fanya wema kuni mention 🙂

Kwa mnaoamini Mungu wa biblia, imani yenu ni solid and reasonable, ishikilieni. Kwa msioamini Mungu naomba niwaache na zawadi hii hapa chini.


Mungu awabariki na mjadala uendelee
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…