Kama complexity ni lazima iumbwe, complexity kubwa inayoumba complexity ndogo nayo ni lazima iumbwe.
Huwezi kusema kiti ni lazima kiumbwe, halafu mwanadamu aliyekiumba kiti awe hajaumbwa sawa?
Same argument.
Mfanye mwanadamu awe kama kiti, na muumbaji wake awe mungu.
Huwezi kusema mwanadamu ni lazima awe ameumbwa, halafu muumbaji wake awe hajaumbwa.
Kama complexity ndogo kama mwanadamu ni lazima iwe imeumbwa, kwa sababu complexity haiwezi kutokea yenyewe bila kuumbwa, basi complexity kubwa zaidi, mungu, ni lazima zaidi iwe imeumbwa.
Kwa hiyo ukishikilia kwamba mwanadamu ni lazima awe ameumbwa, kwa kuwa hawezi kutokea hivi hivi tu, unachoandika bila kujijua ni kwamba mungu naye ni lazima awe ameumbwa. Ndiyo line ya logic ya argument yako.
Of course unaweza kuchomeka any arbitrary "deus ex machina" hapo kati kujitoa katika kamba uliyojifunga wewe mwenyewe. But that would be illogical.
Mungu wenu haelezeki logically.
Kwa sababu hayupo.
Kama yupo toa ushahidi.