Ushawahi kusikia kitu kinaitwa "immanent critique" maishani mwako?
Soma zaidi hapa
Immanent critique - Wikipedia, the free encyclopedia
Lete majibu ya hoja husika badala ya link. Kwa mtu unayedai kufanya mambo kwa fikra siktarajii link bali majibu mujarabu. Link waachie wengine.
Kifupi, mimi kama sikubali kuna mungu, na wewe kama unasema kuna mungu, tukibishana wote kwa kusimamia pande zetu, hatutapata hata pa kuanzia.
Mimi nina pa kuanzia wewe huna. Mimi naanza na Mungu na kutoka hapo napata Mantiki kwa sababu nimeumbwa kwa mfano wa Mungu mwenye mantiki. Napata sheria za kimaadili (Moral laws) kwa sababu nimeumbwa kwa mfanow wa Mungu aliye chanzo cha sheria hizo. Ninatumia sayansi kwa sababu Mungu ameweka uniformity na kufanya sayansi iwezekane.
Wewe unaelea tu. Huna pa kusimamia. Una argue kwa kutumia logic, lakini huna sababu kwa nini utumie logic. Unajaribu kumkosoa Mungu kuwa ana makosa ya kimaadili bila kutuambia unapataje maadili katika dini yako ya hakuna Mungu. Unaongea sana kuhusu sayansi lakini katika dini yako ya hakuna Mungu unapataje sayansi?
Inabidi uibe kutoka kwa Mungu unayemkana... What a proof for God's existence!
Sasa kinachofanyika hapo, mimi naachana na position yangu ya kutokubali kwamba mungu yupo, kwa muda tu, ili kuangalia upande wako na mjadala uendelee.
Nasema, OK, tuseme mungu yupo, na ni mwenye ujuzi wote, na uwezo wote, na upendo wote. Tukubaliane kwamba hili ni kweli.
No hii sio mechi wala sio majaribio. Ni kitu kiko halisi na kina madhara kukubali au kukataa.
Kwa hiyo sioni haja ya kuhangaika na majaribio yako. Ni aidha unakataa au unakubali. Na ukikataa, ishi consistent na dini yako ya hakuna Mungu. Hiyo ndiyo maanaya kuwa na utashi!
Hii inafanya maswali yako yawe meaningless!
Swali linakuja tukishakubaliana hivyo.
Kama mungu yupo, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye uwezo wote, na ni mwenye upendo wote.
Kwa nini karuhusu iwezekane kuzaliwa watoto vilema?
Hii ni hesabu ya ku solve for x, ambapo katika ku solve for x, unafanya let x be y, halafu jibu utakalopata la x unaweza kuli verify.
Kwa sababu dini yake imeshindwa kutoa hata tafsiri ya uovu umeamua kuhamia kwa Mungu kwa muda?
No free lunch. Aidha unamkataa au unamkubali... nukta!
Naona somo zima la "immanent critique" limekupitia mbali.
Wala hata sio la muhimu kama unavyodhani!
Mtu anaposema "let's say god exists, for the sake of carrying the ergument and analysis forward" hamaanishi kusema kwamba kakubali kwamba mungu yupo.
And that makes whole thing silly!
Kuna njia nyingi tu. Unaweza kuanza kwa kusema kwamba yale yote ambayo sipendi kutendewa ni mabaya, na yale yote ambayo napenda kutendewa ni mazuri. Hapo hujamhitaji mungu.
Lets see!
Kwa mfano, mimi sipendi kuuawa, kwa hiyo hili ni baya kwangu, sipendi kufanyiwa, na sitaki kumfanyia mwingine.
Hitler aliua watu million 6+ kwake lilikuwa Jema. Stallin, Mao na wengineo wakaua mamilion. Wao waliona sawa ni mema. Je unakubaliana nao kuwa walifanya mema. Au unadhani mabaya?
Pia mimi napenda zawadi za Swiss watches, kwa hiyo hili ni jema, mtu akinifanyia nitapenda na mimi nitapenda kumpa mwingine.
Kwa wale wanaojisikia fahari kubaka watoto wadogo nao vipi wako sahihi? Wanafanya mema au mabaya?
Kipimo chako cha mema na mabaya ni nini? Nataka kujua mizani unayotumia!
Hapo tayari tushaona mema na mabaya ambayo hayamtegemei mungu.
Fallacy! Sio kweli, hatujaona popote!
Hebu ona hapa wanajadili "secular morality" ambayo haimuhitaji mungu
Secular morality - Wikipedia, the free encyclopedia
Hamna kitu hapo! Huwezi kuwa na morality bila kuwa na Moral laws and laws never pop from nothing. They demand Law giver.
Kiranga whay can't you get it...soo simple!
Kwa hiyo kufikiri hakuna wema na ubaya nje ya mungu ni makosa, ni kama samaki kufikiria hakuna dunia isiyo na maji. Just because wewe umegubikwa katika bahari ya dini inayomtegemea mungu kwa kila kitu hilo halimaanishi hakuna watu wenye moral standards bila kumtegemea mungu
This explanation fits you well. Dini yako ya hakuna Mungu imekufanya udhani kuwa kweli hakuna na kuwa "yote yawezekana kwake aaminiye hakuna Mungu".
Msome Albert Einstein hapa
Einstein kakusaidia hapo jinsi ya kupata moral code ambayo haimtegemei mungu.
Hizo ni assertion za Einstein. Hajatuambia ni jinsi gani elimu inatupa Moral law wala jinsi social ties zinavyolete Moral law na hivyo ni empty assertion.
Unakataa kuamini Mungu ambaye ameumba braini ya Einstein lakini unashindwa hata kuhoji upumbavu wa Einstein.
Sijui kama unapata picha ni kiasi gani dini yako hii imekupiga upofu!
Huu uongo wa "mungu ameacha mabaya kwa kuwa anapenda uhuru wa kuchagua" nilisha u debunk.
Hii ngano mbona haipo katika maneno uliyonukuu. Umeitoa wapi?
Kama mungu anapenda kuchagua mbona hajanipa uchaguzi wa kuamua nizaliwe katika dunia ya namna gani, nchi gani, kwa wazazi gani, niwe na genes gani etc? Mbona nimejikuta nimezaliwa tu? Huyu ni mungu anayependa tuwe na uhuru wa kuchagua kweli?
Kama anapenda sana uchaguzi, mbona hakunipa mimi uchaguzi wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe?
Kwanza jua Mungu ninayemwongelea sio mdoli wala mtumwa. Ni Mungu mwenye mamlaka ya kuamua, Alipoamua kuumba kwa mfano wake hakuomba ushauri. Kwa hiyo Mungu hakuumba mungu mwingine bali mwanadamu aliyebeba mfano wake. Kama mwanadamu na yeye akiwa Mungu kuna limits. Na moja ya limits ndio hizo.
Huna namna. Kama ambavyo utakufa na hna cha kufanya na hilo ni vivyo hivyo
Sasa mungu kaumba ulimwengu ambao anajua una maasi, na anajua kaumba wanadamu na udhaifu, makusudi, na kawawekea majaribu, na kajua kabisa wataasi, na kwa sababu kajua wataasi, na hawezi kukosea, hawawezi kuepuka kuasi.
Kwa maneno mengine kashawapangia kuasi.
Straw man argument!
Umetengeneza mungu bandia halafu umemdili sawasawa lol
🙂
Hayo yote Mungu wangu hajawahi kuyafanya! Get facts straight!
Wakiasi atawalaumu?
Atawachoma moto kama wafanya dhambi? Wakati yeye mwenyewe ndiye aliyefanya kila jitihada kuhakikisha wanaasi? Kaumba ulimwengu ambao uasi unawezekana, isitoshe kaweka vishawishi, isitoshe kawaumba binadamu dhaifu. Binadamu wakiasi kosa ni la nani? Binadamu au mungu?
Hapana.
Ukiwa software designer tu, halafu una uwezo wa kutengeneza software ya computer isiyo crash, lakini ukaamua tu kutengeneza software inferior inayocrash, unaweza kufukuzwa kazi. Hii ni standard ya kibinadamu tu.
Kwa nini mungu mwenye uwezo zaidi (mkuu) na ujuzi zaidi (mkuu) na upendo zaidi (mkuu) tumuwekee lower standards?
False premises, false conclusion!
Uwezo wa mwanadamu kumuasi mungu mwanadamu aliutoa wapi? Mungu alipoumba ulimwengu kwa nini aliruhusu uasi uwezekanike? Kama mungu kaumba ulimwengu na kuweka parameters zote, kwa nini aliruhusu parameters za ubaya kuwezekana?
Unapata shida kwa kuwa hutaki kukubali ukweli kuwa "Hapo Mwanzo Mungu..."
Tatizo ni dini yako ya hakuna Mungu...vinginevyo ni swali rahisi tu. Mungu aliumba mtu kwa mfano wake akiwa na uwezo wa kuchagua.... kutii au kuasi. God of Love made men with choice.
Huwezi kuelewa hili usipotaka kutoka huko gizani uliko aisee!
Usiniambie kwa sababu alitaka mwanadamu awe na chaguo, kwa sababu mimi hakunipa chaguo nizaliwe au nisizaliwe, na nizaliwe wapi, vipi, niishije etc. Huyu si mungu anayependa viumbe wake wawe na chaguo
Utasema hakukupa chaguo kwa kuwa hakukuruhusu ukalie kiti cha Mamlaka yake ya Uungu... silly argument!
Uwezo wa mwanadamu kutumia vibaya utashi wake umeumbwa na nani? Na kwa nini uliumbwa?
Mimi mbona sikupewa uweza wa kuchagua nizaliwe au nisizaliwe? Katika tendo moja la kujamiiana kuna viini kama milioni mia mbili na nusu vinakufa ili kimoja tu kifanikiwe, kama mungu anapenda uchaguzi sana, mbona hivi vingine hajavipa uchaguzi wa kuishi?
Mbona mimi sijapewa uchaguzi kuamua nizaliwe au nisizaliwe? Na nizaliwe vipi? sehemu gani etc? Kama mungu kutoa uchaguzi ni upendo, sisi ambao hatujapata option kuchagua hatupendi.
Alishindwa kuyazuia?
Kama si sahihi kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao hili linawezekana?
Maswali haya nimejibu kitambo ila unayaleta kwa staili tofauti essentially ni yaleyale!
Na lengo lako ni kuondoka katka hoja za msingi ambazo so far hujajibu hata moja.
Kiranga huwezi kutetea kitu ambacho kinapingana na mantiki, sayansi na hata akili ya kawada tu!
Utaishia kufanya vituko unavyofanya hapa!
Nani kakwambia naamini dini ya random and chance?
Mwanadamu alifikaje hapa alipo? Ulimwengu ulifikaje hapa ulipo?
Unaamini evolution ni ukweli au uongo?
Ushaoneshwa hapo juu kwamba huhitaji mungu kuwa na mema na mabaya. Wewe hujaweza kutuambia kama mungu mwenye uwezo wote na ujuzi wote na upendo wote kauumba ulimwengu huu, mbona ulimwengu una maovu mengi sana?
Zaidi ya taralila za Einstein na visasili vya "secular ethics" hujaleta chochote cha maana.
Kwa nini mungu alimuumba Hitler na kuruhusu haya mauaji? Ina maana alishindwa kuyazuia? Kama hakushindwa kwa nini hakuyazuia? Alipendezwa nayo?
Nimeuliza swali kwako usiyeamini Mungu. Huwezi kujibu ukiwa na imani ya dini yako ya hakuna Mungu.
Ili ujaribu hata kujibu lazima ukubali uwepo wa Mungu kwanza.
Ukweli mchungu ni kwamba hujajibu swali jepesi tu la "the problem of evil".
How does evil exists in religion of no morality like atheism? Its silly to even say the word!
Kifupi hujajibu hoja hata moja katika zote ambazo nimezileta. na hii kama nilivyosema mwanzo ni kwa sababu tamko la imani la dini yenu ya hakuna Mungu haliwaruhusu na mnakuwa force kujibu bila mantinki.
Kiukweli sijawahi kuona mkana Mungu yeyote akiishi sawia na dini yakehiyo. Wote ninaowafahamu wanaishi na Christian Morals za Mungu wanaye profess kumkataa! Strange!