Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Shida hapa ni kwamba serikali ikiwaondoa tu,

Vyama vya upinzani vitawatumia watu hawa kuomba kura watawaambia kuwa watawaruhusu kufanya watakalo kwenye stendi hiyo.

Kwahiyo mpaka tutakapo jifunza siasa zenye tija ndipo tutakapo pata tunachokitaka.
 
Labda miradi ya kinyesi, kama neno lenyewe kujiajiri limekushinda kuandika sembuse kujilipa 80k
Nilichelewa Kusoma hii post yako Ndugu. Nimecheka hadi Kuanguka katika Kiti changu. Kuna Watu (JF Members) hapa mna Majibu ya Shombo mno. Umenivunja Mbavu!!!
 
Ficha ujinga wako
 
Inabidi hata wapiga debe waruhusiwe kuingia ndani na pembezoni mwa Hiyo stand maana ndio shughuli yao inayowaingizia kipato. Wasafiri wataibiwa kwa Sana.
 
Inabidi hata wapiga debe waruhusiwe kuingia ndani na pembezoni mwa Hiyo stand,maana ndo shughuli yao inayowaingizia kipato.Wasafiri wataibiwa kwa Sana.
Kupiga Debe ni Ajira rasmi nchini Tanzania? Kuibiwa kwa Wasafiri hapo Stendi ndiyo Fursa ya Kiuchumi ( Kimaisha ) kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini hapo Stendi Mpya Mbezi? Kuna Vitu Vinakera mno na havivumiliki kama kweli Kichwani mwako kuna Akili za Kutosha na Uwerevu usio na Shaka.
 
Sitendi sio sehemu ya biashara..ni sehemu ya usafiri. Hebu tusichanganye mada hapa..kule ni sehemu pekee ya kupata usafiri..kuuza na kununua ni MADUKANI na sio standi..nani aliye tuloga? Nani kasema msafiri lazima anunue kitu standi....mbona uwanja wa ndege hatununui wala kula kwa mama lishe??
 
Kama hakuna utaratibu hao wamachinga wanaingiaje stand?
Au kwako utaratibu ni kuona wamachinga hawaruhusiwi kuingia stand🤔🤔🤔🤔
Wanaingia bila utaratibu na kufanya biashara bila utaratibu. Unajua kidogo Mipango miji? Hakuna anayewachukia, tunachukia pale utaalamu umapozidiwa na wanasiasa. Hivi pale Congo kkoo kituo cha basi kimevamiwa na machinga hakuna tena pakrking ya daladala, njia za watembea kwa miguu kkoo ni majiko ta supu, na mamalishe, msongamano usiokuwa na sababu wakati tuna watu wa mipango miji, maafisa biashara n.k si AIBU hii.
 
Mnataka mbaki wachache wenye biashara hapo mtukandamize na bei zenu acha wanyonge wanaosafiri wahudumiwe na wanyonge wenzao
 
Ona haoo acha niwaweke na ushahidi hao wazee wa kuzungumzia mambo bila kujua uhalisia wowote
mama D

Ova
View attachment 1715371
Shauri yenu..mtaishia hadi kuuziwa mayai vinza ndo akili labda zitawarudia . hahahahaaaa.. jamani kila kitu ni bora kiwe ' terms and conditions' otherwise itakuwa vurugu tu..na ustaarabu na mipangilio makini na sheria kufuatwa ndo maendeleo yatakuwepo.
 
Zamani mtu akikuita mnyonge, ni tusi, ila awamu hii imelifanya kuwa ni sifa!!na ZUZU kuitwa mnyonge anajisikia rahaaa!!!
Si afadhali hata neno mnyonge kidogo lina heshima. Mtu anaitwa masikini..mlala hoi anashangilia na kupiga makofi. Jamani ni Upogo gani huu?? Mmesahau maneno matakatifu ya Mungu yakisema ...."Mungu hafanyi maagizo na Masikini?" Sasa vipi wanasiasa wanawaita masiki na mnashangilia...?? Wanyonge ..amina bwana..amakweli tumekuwa matutusa..sikamakwamba nawatusi..lahasha..mwajitusi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…