Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Muonekano mzuri wa Stendi mpya ya Mbezi umeharibiwa na Siasa zetu za kutafuta sifa kwa Wanyonge waliobatizwa Masikini

Pale utauziwa mikate ndani.....nenda tu mfano kwenye coater za Turiani.....utaleetewa mpaka chips take away. Labda kama wewe huwa unapita kwa ndega.
Kuna mwenye hotel ameingia mkataba na manispaa mle ndani. Ili aweze kutumiza marejesho ni pamoja na kuhodhi biashara za ndani.

Ukiona wameingia wachache ni njaa ya mgambo, kila mtu anakula ofisini kwake
 
Kama muonekano ule mzuri kuanzia Jengo zima na mandhari ya pale leo hii umeanza Kuharibiwa kwa Wanasiasa wetu Wanafiki wanaocheza na Uelewa mbovu wa baadhi ya Watanzania uliochanganyika na Ushamba wao kwa Kuwaruhusu hadi Wamachinga, Mama Lishe na Vibaka wajazane mule ndani Stendi hadi kuleta Kero naomba waruhusiwe pia kwenda pale JNIA Terminal III haraka sana.

Kama kweli Wanasiasa wetu nchini Tanzania wanawapenda kweli kweli Watu (Wananchi) wao hasa Masikini ( Walalahoi ) basi wasiishie tu kutafuta Sifa za Kiumaarufu kwa Kuwaruhusu waingie ndani kabisa ya Stendi mpya ya Mbezi Kufanya Biashara zao bali wawaruhusu pia kuingia JNIA Terminal III, KIA na kama kweli tunawapenda basi waruhusiwe kuingia hadi Ikulu Magogoni na Chamwino.

Inakera!
Kuruhusiwa kufanya biashara ni jambo Moja na kupangiwa utaratibu wa kufanya biashara ni jambo jingine kabisa...

Ni jukumu la uongozi wa Mbezi Luis Bus Terminal kuwatengenezea utaratibu wa namna ya kufanya biashara ili kulinda hadhi ya MLBT
 
Umefanikiwa kufika pale ukauona utaratibu?
Km ulikua hujui pale kuna Uhuru bila utaratibu mambo ni vagalanti...viongozi wote wanawaogopa wamachinga.
Kama hakuna utaratibu hao wamachinga wanaingiaje stand?
Au kwako utaratibu ni kuona wamachinga hawaruhusiwi kuingia stand🤔🤔🤔🤔
 
Hivi kwann masikini wanajiona wao nd watu kuliko matajiri yani wanataka shari muda wote, walalamishi muda wote. Mi nawaambia nyny masikini acheni ubaguzi wa kishamba unaoletwa na chuki na wivu. Mnamuona bakhresa kinyago anawalipia kodi kubwa sana ila mnachafua mazingira ambayo mwenzenu anaishi, Mo anaishi, akina GSM na wengineo wengi. Wanawapa ulaji kwa ajira ambayo serikalini hamuezi pata wanawalipia na kodi. Kwann hamtaki kufuata utaratibu kwann serikali ikitaka kuwapa maeneo mnakuwa na vinyongo? Hatuwezi kuwa na nchi isiyo staarabika miaka yote kiasi hichi. Niwaulize swali nyi ni akina nani hasa? Umuhimu dhidi ya matajiri ni upi hasa? Matajiri wamewafanya muwe masikini? Badilikeni mkipewa maeneo basi muwe waelewa sio ulalamishi wa uongo uongo 2. Mnawapa presha viongozi wanafanya kazi bila weledi 100% maan hakuna anaependa kuzomewa hovyo.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo wakienda uwanja wa ndege watageuka kuwa mbuzi? tuache ushamba tujadili hoja, jamaa katoa hoja tuna takiwa tumjibu kwa hoja na siyo matusi ya kijinga
Bongo tunatengeneza kitu cha ajabu sana kinaeza leta madhara baadae kwa kuwalea hawa masikini wafanye watakavyo. Ipo siku matajiri watasema basi na kwa nguvu zao kitatokea nn sijui. Umeona kama anavyojibu huyo ni chuki za wazi.

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Kuna mwenye hotel ameingia mkataba na manispaa mle ndani. Ili aweze kutumiza marejesho ni pamoja na kuhodhi biashara za ndani.

Ukiona wameingia wachache ni njaa ya mgambo, kila mtu anakula ofisini kwake
Sawa......nimekuelewa mkuu.
 
Ofsi sio sehemu inafanyika biashara

Stend ni sehemu ya watu kufanya biashara, ni haki ya kila mtu kufanya biashara, stend ni ya Watanzania wote maskini na tajiri, kama unaona huo ni uchafuzi na unakuboa, Jenga stend yako ama boresha nyumbani kwako pakuvutie ili uvinjali zaidi
Kwani uwanja wa ndege siyo eneo la umma na masikini? mpuuzi wewe acha kulea ujinga
 
Punguza stress ndugu yangu!

Punguza chuki zako dhidi ya serikali na wananchi wanaoipenda au kuifurahia serikali yao.
Punguza hasira na wamachinga,mamalishe na wengine wanaopambana kupata tonge.

Pita nchi nzima,machinga na mama ntilie biashara zao wanafanya stendi ama pembezoni mwa barabara....ama mahali popote penye shughuli zinazofanya watu kupatikana kwa wingi...mfano viwandani na maeneo yanapopatika wanachuo au hata ndani ya fensi za baadhi ya shule za msingi na sekondari.

Ni upumbavu kutaka watu waruhusiwe kufanya shughuli hizo kwenye viwanja vya ndege au ikulu. Na pia,natiliashaka uelewa wako wa mambo. Jaribu kuwa na akili ya ziada kwenye kupambanua mambo.

ACHA HASIRA NA CHUKI.
Akili yako ni ya Kihayawani ( Kipumbavu ) kama ya huyo ( huyu ) Mwanasiasa unayemtetea hapa. Wenye Upeo mkubwa tulishawadharau Kitambo.
 
Umenikubusha mbali tulipokuwa tunachanganyika skuli kuna kabila lilikuwa linapanda juu ya vyoo vya kukaa tulikuwa tunapata tabu sana mpaka walipo elewa matumizi ya vyoo hivyo hivyo kwenye hili tutaelewana baada ya hasara
Ndugu kwa hili huwasemi Watani zangu Waha na Wahaya?
 
Back
Top Bottom