SI KWELI Muonekano wa Mabasi mapya ya Mwendokasi yaliyoletwa na DART

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Sema wenzetu wanajali sana service, professionalism ya uendeshaji, miundombinu gari inayopitia na muda wa chombo kutumika. Gari linaweza kufanyiwa service za kawaida ndani ya miaka 2 basi halitumiki tena, wana expose kabla hata halijabadilishwa chochote, likija huku tunasema gari mpya kabisa. Sisi tunatumia gari mpaka life, ambapo utakuta vitu vyote vilishabadilishwa, huwezi ukakuta spare iliyokuja na gari.
 
hayo mabasi wanadai ni ya nchi jirani nyie bongo endeleeni kusifiana tu wakati mibarabara mnajenga mji mzima lakini magari hamna , yaani wabongo tunaweza uchawa tu na kusifiana ila masuala ya msingi walaaaaaa hatumo.POLENI
 
N kweli yapo mengi. Lakini mimi naona hata Europe yanachakaa haraka sana. Kuna nchi moja niliona walinunua mengi mwaka juzi sasa hivi ni kama yamechakaa hivi.
 
Udart haitunzi mabasi. Viti vinapasuka hakibadilishwi, mabasi hayaoshwi, camera zinaning'inia tu. Wanachojua ni kujaza mafuta tu. Gari likipata tatizo kila mfanyakazi anajifanya fundi.
 
Eeh Mungu usiyeshindwa kitu ninakuomba unipatie gari yangu mwenyewe iwe ist au raumu au wish ila tu isiwe Passo ili hayo magari niyaonee tu yakipita kwa mbaliii. Sipendi Kubanana na lile jasho la mwendokasi. Yani unibariki kama ikitokea nimeyapanda basi iwe kwa kupenda mwenyewe ila sio kwasababu Sina mbadala. Amen
 
Omba pikipiki
 
Maisha yangu yote Dar ila sijawai kufika Tegeta na nisingeamua kwenda bila sababu pia nisingefika Gongo la mboto.

Mtu ukisema hujawahi kufika Mbagala kuna watu wanaona kama kejeli
Binafsi ni kama wewe,siwezi kwenda sehemu bila sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…